Friday, June 15, 2018

SALA YA JAMAA PART 2

Asalaam Aleyikum

Naam nini Nia?, Nia ni kusudio la kutenda jambo, sasa swali wapi kusudio hili linaishi na vipi linakuja mpaka likawa hai?. Tendo hili la Nia linaishi kwenye (Moyo) hiyo ni kwa lugha nyepesi, Kwa lugha ngumu tutaita kwenye (Roho) au lugha ya sayansi tuite (Subconscious)yako.
Ndio Maana hadith maarufu ya (Mtume s.a.w)ikasema "Hakika ya Amal yoyote ni kwenye Nia yako", Unaweza kuingia kwenye Ibada bila ya kutamka chochote, hiyo ni sawa na vizuri sana, lakini kufanya hivyo kuna shuruti lazima wewe uwe katika wale wenye kutajwa wanamkumbuka Mollah wao wakiwa wamesimama au kukaa au wamelala, hao wanaweza kufanya Ibada zao bila ya manuizi, kwa sababu wao wakati wote wako pamoja na Mollah wao, lakini matatizo yanakuja pale mimi na wewe ambao nusu tumelala na nusu tuko macho, sisi nini tunatakiwa tufanye inabidi tuamshwe, ndio ikawekwa Adhana, kukumbushwa wakati wa sala, halafu inatubidi mimi na wewe tukurupuke sio kama hatujijui ila tunafanya manuizi ili kuunganisha (subconscious na conscious)kumbuka dakika tano zilopita ulikua pengine unatizama mpira au kusikiliza nyimbo, kwa hiyo ili uipate Sala yako kikamilifu unaondoka kwenye (Conscious)ya kusikiliza mazungumzo unaipeleka kuungana na kile kilichokuja kika kukumbusha sasa hivi kusali, ikiwa utakwenda kwenye sala bila ya kujipiga nyundo, na hivyo ndio unavotakiwa ufanye kutokana na mfundisho ya kuto kunuia, basi utajikuta kwenye hiyo Sala hujajisaidia chochote ila unaendelea kufunga mahesabu, au unapanga miadi au unaendelea kusikiliza nyimbo ndani ya sala, unapata upande sala upande nyimbo au mazungumzo.
Nikisema hivyo bado wengine watakua na wasiwasi wa jambo hilo, basi wacha nitoe mfano wa Msahafu au juzuu nzima unayo umehifadhi, unakwenda Msalani au(Chooni)haziji zenyewe zile sura mpaka utake kuzisoma, zipo (somewhere)lakini wakati ule huzihitaji kwa hiyo haziji kwenye (Conscious)yako mpaka utake.
Sasa Ulimi unahusika vipi?, ipate darsa hii ili upate kufahamu vizuri kwanini unatia nia tena kwa sauti, na hao waloleta waligundua nini katika hili?. Ulimi kwa njia ya kuitamka (Nia)una kazi mbili, Kazi ya kwanza unaiamsha Akili yako kukaa tayari kwa Ibada, kwa sababu huwezi kusema huku ukawa unafikiri, lichunguze hilo utabaini mwenyewe, Na jambo la pili kujulisha viumbe vyengine (Kama Malaika)na vyengine avijuavyo Mollah wako kwamba sasa wewe unaingia ndani ya Ibada, Ulimwengu na vilivyomo vinakusikia(Napenda uelewe sauti yako inabaki milele haipotei kabisa) Ndio maana utaona kwenye Ibada zote tunatoa sauti, ingekua Ulimi hauna nafasi basi kwenye Sala ilikua haina haja ya kutamka chochote, ila tungesema (Hakika ya Ibada zetu kwenye nia) hapa sina haja ya kupinga kauli zote mbili nazikubali za kutamka na kuto tamka zinakubalika na wala hazina mushkeli inategemea na daraja yako upo katika (Level)gani ya Kumkumbuka Mollah wako, Na wala hakuna makosa katika hilo.
Halafu kabla ya kuingia katika hiyo Sala ya Jamaa unaingia katika jambo la pili, kumbuka jambo la kwanza ni nia, Na hili la pili ni (Tohara Udhu), kusafisha Mwili wako kwa ajili ya kwenda kuungana na Mollah wako.
Na katika Udhu kuna mazingatio makubwa vile unavojisafisha kiwiliwili chako, inokwenda kusali ni Roho yako, lakini vipi utakwenda wewe na guo lilochafuka kwa Mollah wako, ndio hapo unaingia Udhu, unasafisha Mikono (Symbolic) kama kiwiliwili hichi kimeshika vya haramu, au Uso na macho vimeona vya haramu, au miguu ilipita au kwenda kwenye haramu, au masikio yalisikia vya haramu sasa mimi najisafisha ili kusogea na kuungana na Mollah wangu nikiwa safi. Sasa tutaingia katika sala Ya Jamaa,
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment