Saturday, March 3, 2018

KIMYA KINAFUNDISHA PART 1

Asalaam Aleiykum

Kuna Msemo wa Kiswahili Naupenda sana japokua wasemaji wameupa maana nyengine lakini kwenye Ulimwengu wa Mafundisho una maana kubwa kabisa, "Msemo Wenyewe unasema hivi, "Asofunzwa na Mamae hufunzwa na Ulimwengu".
Niliposema naupenda nilikusidia ulivotamkwa kwa maandishi yake, lakini  kwa maana  halisi naupinga kwa nguvu zangu zote kwa kusema hakuna Mwenye kufunzwa na Mama, Nitaukubali msemo huu ukitamkwa "Asosomeshwa na Mamae atasomeshwa na Walimwengu".
Napenda ukumbuke hayo yote alokua nayo Mama na yeye kasomeshwa, huo ni Urithi kutoka kwa Wazee wake, Darsa yangu hii nataka nikuondoshe kwenye Urithi nikupeleke kwenye Mali yako Mwenyewe, Nisafishe matope ili upate kuishuhudia (Diamond) wewe Mwenyewe.
Wameniletea Swali wananiuliza Umesoma wapi?, Mwalimu wako nani?, Umesoma Chuo gani?, Nimefurahi wameniuliza Umesoma wapi ni rahisi kuwajibu, lakini wangeniuliza umejifundisha wapi hapo ningekua na Mashaka makubwa kujibu swali kama hilo. Lakini (One Thing)naweza kusema nina uhakika sijasomeshwa na Mama yangu, Kwa hilo naogopa kumtia Aibu Mama yangu kwani Walimwengu watasema Mama yangu alikua Mwalimu mbaya, Lakini niko tayari kuwalaumu Walimwengu kwani wao ni Walimu wabaya sana, Takriban mabaya yote nime(Copy)kutoka kwao, kutokana na hilo naweza kusema nimesomea kutoka kwa kila mtu nilokutana naye katika maisha yangu.
Nini Kusoma?, Kusoma ni kukusanya (Information) za kuweza kukusaidia katika shughuli zako za kawaida, ama ukitaka kuzijua za  kawaida ni huko ku(Copy)tabia, na kikazi katika kupata ajira ilo bora ili utende kazi kwa ufanisi na ujuzi mahiri kwa kile ulichosomea, ndio Maana unaambiwa somea (Biology)uwe (Doctor)Somea (International Relation)utakua Balozi, huko ndio kusoma.
Lakini kufundishwa ni (More Deep), kufundishwa inahusiana na (Life)maisha, kwa hiyo katika kufundishwa lazima vipatikane vitu vitatu(Soul)Roho, (Body)Mwili na (Mind)Akili ndio unaweza kuitwa yule kafundishwa. Sasa vipi hii Kufundishwa ina Mahusiano na hiyo sauti ya(Ukimya)ambayo hutaki kuisikiliza na kila mara unakumbushwa sauti hii ipo , na ndio inayo kufundisha, lakini wewe husikii kwa kuwa ume (Invest) kwenye makelele zaidi, ndio ukakumbushwa kwenye sura ya Muumin aya ya (3).
"وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ"
Na Ambao hujiepusha na Mambo ya Kipuuzi.
Mambo ya kipuuzi ni hizo kelele za mazungumzo, mtazamo wa kipuuzi, kelele za nyimbo na mengineo, Kwanini ikawa hivyo kwa sababu wewe una (Tape Record) na hiyo ndio inokufanyia zogo ukawa husikii sauti ya ukimya.Sasa ufanye nini ili upate kuijua na kuisikiliza na kuifahamu hiyo sauti ya (Ukimya)inokufundisha?.
Endelea part 2


No comments:

Post a Comment