Friday, May 4, 2018

DARSA YA RAMADHAN PART 1

Asalaam Aleiykum

Hutaki nikupe siri itakayokufanya Funga yako iwe bora na yenye kukubaliwa na Mollah wako, Hupendi wewe kuwa na furaha moyoni mwako kwa kujua Mwaka huu kwa mara ya mwanzo nimeipata Taqwa, huna hamu yakuwafahamisha wengine yakwamba funga iko namna hivi, basi ikiwa Mwenye kuyataka hayo wacha nikufahamishe sababu za weye kuambiwa ufunge.
Tuliza macho kwenye darsa hii nikuchukue katika safari fupi ili upate kunifahamu vizuri.
Siku zote Masheikh wanaanza na aya hii iliyomo sura ya (Baqarah aya ya 183)
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ 
"Enyi Mloamini Mmelazimishwa Kufunga kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu".
Wacha nikuchukue  twende kwenye Bustani tukachume tunda la Saum na hakuna kwengine lilipoanzia Tunda hili ila huko Mbinguni pale Mwenye enzi Mungu alipowaambia Malaika kwenye sura ya (Hijr aya ya 28 na 29)
وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ إِنِّى خَـٰلِقُۢ بَشَرً۬ا مِّن صَلۡصَـٰلٍ۬ مِّنۡ حَمَإٍ۬ مَّسۡنُونٍ۬ 
"Na Mollah wako alipowaambia Malaika, Hakika Mimi nitamuumba Mtu(Binaadamu) kwa Udongo Mkavu unaotoa Sauti, Wenye kutokana na matope meusi yalovunda".
فَإِذَا سَوَّيۡتُهُ ۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُواْ لَهُ ۥ سَـٰجِدِينَ
"Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia Roho inayotokana na Mimi, basi Mumuangukie kwa kumtii(Sujud)".
Hapo kwenye aya hizo mbili kuna mambo lazima uyatupie macho upate faida zake, Mambo yepi?, la kwanza lenye kuonesha udhaifu wako kuwa wewe ni udongo mkavu unaotoa sauti, tena ulovunda ndio maana ukifa unaanza kutoa harufu.
Na hiyo aya ya Pili inakupandisha daraja kubwa yakuwa wewe ni Roho iliyotokana na Mwenye enzi Mungu, basi nitakapomaliza kumuumba poromekeni kumtii, msujudieni hichi kiumbe changu. Sasa jambo la mwanzo kujitambua wewe ni (Khalifa)wala usikubali mtu mwengine akakwambia vengine, kwa hayo unayotenda labda itakua dunia imekulevya, Na umejisahau kama wewe ni (Khalifa) katika Ardhi hii.
Hili neno (Khalifa)likazie macho sana lina maana kubwa katika Darsa hii ya Ramadhan. Naam sasa umeshajijua kwamba wewe ni (Khalifa)na hapa Ulimwenguni unapita tu, (Ndio maana Mtu akifa tunasema sote ni wa Mwenye enzi Mungu na kwake tunarejea) ilipotajwa kuhusu (Khalifa)"Malaika kwenye aya ya (30)Sura ya (Baqarah)"wakasema Utaweka humo watakaofanya Uharibifu humo na kumwaga damu,"Mwenye enzi Mungu akawajibu"Hakika Mimi nayajua msiyoyajua".
Sasa hapo Malaika walijuaje kuwa tutafanya visa Ardhini, Jawabu ni kutokana Majini walotutangulia walileta uharibifu kwenye Ardhi hii, Mollah wetu akatufundisha na anaendelea kutufundisha chungu ya Mambo yaliyomo kwenye Ardhi hii, haya ma(Computer)magari,meli,Madege, kila machine iliyomo kwenye Ardhi hii ni kutokana na elimu anayotufunulia yeye na sisi kuweza kutekeleza. Sasa haya yote yamehusiana nini na Saum. 
Endelea part 2


No comments:

Post a Comment