Asalaam Aleiykum
Kinachotakiwa kifanyike itakubidi urudi uwe kama mtoto (Empty cassette)vipi utafanya inabidi ujitenge na makelele kwa njia unazozijua Mwenyewe, utakapo jitenga na mambo ya kipuuzi yaliyo nje hayaingii ndani kidogo kidogo utaanza kufuta yaliyomo(Record)ya ndani kwenye kichwa chako.
Ukifanikiwa kufuta makelele yaliyomo ndani ndio kidogo kidogo utaanza kusikia sauti yenye kufundisha, Sauti ambayo inakutoa kwenye Kiza na kukupeleka kwenye Nuru, Na hapo ndio utakapo pata maana halisi ya aya iliyomo kwenye sura ya (Insaan aya 2 na 3)
إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا
Kwa hakika tumemuumba Mtu (Mwanaadamu)kutokana na Mbegu ya Uhai iliyochanganyika, ili tumfanyie Mtihani, kwa hivyo tukamfanya ni Mwenye kusikia na kuona.
"Wacha nikupe habari"Wewe hapo ulipo unazo hizo mbegu za uhai uwe mwanamme au mwanamke, zinakupa (Energy)unaishi nazo ndani ya Mwili, ndio maana ukimaliza tendo la ndoa unakua taabani, ndio maana usingizi wake unakua kama kifo, kwa sababu umepoteza mbegu, uhai umepungua (Ndio maana unaambiwa usifanye mambo ya uzinifu sana utakufa mapema), Naam kwa hiyo tukamfanya Mwenye kusikia na kuona, kwa kawaida tendo la kusikia unakua unasikia vitu vya nje hata siku moja hujasikia vya ndani, Hujapata kusikia moyo wako unavopiga, ila ulipokua mdogo ndio ulikua unasikia vizuri, lakini kwa sasa ni mara chache unasikiliza sauti ya ukimya, Ama ukisikiliza sauti hii utagundua ndio ilokufundisha mambo mengi"(عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ )"Alomfundisha Mwanaadamu chungu ya Mambo asoyajua.
Nani alokufundisha kulia, ukafundishwa kunyonya, ukafundishwa kutambaa, ukafundishwa kutembea, nani huyo ushapata kujiuliza?. Basi kabla ya kujiuliza jitizame Binaadamu wewe ujio wako kwenye Ulimwengu,(Aya Ya Mwanzo kwenye sura hii ya Insaan) Imekutaja wewe kama Mbegu, Wewe na Mti hamna Tafauti nyote Mmeumbwa, Mbegu ya Mti inatiwa chini ya tumbo la Ardhi baada ya muda inatokeza juu kwa kuchipuka na kuwa Mti, Mti huo unakua mkubwa unatoa majani na matunda, na mbegu zinotoka kwenye matunda hayo zinatawanyika kwenye ardhi hapo tena inaota miti mengine."Kama umesoma uzuri hicho kipande hapo juu cha hadithi ya Mti" basi utakua umepata fundisho na huo ndio mfano wa kufundishwa mambo mengi na Mollah wako, hicho hapo kitakua kitendo cha kutizama maisha ya mti, (Hiyo itakua sifa yako ya kuona).
Na wewe Mwenyewe unapitia (System)kama hiyo unaanza Kwenye Mbegu unatiwa kwenye tumbo ikisha watu wanasubiri miezi tisa ili utoke mtoto tumboni, unaishi unakua mkubwa unazaa na unaleta familia yako nyengine kabisa, basi ukiyajua hayo basi elewa kuna (System) Nyengine yenye kufundisha huo mti vipi kutafuta maji, vipi utakula, na (System) hiyo hiyo ndio inokufundisha wewe mambo mengi usoyajua, Jiulize kwa umakini hiyo miaka yako ulokaa (School au University) ndio ilokufundisha mambo yote unayoyajua, ikiwa sio basi jee elimu hii inatokea wapi?.
Ndio Mwenye enzi Mungu akasema ikisha tukamjaalia kusikia na kuona, sasa kwanini ikaanzwa kusikia mwanzo?
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment