Asalaam Aleiykum
Pale mwanzo nilitaja kuwa wewe uko sawa na mti sasa hapa nakutajia sababu za wewe kunyanyuliwa juu zaidi kwa mapenzi ya Mollah wako, Aliposema "Tukamjaalia kusikia na kuona", Unajua kwanini kusikia ikaanzwa mwanzo, kwa sababu kuona hata wanyama wanaona lakini kusikia inaenda (Deep)kusikia ni nyenzo ya wewe kufahamu au kujua (Mollah) wako anasema nini, hapo ndipo uliponyanyuliwa, lakini kumbuka unaweza kuona usifahamu ni kitu gani, na unaweza kusikia pia ukawa hujui wamesema nini, ukiwa katika hali hiyo basi jijue wewe bado uko kwenye fungu la wanyama, Lakini ukianza kusikiliza sauti ya ukimya ukaifahamu ndio unaondoka kidogo kidogo kwenye Unyama unaanza kuwa Binaadamu, sasa ukitoka kwenye Ubinaadamu unatakiwa uingie kwenye kundi la Muumin, hapo ndipo inaanza safari ya aya ya pili inayosema:"إِ نَّا هَدَيۡنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرً۬ا وَإِمَّا كَفُورًا"
"Hakika sisi tumemuongoa (Kwenye)njia Basi (Akitaka)atakua Mwenye shukurani au Mwenye kukufuru".
Vipi Uongofu huo unapatikana?. Unapatikana kwa kusikiliza sauti hiyo ya ukimya, unaposafisha (Noise) zako utaanza kusikia, vipi unasafisha mwanzoni nimezitaja na hapa naongezea, kuwa mtulivu fanya yalo mema, ukisha kuwa msafi hakuna ufisadi, wala tamaa au chuki kwenye moyo wako ghafla utaanza kusikia Sauti ya Ukimya inakufundisha, ukipata (Direct contact)utaona wewe Mwenyewe unaanza kufahamu, unaacha dhuluma, unaacha kulewa, unaacha kuzini, unaacha kusema uongo, unaanza kusali, unatoa sadaka, unasaidia maskini, wapi uongofu huu umetokea?, lazima kuna kitu kinakufundisha hichi nifanye na hichi nisifanye na hiyo ndio kauli ya tumemuongoa kwa kumfundisha na kumuonesha muongozo wenye kuambatana na khiyari katika hiyo (Roho)yako, ikisha ukapewa hiyari, baki kama mnyama ukufuru au kuwa Muumin ushukuru.
Na huko kushukuru ni kutambua kuwa Mwenye enzi Mungu kaniongoa mimi kumfata yeye kwa uwezo wake, kilichotakiwa kwangu ni kusikiliza tu anaamrisha nini, Yeye ndie aliyeniita kwenye njia ya Ufalme wake kwa Uwezo wake Mwenyewe, mbona kuna wenzangu bado wako kwenye maasi, mbona kuna wenzangu wanadhulumu watu, Lakini Mimi nafurahi kwa ajili ya Mollah wangu kunionesha njia hii ya kheri nikaifata. Siwezi kukufuru mie nikasema eti kwa uwezo wangu nimekua mtiifu, isipokua kataka Mollah wangu kwa Rehma zake kanifanya niwe Mwenye kusikiliza na kutii Amri zake, Na kwa ajili hiyo Naamini Mwenye enzi Mungu ndie Mwenye kunionesha njia hizi za kheri, kwa nguvu za ajabu kaniweka mimi katika njia hii wala sipepesuki namsikiliza yeye pekee.
Basi alo Muumin wa kweli anawaombea Yaarab Wajaalie na wengine wenye kuusikiliza wito wako wa ukimya na wauelewe na kuufata Amin.
No comments:
Post a Comment