Sunday, April 15, 2018

KIVULI CHA MAUTI PART 1

Asalaam Aleiykum

Katika sura ya (Mulk)kumetajwa mambo mawili ambayo yanapaswa tuyazingatie kwa undani, Maneno yenyewe ni haya "Mwenye enzi Mungu ameumba Mauti na maisha" viwili hivi vimetuzunguka na tunaishi navyo lakini wengi hatuna ujuzi wa kuvijua.
Leo umefika muda wa kujua kikoje kivuli hicho cha Mauti, Na kwanini naishi nacho halafu nikawa sikijui. Sasa Kabla ya kuendelea na darsa yetu napenda kukupa dondoo ya "Kivuli cha Mauti" ili nipate kukujulisha vilivyomo pembeni mwa "Kivuli"hicho.
Wewe Mwanaadamu yaweza kuwa pengine umeghafilika au hujui kabisa pembezoni mwa kivuli cha Mauti kuna kaa nini, Ukiangalia vizuri katika umri huu ambao unaishi katika Ulimwengu huu kuna hesabu ya Namba 7 imekuzunguka, kama Mbingu 7 na Ardhi mfano huo huo wa 7, Basi na maisha yako pia yamezungukwa na Namba hiyo ya 7, kila baada ya miaka 7 maisha yako yanabadilika ndani na nje kuanzia Riziki mpaka maumbile, ukitaka ushahidi wa hilo lifanyie uchunguzi nakujulisha wapi kwa kuanzia, rudi nyuma ulipozaliwa mpaka ukafika miaka saba ulikua unaishi ndani ya kivuli hujali kitu, huna fahamu, huogopi kufa wala chochote, ulipoanza kufika miaka saba ukaanza kupewa fahamu kidogo kidogo ndio maana hekima ya kuambiwa watoto wakifika miaka saba wafundishwe kusali, kufunga, wakiachiwa kipindi hicho kama hakijatiwa kitu kwenye Akili wakakizoea basi watakua hawafahamu tena, Sasa ilipofika saba ya pili(14) unafunguliwa raha ya (Sex).
Ulipofika Miaka (21) Pengine umemaliza (Uni au School)Ukaolewa au ukaoa, na ulipoingia saba ya nne(28)sasa unakabidhiwa utu Uzima na hapo ndio kidogo unaanza kukutana na Kivuli, unaanza kujua kumbe jua litakuchwa, kuna usiku utanivaa, kivuli kinakuja na hivyo ndio Mauti yanapowasili kwa kujitambulisha umebakiza muda sio mrefu na mimi nichukue nafasi yangu. 

No comments:

Post a Comment