Sunday, April 15, 2018

KIVULI CHA MAUTI PART 3

Asalaam Aleiykum

Alama yetu ya pili kukijua kivuli hichi ni aya iliyomo sura ya Yaasin aya ya 68.
"وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَڪِّسۡهُ فِى ٱلۡخَلۡقِ‌ۖ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ "
Na tunayempa Umri (Ikisha)tunamrejesha nyuma katika umbo lake basi jee hawayatii Akilini(Kuzingatia).
Alama yakua sasa kivuli kinaondoka ni kupoteza kwako kwa uwezo wa mambo mengi katika Mwili wako, unatakiwa uyazingatie kuwa hivi karibuni safari itawadia ya wewe kuondoka kwenye (Maisha) na hicho kiitwacho (Mauti) viwili vyote hivi vinatoweka, na dalili zipo nyingi tunapewa ili tujiandae, viwili hivi vinaondoshwa kidogo kidogo pasi wewe kushituka, Ama kwenye maisha huwezi kwenda mbio, nywele kuwa nyeupe, huwezi harakati nyingi, Maradhi yanawasili kutokana na muda wa viungo kutenda kazi ushamalizika, na katika kadhia ya (mauti)mpaka usingizi una punguziwa, ukiona vitu vyote hivi vimewasili basi elewa sasa wakati wowote unatarajiwa urejee nyumbani, unatakiwa kulala ule usingizi wa moja kwa moja, uondoke kwenye Uhai, upite kwenye mauti ili urejee nyumbani kwa aliyekuumba.
Yote hayo yanafanyika lakini kuna kitu unakiona kivuli chake bado kipo, daima jitizame ukiumwa, ukiwa mzee, kuna kitu kinakujulisha kiko (The same)hakibadiliki, Kitu hicho kitu gani daima kipo na wewe kwa mfano wa kivuli, siku utakapo kigundua kivuli hicho ndio siku yako ya kurudi nyumbani, tegemeo langu utapokelewa kwa salama na Msamaha kutoka kwa Mollah wako kama alivosema Mwenyewe kwenye sura ya Mulk aya hiyo ya pili.

No comments:

Post a Comment