Asalaam Aleiykum
Nini Jamaa?
Jamaa maana yake ni ku(Unified oneness together) kwanini ikawa hivyo, Quraan (An Nisai aya 1).
يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٍ۬ وَٲحِدَةٍ۬ وَخَلَقَ مِنۡہَا زَوۡجَهَا وَبَثَّ مِنۡہُمَا رِجَالاً۬ كَثِيرً۬ا وَنِسَآءً۬ۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِى تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلۡأَرۡحَامَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيۡكُمۡ رَقِيبً۬ا
"Enyi Watu Mcheni Mollah wenu ambaye amekuumbeni katika Nafsi Moja, Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile, Na akaeneza Wanaume wengi na Wanawake kutoka katika wawili hao, Mcheni Mwenye enzi Mungu ambaye kwake (Mnaomba)Mnaombana, Na Muwatazame Jamaa, Hakika Mwenye enzi Mungu ni Mlinzi juu yenu".
Vipi inakua, nakupa nafasi ili na wewe uijue Sala ya Jamaa kwa njia ya Tawhid, Nyinyi jiangalieni kwanza kwa njia ya nje vipi mlivo fanana hakuna tafauti, uwe mweupe au mweusi uwe kabila au dini yoyote lakini nyote mefanana katika Maumbile, Wanaume wako sawa na Wanawake wote wako sawa, Na hali hiyo hiyo ndani yenu pia Meungana kama Nafsi moja ila hamjachunguzana, kama utajaaliwa kupewa macho ya Mcha Mungu ukaiona Miujiza ya Roho utaona kumbe sote tuna Nafsi Moja, Kumbe mimi na yule ndani yetu ni kitu kimoja.
Mollah wetu huyo huyo Mwenye Kuamrisha wewe uzaliwe na Kufa ndie Yeye Mwenye kuamrisha Mwengine azaliwe na kufa kwa njia hiyo hiyo, Nani Mwenye kukupa Wewe uwezo wa kuona ndio alompa Jirani yako, ndugu yako, rafiki yako, Mzee wako uwezo huo huo wa kuona na kusikia, Nani Mwenye kutupa sote kwa pamoja uwezo wa Kuhema bila ya Amri yetu isipokua yeye Mollah wetu anatupa kwa pamoja tunahema bila ya masharti sote tukiwa chumba kimoja, pumzi ndani pumzi nje, nini habari yetu sisi kama zitazuiliwa zisije tena.
Hiyo nakupa kwa uchache ili upate kujua kumbe sisi wanaadamu sote ni (One Unity)ulichokua nacho wewe na mwenzako ana hicho hicho, ukishagundua hilo basi kuna mabadiliko yatatokea katika Nafsi yako, Na Wakati huo ndio utajua kwanini unasali Sala ya Jamaa. Utaelewa Umuhimu wakuwa na Imam Muadilifu, utatambua vilevile Wakati unasali Sala za Eid, au Sala ya Alfajiri, Magharib na Isha umuhimu wa kuitikia Amin, utaiona vipi Aamin yenu inavofungika na kutoka kwa pamoja na mkanyamaza kwa pamoja bila ya kufanya (mazoezi) yoyote ya jambo hilo.
Vipi utajua Umeipata Sala ya Jamaa pale Fikra zitakapotea, Moyo utakapo jaa ghushuu, na kama Sala ya kutoa Sauti utaona unaisikia kwa njia ya Moyo sio kichwani, na Kama ikenda (Deep)utaona machozi yanakulenga lenga, hapo utajijua umeipata Sala ya Jamaa na hata ikimalizika huna haja yakutoka mbio Msikitini bado (Energy)ya Sala iko na wewe, na hata ukitoka bado unaendelea kuwemo katika hali ya Ucha Mungu. Ukiyapata hayo ndio inakua Sala imekutokezea wewe kwenye Nafsi, Na ndio inaweza kukuepusha Na Machafu, Madhanbi, Viburi na mengineyo hapo ndipo utafahamu nini Tafauti ya Sala ya Msikitini na Sala ya Jamaa.
No comments:
Post a Comment