Saturday, March 3, 2018

KIMYA KINAFUNDISHA PART 1

Asalaam Aleiykum

Kuna Msemo wa Kiswahili Naupenda sana japokua wasemaji wameupa maana nyengine lakini kwenye Ulimwengu wa Mafundisho una maana kubwa kabisa, "Msemo Wenyewe unasema hivi, "Asofunzwa na Mamae hufunzwa na Ulimwengu".
Niliposema naupenda nilikusidia ulivotamkwa kwa maandishi yake, lakini  kwa maana  halisi naupinga kwa nguvu zangu zote kwa kusema hakuna Mwenye kufunzwa na Mama, Nitaukubali msemo huu ukitamkwa "Asosomeshwa na Mamae atasomeshwa na Walimwengu".
Napenda ukumbuke hayo yote alokua nayo Mama na yeye kasomeshwa, huo ni Urithi kutoka kwa Wazee wake, Darsa yangu hii nataka nikuondoshe kwenye Urithi nikupeleke kwenye Mali yako Mwenyewe, Nisafishe matope ili upate kuishuhudia (Diamond) wewe Mwenyewe.
Wameniletea Swali wananiuliza Umesoma wapi?, Mwalimu wako nani?, Umesoma Chuo gani?, Nimefurahi wameniuliza Umesoma wapi ni rahisi kuwajibu, lakini wangeniuliza umejifundisha wapi hapo ningekua na Mashaka makubwa kujibu swali kama hilo. Lakini (One Thing)naweza kusema nina uhakika sijasomeshwa na Mama yangu, Kwa hilo naogopa kumtia Aibu Mama yangu kwani Walimwengu watasema Mama yangu alikua Mwalimu mbaya, Lakini niko tayari kuwalaumu Walimwengu kwani wao ni Walimu wabaya sana, Takriban mabaya yote nime(Copy)kutoka kwao, kutokana na hilo naweza kusema nimesomea kutoka kwa kila mtu nilokutana naye katika maisha yangu.
Nini Kusoma?, Kusoma ni kukusanya (Information) za kuweza kukusaidia katika shughuli zako za kawaida, ama ukitaka kuzijua za  kawaida ni huko ku(Copy)tabia, na kikazi katika kupata ajira ilo bora ili utende kazi kwa ufanisi na ujuzi mahiri kwa kile ulichosomea, ndio Maana unaambiwa somea (Biology)uwe (Doctor)Somea (International Relation)utakua Balozi, huko ndio kusoma.
Lakini kufundishwa ni (More Deep), kufundishwa inahusiana na (Life)maisha, kwa hiyo katika kufundishwa lazima vipatikane vitu vitatu(Soul)Roho, (Body)Mwili na (Mind)Akili ndio unaweza kuitwa yule kafundishwa. Sasa vipi hii Kufundishwa ina Mahusiano na hiyo sauti ya(Ukimya)ambayo hutaki kuisikiliza na kila mara unakumbushwa sauti hii ipo , na ndio inayo kufundisha, lakini wewe husikii kwa kuwa ume (Invest) kwenye makelele zaidi, ndio ukakumbushwa kwenye sura ya Muumin aya ya (3).
"وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ"
Na Ambao hujiepusha na Mambo ya Kipuuzi.
Mambo ya kipuuzi ni hizo kelele za mazungumzo, mtazamo wa kipuuzi, kelele za nyimbo na mengineo, Kwanini ikawa hivyo kwa sababu wewe una (Tape Record) na hiyo ndio inokufanyia zogo ukawa husikii sauti ya ukimya.Sasa ufanye nini ili upate kuijua na kuisikiliza na kuifahamu hiyo sauti ya (Ukimya)inokufundisha?.
Endelea part 2


KIMYA KINAFUNDISHA PART 2

Asalaam Aleiykum

Kinachotakiwa kifanyike itakubidi urudi uwe kama mtoto (Empty cassette)vipi utafanya inabidi ujitenge na makelele kwa njia unazozijua Mwenyewe, utakapo jitenga na mambo ya kipuuzi yaliyo nje hayaingii ndani kidogo kidogo utaanza kufuta yaliyomo(Record)ya ndani kwenye kichwa chako.
Ukifanikiwa kufuta makelele yaliyomo ndani ndio kidogo kidogo utaanza kusikia sauti yenye kufundisha, Sauti ambayo inakutoa kwenye Kiza na kukupeleka kwenye Nuru, Na hapo ndio utakapo pata maana halisi ya aya iliyomo kwenye sura ya (Insaan aya 2 na 3)
إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا
Kwa hakika tumemuumba Mtu (Mwanaadamu)kutokana na Mbegu ya Uhai iliyochanganyika, ili tumfanyie Mtihani, kwa hivyo tukamfanya ni Mwenye kusikia na kuona.
"Wacha nikupe habari"Wewe hapo ulipo unazo hizo mbegu za uhai uwe mwanamme au mwanamke, zinakupa (Energy)unaishi nazo ndani ya Mwili, ndio maana ukimaliza tendo la ndoa unakua taabani, ndio maana usingizi wake unakua kama kifo, kwa sababu umepoteza mbegu, uhai umepungua (Ndio maana unaambiwa usifanye mambo ya uzinifu sana utakufa mapema), Naam kwa hiyo tukamfanya Mwenye kusikia na kuona, kwa kawaida tendo la kusikia unakua unasikia vitu vya nje hata siku moja hujasikia vya ndani, Hujapata kusikia moyo wako unavopiga, ila ulipokua mdogo ndio ulikua  unasikia vizuri, lakini kwa sasa ni mara chache unasikiliza sauti ya ukimya, Ama ukisikiliza sauti hii utagundua ndio ilokufundisha mambo mengi"(عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ )"Alomfundisha Mwanaadamu chungu ya Mambo asoyajua.
Nani alokufundisha kulia, ukafundishwa kunyonya, ukafundishwa kutambaa, ukafundishwa kutembea, nani huyo ushapata kujiuliza?. Basi kabla ya kujiuliza jitizame Binaadamu wewe ujio wako kwenye Ulimwengu,(Aya Ya Mwanzo kwenye sura hii ya Insaan) Imekutaja wewe kama Mbegu, Wewe na Mti hamna Tafauti nyote Mmeumbwa, Mbegu ya Mti inatiwa chini ya tumbo la Ardhi baada ya muda inatokeza juu kwa kuchipuka na kuwa Mti, Mti huo unakua mkubwa unatoa majani na matunda, na mbegu zinotoka kwenye matunda hayo zinatawanyika kwenye ardhi hapo tena inaota miti mengine."Kama umesoma uzuri hicho kipande hapo juu cha hadithi ya Mti" basi utakua umepata fundisho na huo ndio mfano wa kufundishwa mambo mengi na Mollah wako, hicho hapo kitakua kitendo cha kutizama maisha ya mti, (Hiyo itakua sifa yako ya kuona).
Na wewe Mwenyewe unapitia (System)kama hiyo unaanza Kwenye Mbegu unatiwa kwenye tumbo ikisha watu wanasubiri miezi tisa ili utoke mtoto tumboni, unaishi unakua mkubwa unazaa na unaleta familia yako nyengine kabisa, basi ukiyajua hayo basi elewa kuna (System) Nyengine yenye kufundisha huo mti vipi kutafuta maji, vipi utakula, na (System) hiyo hiyo ndio inokufundisha wewe mambo mengi usoyajua, Jiulize kwa umakini hiyo miaka yako ulokaa (School au University) ndio ilokufundisha mambo yote unayoyajua, ikiwa sio basi jee elimu hii inatokea wapi?. 
Ndio Mwenye enzi Mungu akasema ikisha tukamjaalia kusikia na kuona, sasa kwanini ikaanzwa kusikia mwanzo? 

Endelea part 3 

KIMYA KINAFUNDISHA PART 3

Asalaam Aleiykum

Pale mwanzo nilitaja kuwa wewe uko sawa na mti sasa hapa nakutajia sababu za wewe kunyanyuliwa juu zaidi kwa mapenzi ya Mollah wako, Aliposema "Tukamjaalia kusikia na kuona", Unajua kwanini kusikia ikaanzwa mwanzo, kwa sababu kuona hata wanyama wanaona lakini kusikia inaenda (Deep)kusikia ni nyenzo ya wewe kufahamu au kujua (Mollah) wako anasema nini, hapo ndipo uliponyanyuliwa, lakini kumbuka unaweza kuona usifahamu ni kitu gani, na unaweza kusikia pia ukawa hujui wamesema nini, ukiwa katika hali hiyo basi jijue wewe bado uko kwenye fungu la wanyama, Lakini ukianza kusikiliza sauti ya ukimya ukaifahamu ndio unaondoka kidogo kidogo kwenye Unyama unaanza kuwa Binaadamu, sasa ukitoka kwenye Ubinaadamu unatakiwa uingie kwenye kundi la Muumin, hapo ndipo inaanza safari ya aya ya pili inayosema:"إِ نَّا هَدَيۡنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرً۬ا وَإِمَّا كَفُورًا"
"Hakika sisi tumemuongoa (Kwenye)njia Basi (Akitaka)atakua Mwenye shukurani au Mwenye kukufuru".
Vipi Uongofu huo unapatikana?. Unapatikana kwa kusikiliza sauti hiyo ya ukimya, unaposafisha (Noise) zako utaanza kusikia, vipi unasafisha mwanzoni nimezitaja na hapa naongezea, kuwa mtulivu fanya yalo mema, ukisha kuwa msafi hakuna ufisadi, wala tamaa au chuki kwenye moyo wako ghafla utaanza kusikia Sauti ya Ukimya inakufundisha, ukipata (Direct contact)utaona wewe Mwenyewe unaanza kufahamu, unaacha dhuluma, unaacha kulewa, unaacha kuzini, unaacha kusema uongo, unaanza kusali, unatoa sadaka, unasaidia maskini, wapi uongofu huu umetokea?, lazima kuna kitu kinakufundisha hichi nifanye na hichi nisifanye na hiyo ndio kauli ya tumemuongoa kwa kumfundisha na kumuonesha muongozo wenye kuambatana na khiyari katika hiyo (Roho)yako, ikisha ukapewa hiyari, baki kama mnyama ukufuru au kuwa Muumin ushukuru.
Na huko kushukuru ni kutambua kuwa Mwenye enzi Mungu kaniongoa mimi kumfata yeye kwa uwezo wake, kilichotakiwa kwangu ni kusikiliza tu anaamrisha nini, Yeye ndie aliyeniita kwenye njia ya Ufalme wake kwa Uwezo wake Mwenyewe, mbona kuna wenzangu bado wako kwenye maasi, mbona kuna wenzangu wanadhulumu watu, Lakini Mimi nafurahi kwa ajili ya Mollah wangu kunionesha njia hii ya kheri nikaifata. Siwezi kukufuru mie nikasema eti kwa uwezo wangu nimekua mtiifu, isipokua kataka Mollah wangu kwa Rehma zake kanifanya niwe Mwenye kusikiliza na kutii Amri zake, Na kwa ajili hiyo Naamini Mwenye enzi Mungu ndie Mwenye kunionesha njia hizi za kheri, kwa nguvu za ajabu kaniweka mimi katika njia hii wala sipepesuki namsikiliza yeye pekee.
Basi alo Muumin wa kweli anawaombea Yaarab Wajaalie na wengine wenye kuusikiliza wito wako wa ukimya na wauelewe na kuufata  Amin.