Thursday, February 1, 2018

MAISHA YA SHAHIDI PART 1

Asalaam Aleiykum

Leo naanza Darsa kwa kuuliza swali ambalo ntakusaidia kujibu lakini uwe mkweli kabla ya kuendelea kuichambua darsa hii ujiulize Mwenyewe hivyo nilikua najua jawabu.
Swali: Hivyo kama nitakuuliza unajua nini maana ya kufa Shahidi? utanijibu vipi?.

Najua jawabu lako litaegemea kwenye matendo ya huko kufa Shahidi lakini sio maana asilia ya kufa Shahidi, utanambia kufa kwenye vita vya dini, au baharini, au uzazi na hivi na vile, lakini maana na kusudio lenyewe hulijui, basi kuanzia leo utapata maana yake si ya kufa Shahidi tu bali pia ya kuishi kama Shahidi.

Hakuna Jambo gumu kwa Mwanaadamu kama hilo la kuishi Kama Shahidi, Linashindikana jambo hili kutokana na Mwanaadamu kamilikiwa au (Shape)na Jamii au (Community). Kilicho mlea na kumkuza katika maisha yake ni yale mafunzo ya Tabia, hisia na muelekeo mzima wa (Eviroment)anayoishi, (Something very Powerful) Imeota kwa Mwanaadamu huyu inayoitwa (Ego) ambayo imetawala na kuweka kivuli mpaka kufikia kuwa haoni tena au hajui kama yeye ni Shahidi.
Vipi ? atakua Shahidi Wakati katawaliwa na Tabia, vipi awe Shahidi wakati karithi Tabia za Baba na Mama, vipi atakua Shahidi wakati kichwani humo kuna Mwalimu anakaa humo, Umetawaliwa na Kabila lako, umemilikiwa na unaongozwa na Jamii, vipi utakua Shahidi wakati kwenye (Mind) yako umejaa umbea, ndani humo kuna magonvi, wanawake na wanaume wanaishi humo, Dhiki ya maisha imo humo, kila mambo ulojifunza na kuyaona yamejaa humo mpaka umesahau sasa kuwa wewe Roho au Akili.
Kwenye (Stage) ulofikia Akili imeshachukua madaraka Kamili na sasa inaendesha maisha yako huku wewe ukifata Amri yake, Jiangalie kwa undani utaona kila kitu chako kimekua (Influence by the other), Hata hiyo Imani yako ya Dini unayoitegemea Masheikh ndio wameishika, unasikiliza nini wamesema, wewe Mwenyewe umekua huwezi hata kuwasiliana na Mollah wako Mpaka upitie Kwa Masheikh, umeishia unasema mimi naamini lakini hujui unaamini nini.
Na hilo linakutia wasiwasi huwezi kwenda kwa Mollah wako na moyo ulosalimika, Nini kitakacho kujulisha huo moyo ulosalimika?, hakuna chengine ila kurudi ili uwe Shahidi, kumbuka Shahidi ndio pekee anokwenda akiwa salama kwa Mollah wake. Sasa vipi Unakua umetawaliwa, itabidi nikurudishe kwenye Sala uone vipi ushahidi unavokutoka, vipi usingizi ulivokushika, au vipi hiyo (Mind) au Akili inavotawala mpaka ukawa huna ushahidi.
Wewe unapewa vipindi vitano vya Sala kuwasiliana na Mollah wako, Lakini wapi ukisimama kwenye hiyo Sala kitu cha mwanzo chenye kukujia vipi utakula sadaka ya msikitini, dukani umemuacha nani, Leo barazani wamesema nini, Kila ukikaa Akili yako masaa 24 inachambua habari mpya au ya zamani, siri za ngono, au magazeti, vipi mtamfukuza Imam, mbona hasalishi vizuri, hadith fulani inasemaje, leo hakuja kusali na sisi, sala yake haikubaliwi, utaona kadhia hii imejaa misiskitini na makanisani kwa jumla, utaona Mwili(Body)Upo Msikitini lakini (Mind) Akili ipo kwengine kabisa, sasa jiulize hapo Shahidi yuko wapi?
Endelea part 2




MAISHA YA SHAHIDI PART 2

Asalaam Aleiykum

Utaona Mtu anasali miaka 40 hata siku moja hajapata (Something of beyond) Vipi wewe unakua Muumin halafu hupati ishara yoyote, umejiuliza kwanini husogei kwa Mollah wako ukaoneshwa japo taa, Kwani wewe siku zote si unalala Akhera ukiamka duniani?, Baadhi ya wakati huwauliza Masheikh wenu jee wewe kuna chochote kimetokezea kutoka kwa Mollah wako, una dalili yoyote katika maisha yako kwamba utakufa na kufufuliwa, jee umepata alama zozote za Imani yako, au zawadi kutoka mbinguni?, utawaona mashavu yanawacheza hawana la kujibu na hivi ndio sote tunavoishi, na (Quraan) ina tu (Challange) katika sura ya (Dhaariyat aya ya 21 na 22)

"وَفِىٓ أَنفُسِكُمۡ‌ۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ"
"Na Katika Nafsi zenu(Pia zimo Alama)Je Hamuoni"(21)
Alama ziko nyingi mie leo ntazungumza chache ya Alama hizo ambayo imetajwa katika aya hiyo, nini kimetajwa "Jee kwenye Nafsi zenu hamuoni" Hamuangalii, Jiulize nani huyu anayeambiwa ajiangalie, katika kujiangalia lazima viwepo vitu vitatu, ntavitaja ya Mwanzo hiyo nafsi, Yapili hiyo inayoangalia na ya Tatu ni hiyo inayoona viwili hivyo, Na huyo ndio Shahidi au kwa jina lengine hiyo Roho Yako, au kwa njia nyengine "weka Kioo, halafu kutakua na Kioo, ikisha kuna wewe unayejiona kwenye kioo, lakini kuna watatu hapo huyo Shahidi kajificha anatizama kioo na nafsi, ndio maana utaona kwenye kioo umeona nafsi ama (Body)lakini hujamuona Shahidi.
Ulipoambiwa kurejea uwe Shahidi utizame nafsi yako, kusudio lake uwe Shahidi (Complete)Kwani ukiwa Shahidi ndio unasita kutenda dhanmbi kabisa, Shahidi hajawahi kutenda dhanmbi, ndio maana tukiomba dua tunasema (Ewe Mollah Mimi nimeidhulumu Nafsi dhuluma kubwa kabisa naomba unisamehe)hili nitalitolea ufafanuzi kwenye darsa za mbeleni, leo wacha tumchambue Shahidi tuone ana siri gani anataka kutwambia.
Unaendelea na darsa ya Shahidi fanya umuhimu uishi maisha ya ushahidi ili upate kufanikiwa hapa duniani na huko Akhera uendako. Kwa ajili hiyo ndio napenda kukumbusha tena ukisikia Mtu kafa Shahidi maana yake kafa hana Dhanmbi.
Sasa na wewe huna haja ya kufa ukiwa Shahidi unaweza kuishi katika Ulimwengu ukawa na wewe pia Shahidi, kwa maana hiyo utakua matendo ya dhanmbi huyatendi, Na hiyo ndio Darsa yetu ya leo na Faida zake.
Wewe hapo ulipo Maisha yako yote Umefunikwa na Akili, unachotakiwa kufanya ufunue pazia, umeiwachia Akili yako inafanya kazi masaa 24 bila ya mapumziko, mpaka ukilala unasema na kugombana usingizini, sasa umefika wakati uipumzishe (Computer)Chukua madaraka kamili ili uwache kuamuliwa mambo yako na Akili, ndio kwenye hiyo Aya ukaambiwa basi kwenye nafsi zenu hamuoni, na moja katika la kutizamwa ni hii Akili, kwani Akili ni Nyenzo katika nafsi yako, ndio maana wakati wengine unaambiwa wewe hutumii Akili yako.
Wewe Mwenyewe ndio umeifundisha Akili yako kukufanyia kazi zako, si vibaya inafanya zile za muhimu na nzuri, lakini kwa bahati mbaya umeifundisha mabaya vile vile na kwa kuwa Walimu walikuwa wengi ndio maana kichwani umekuwepo mtafaruku mkubwa sana, kutokana na mtafaruku huo ndio umeamua kuiweka kwenye (Automatic mode) ikisha huyo umelala, ninachofanya mimi kukuamsha na kukwambia rejea kwenye (Manual Mode) na ukirejea kwenye (Manual) ndio unakutana na huyo |shahidi ambaye ni wewe Mwenyewe (Original)Jijue wewe ni (Holy) wala Mtu asikwambie vengine.
Sasa Ukitaka kuwa Shahidi ina maana Uchukue (Control)lazima urejee kwenye (Basic)na jambo la mwanzo kufanya huwezi kwenda kwenye (Basic)lazima uisimamishe Akili yako kufanya kazi,(Stop your mind)Ndio maana aya ikatwambia (Hamuoni)kwanini haijasema hamtizami, kwa sababu kutizama ni kitu cha mbali, lakini kuona ni kitu cha karibu, utizame ndani, Kwa kawaida macho yetu yamekua (Trained)au Kufundishwa kuona Nje, Sasa hapo unatakiwa kujifunza kuona ndani, basi ni kitu gani hicho kinotizama ndani na nje?.
Endelea part 3

MAISHA YA SHAHIDI PART 3

Asalaam Aleiykum

Kitu chenyewe kionacho ndani na nje ni hiyo wewe ambayo(Eternal)Roho yako, au Tuite Shahidi.
Hii Roho au Shahidi inaponza kufanya kazi yake ndipo (Mind)au Akili ina (Stop)Na Akili ikisimama ndio inaanza kufata amri zako, Na ukianza Maisha ya Shahidi inakua vigumu kwako kutenda kosa lolote kwa sababu Shahidi ana mahusiano na Mapenzi, toka lini ukasikia Mwenye mapenzi anaua, Mwenye kuua ni yule Mwenye chuki, Kwa sababu Shahidi hajui Uadui, ila Shahidi Akilala Akili au (Mind) ndio inatenda Makosa, ndio maana ukiwa kwenye mapenzi una (Lost your mind)watu wanashikwa karogwa huyo, hajarogwa abadan, anafanya mambo kinyume cha nyinyi wenye chuki, ndio maana mnaona karogwa, mbona anamsomeshea watoto wake, hii kamnunulia nyumba, utajiri wote kamuachia Mwanamke huyo ndio Shahidi(Nimekupa Mfano).
Niliposema Shahidi hajawahi kutenda kosa  ila alikua kalala hapo nilikosea kidogo, kwa sababu huko kulala pia kunategemea Akili(Mind) ndio maana ukiwa Jasiri unaweza kuuona usingizi unapokuvaa, taratibu unapoingia nyayoni unapanda mpaka kwenye Akili yako, lakini unatakiwa Ujasiri(Siku ya mwanzo nilipokua nafanya zoezi hilo nilidhani nakufa mambo yanatisha)
Naam Napenda ujue yakua Shahidi halali, yeye hapati usingizi, Sasa utakua bado unajiuliza ni nani huyu Shahidi?. Wacha nikupe jawabu Shahidi ni yule ambaye Habadiliki ndani yako, kila kitu kinabadilika isipokua Shahidi, toka akae kwenye hiyo Nafsi hajawahi kuondoka, Shahidi huyu hata ukiwa kwenye Usingizi mzito yeye anaangalia(Ndio maana ukaambiwa Uhai)Yeye anaendelea kuangalia ndoto zako, Na hata ukiwa huna ndoto basi yeye anaendelea kuangalia usingizi wako wa nafsi ulio mzito, Na pale unapoamka Shahidi anaendelea kuangalia Ulimwengu, Na unapolala inaangalia Ulimwengu wako wa ndani, Haijawahi kusimama hata sekunde kuangalia mambo yote yanozunguka Ulimwengu wa nje na kwenye nafsi yako, Na ukiijua hali hiyo ya Ushahidi ndipo Akili ina simama na dhanmbi zinatoweka, Na ukifanikiwa kuwa Shahidi ndio utaona Hamaki zinakuja zinapita, matatizo yanakuja yanapita, maradhi yanakuja yanapita, magonvi yanakuja yanapita, Raha zinakuja zinapita, shida zinakuja zinapita, Baridi inakuja inapita, joto linakuja linapita, sio kazi rahisi lakini inawezekana ndio maana tukaambiwa tujaribu kuangalia kwenye nafsi zetu asaa tunaweza kufanikiwa kuona kitu.
Sasa ili ufanikiwe kumpata Shahidi ndio wema walopita wakatafuta mbinu nyingi ili wawe mashahidi, Madhumuni yao yote ilikua kuisimamisha Akili(Mind), Wakaja na (Tasbih)nazitaja baadhi ya nyezo walotumia ambazo leo mnaelezwa haramu, haifai, lakini watu hawakujua nini kusudio la mambo hayo ya kuanzishwa (Dhikiri)Mtu kukaa na udhu, Kusema (Astrafullah)mara elfu kumi, yote ni katika nyenzo ya kuisimamisha Akili, na Akili ikisimama hapo hapo unakutana na Shahidi na huyo shahidi ndio wewe na wala sio mwengine. 
Vipi unaweza kuisimamisha Akili itabidi uisome hiyo aya hapo umepewa (Trick)(Just Watch your Mind)ndio katika nafsi zenu hamuoni, anza kidogo kidogo kujiangalia vipi unakula, vipi unazungumza, ukiwa kimya isikilize akili yako inavoongea, ukikoga fanya upate hisia ya mwili wako, punguza kuongea kama mchiriku, Ukisali sikiliza Quraan unayosoma, jaribu kurejea kwenye Nafsi yako kidogo kidogo utaona Akili ina (Dissappear) na Shahidi ana (Appear).
Hapo ndio tunaingia aya ya pili, kumbuka huwezi kuingia aya hii mpaka umekua Shahidi.
"وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ
"Na Katika Mbingu ziko riziki zenu na mliyoahidiwa"
Kumbuka ukifanikiwa kuwa Shahidi Muono wako wa Ulimwengu huu unabadilika, Na hapo unaanza kufunguliwa baadhi ya siri, ndipo unapokutana na ukweli wa ithbati kuwa katika hiyo Mbingu ndiko kunako gaiwa Riziki yangu, mimi hata nikifanya nini siwezi kuzidisha wala kupunguza vile ambavyo inavoamriwa huko Mbinguni riziki yangu iwe ya kiasi gani, ndio utaona yule ambaye anauza mchanga anatajirika na wewe Mwenye kuuza dhahabu bado umasikini, Na hapo inakufungukia yakini kuwa siku uhai wangu utakapomalizika basi na mimi ntaelekea huko Mbinguni katika kupata yale nilohaidiwa."Mollah wetu tujaalie Maisha ya Ushahidi na utufanye katika watakaopata pepo yako Mollah wetu".
Amin.