Friday, May 4, 2018

DARSA YA RAMADHAN PART 3

Asalaam Aleiykum

وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ 
"Na Jambo gani litokujulisha Nini huo Usiku Wa Laylatul Qadir"
Kuna baadhi ya watu hapa wanasema ni kushushwa kwa Quraan kwenye (Lahwi Mahfoudh)Sasa ikiwa Mwenye Kufahamu utajua kuwa huko Mbinguni hakuna Mchana wala Usiku, ilipotajwa Usiku kusudio lake (Usiku huu Wenye Heshima wenye Nguvu) Ni ule Usiku Aloteremshiwa Bwana Mtume s.a.w Hii Quraan. 
Sasa Kwanini ukaambiwa nini kitokujulisha Wewe Usiku huu?. Hapo inaonesha unatakiwa Wewe kuujua Usiku huu, Lakini Kujua na kujulishwa ni mambo mawili tafauti kujua itakua kama wengine unajua kuwa Usiku huu umo ndani ya Ramadhan, kwa Mwaka mara moja tunapita ndani ya Usiku huu, Lakini Kujulishwa hapo ni ile (Experience)ukotokezee Usiku huu ndani ya Nafsi yako.

لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٌ۬ مِّنۡ أَلۡفِ شَہۡرٍ۬ 
"Huu Usiku wa Heshima(Nguvu)ni Bora kuliko Miezi Elfu"
Hapa kuna Tafsiri Mbili inabidi tuzipitie, Umo katika Darsa ya Ramadhan pata faida ya kujua mambo ili upate mafanikio. Tafsiri ya kwanza "Kama utaupata Usiku huu" basi hata kama kama utaishi hiyo Miaka 83 basi haiwi bora kama Usiku huu, Ibada zote ulizozifanya na kheri zote unozijua wewe hazifanani na Usiku huu.
Ama Tafsiri ya Pili (ambayo wengine wameitetea kuwa ndio sahihi)"Usiku huu ukiupata (Power)yake au Nuru yake inotokozea kwenye Roho yako ni kupita miezi elfu imurike kwa pamoja kwenye Ulimwengu huu, hapo ndio likapatikana kwa Wale walo (Experience) Wakaita Nyota ya Jaha", Mtu hajui la kusema anaona kageuka Nuru juu ya Nuru, Ndio Maana utaona hata katika ule Mlima nje kidogo ya Makka alipopewa hiyo Quraan Bwana Mtume s.a.w kwa mara ya Mwanzo panaitwa (Jabar Noor).

تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيہَا بِإِذۡنِ رَبِّہِم مِّن كُلِّ أَمۡرٍ۬ 
"Huteremka Malaika na Roho (Za viumbe watakatifu)katika (Usiku)huo kwa Idhini ya Mollah wao kwa kila Jambo."Hapo ndipo niliposema Ukiipata ile (Total Union)Basi unapata cheo cha Utakatifu(Pure Born again)Unakua safi kama ulozaliwa leo, "Ndio maana ikasemwa ni Bora kuliko hiyo miaka 83 utakayoishi". Unakua Umesamehewa ungali uhai na unapewa Nguvu fulani na uwezo fulani inakua hata Binaadamu wenzio wanahisi kuna mabadiliko fulani, mara utasikia dua yake hairudi, yule ana (Makarama) na hivi na vile.
Unapata hayo kwa ajili ya Idhin ya Mollah wako.
 سَلَـٰمٌ هِىَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ 
"Ni Amani (Usiku)huo mpaka mapambazuko ya Alfajiri".
Ukiamka unakua (New Man Transform)(Your past is gone).
Naam tulikua tunachuma tunda sasa wacha turejee kwenye Mzizi wenyewe wa Mti wa Saum. Sasa Neno Funga linatajwa siku zote unalisikia na kulisoma lakini pengine hujawahi kwenda (Deep)ukalifahamu maana yake, Funga kwa Mwanaadamu imekusudiwa uzuie kitu kisiingie ndani.
Sasa utajiuliza kwanini Mwanaadamu anatakiwa afunge, Unatakiwa Ufunge kwa ajili urejee kwenye (Basic)yako ya Maumbile, Au Msingi wako wa Kuumbwa, au kupatikana ile (Separation) Niloitaja mwanzo (Ya Dongo kavu linotoa sauti na Roho yako).Sasa vipi unatakiwa Ufunge uipate hiyo Taqwa, au utoke kwenye Dongo urudi kwenye Roho,(Ndio maana Ramadhan ikaitwa Ustaadh Mwenye kulea Roho)hapo kuna Mambo (4)lazima uyapate ili funga yako itimie, Na funga ikitimia basi (Automatic) unakutana na Taqwa. Napenda Uelewe hiyo Taqwa inatokea au unaijua au imo ndani ya kifua chako, wakati wakuipata Wewe ndio utakua Shahidi wa hilo, Na ukishuhudia kuwa umeipata Taqwa basi moja kwa moja Jijue Sauwm yako imekubaliwa Na Mollah wako Mlezi.
Mambo gani hayo yanotakiwa katika hiyo funga?.
Unapewa darsa hii kabla ya Ramadhan ili na wewe Uwe katika walofunga mwaka huu, Mambo gani hayo (4)Yanokuchukua kukupeleka mji wa Saum ili kuitafuta hiyo Taqwa. (1)Jambo la kwanza unotakiwa ulifunge ni Chakula , Nini kinatokea?, Unaponyima (Body) Mwili wako chakula unaupa (Shock)nini kimetokea, mbona huyu hatupi huduma yetu, hapo mwili unatoka kwenye (Automatic mode)unakwenda kwenye (Manual) unaanza kujihudumia wenyewe kwa kwenda kwenye (Akiba)zake, ukianza kwenda kwenye Akiba ndio unapita kila pahala kutizama wapi kumeharibika, wapi kuna vuja unaanza kujikarabati(Kujitibu)ndio ukaambiwa kufunga siha.
(2)Jambo la pili Baada ya chakula usiruhusu kitu kuingia Mwilini mwako, kama (Sex)na mengineyo kwani yataishughulisha (System) yako isijue inafanya nini.
(3)Jambo la Tatu Ni Mashikio na Macho Usisikilize Nyimbo(Music)Mambo machafu, Habari za Uongo, na vyote vibaya vyenye kupita kutumia sauti, na jicho lisitizame mambo ya kidunia yenye (Munkar) Funga vipasha habari vyote (Tv, wassup, facebook, instagram)hama kwenye mwezi huu.
(4)Na jambo la nne ambalo ndilo litaweza kukujulisha nini hiyo Taqwa ni hili la kuzungumza, ukiweza jiepushe kuongea sana kwani ukiongea sana una(Miss)yanotokea kwenye nafsi yako, kwa sababu hukai kimya, ukikaa kimya unaweza "Kuona Mawazo yako yanavo zaa Maneno, Na Maneno yako yanakua vitendo, Na vitendo vyako vinakua tabia, Na Tabia yako ndio inakua (Nembo) yako fulani (Mchiriku)kweli, anaongea sana, Na Mtu Mkimya pia anatajwa fulani hazungumzi, basi katika Mwezi huu na wewe kuwa asiyezungumza, hapo ndio utakapoipata Saum kwa kujizuia kuongea sana kama alivosema Bibi Maryam kwenye (sura ya Maryam aya 26)
فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلۡبَشَرِ أَحَدً۬ا فَقُولِىٓ إِنِّى نَذَرۡتُ لِلرَّحۡمَـٰنِ صَوۡمً۬ا فَلَنۡ أُڪَلِّمَ ٱلۡيَوۡمَ إِنسِيًّ۬ا
"Na kama ukimuona Mtu yoyote (akakuuliza habari ya mtoto huyu)Sema Hakika mimi nimeweka Nadhir kwa (Mollah)Mwingi wa Rehma ya Kufunga, Kwa hivyo leo sitosema na Mtu".
Naam na wewe jizuie, kuongea sana, ndio maana mkaambiwa ikisha Mkakae msikitini(Kimya) Kumbuka kila kitu kinatokea kwenye Ukimya, ukijizuia na vyote hivyo Akili inakua haina la kufanya, Na Akili ikisimama Taqwa inatokezea na hiyo ndio Saum. Mollah wangu ni Mwenye kujua zaidi, Nakutakieni Mwezi wa Kheri na Baraka na saum zenye kukubaliwa, Mollah atujaalie Ufalme wake sote tuingie katika pepo yake, Atusameh dhanmbi zetu zilopita za sasa na zinokuja, Awasamehe pia walotangulia kabla yetu awatilie nuru katika makaazi yao huko walipo. 
Amin.

No comments:

Post a Comment