Asalaam Aleiykum
Ametukuka yule aliyeumba Nafsi moja ikisha Akutajaalia Fahamu, Namuomba atupe Fahamu ya kuelewa kuwa kwenye enzi yake sote tuko sawa na hatuna tafauti, Ila kuna ubora kwa yule atakaye mpenda Mollah wake zaidi na kumtii.
Kabla ya kuingia kwenye darsa hii kuna kitu napenda nifahamishe ili msije kuifananisha darsa hii na darsa ya (Sala ya Msikiti), kwa sababu kuna baadhi ya watu wanaona kuwa (Kaka na keki)ni neno moja, kumbe ni maneno mawili tafauti na wala hayana mahusiano.
Kwenye hii darsa ya (Sala ya Jamaa)tunakwenda kuchambua jambo lengine kabisa lenye faida na wewe ikiwa utalizingatia, Kwanini nikasema hivyo, kwa sababu unaweza kwenda Msikitini kusali lakini usisali sala ya "Jamaa" ila ukasali sala ya "Msikitini".
Najua unashangaa, ni vizuri kushangaa ndio mwanzo wa kujua, huko ndio kuweka wazi mifupa ya fahamu ili (Nipate kuifanyia Operation). Kufanya hivyo utapata kuelewa vizuri ipi Sala ya Msikitini na ipi sala ya Jamaa, Sasa tuingie kwenye darsa, Ipi Sala ya msikitini?, Sala ya Msikitini ni ile ambayo wengi wetu tunakwenda tukifika hapo tunasalishwa na "Maimam" wenye viburi, au ana mambo sio mema kwenye jamii yalochanganya kila kitu, na nyinyi mnajua ila mnanyamaza kimya na kumuachia aendelee kukuongozeni kwenye Sala zenu, Au Nyinyi wenyewe mna "Viburi"(Ego)Huu Msikiti wetu wa kundi fulani, unakwenda kwenye nyumba hiyo ya Ibada unanuia kusali Rakaa nne na katika manuizi yako unanuia maamuma japo unajua Imam ana mushkeli fulani, au una yakini hapa ninaposali haruhusiwi Imam au Sheikh Mwengine kusalisha, isipokua awe mtu wenu, hiyo ndio Sala ya Msikitini, ambayo sio mbaya ila utalipwa kama (indivisual) na sio Jamaa.
Halafu kuna aina nyengine ya Sala ambayo leo tutapiga mbizi ili tuogelee kwenye hii Sala ya Jamaa tuone ikoje Sala hii halafu utaamua mwenyewe unataka kusali sala ya msikitini au sala ya Jamaa, uamuzi ni wako wewe, basi kabla ya kuchupa kwenye bahari hiyo wacha tupate faida mbili tatu za baadhi ya mambo ili upate kujua, usije ukakatazwa usifanye kumbe vina faida na wewe.
Kuna baadhi ya makatazo unakatazwa na wewe bila ya kufikiria unayakubali hata hujiulizi ni faida yake, kama kutia nia kuna clip zinasambazwa kukataza jambo hilo, sawa hatukatai lakini wacha na sisi kabla ya kukataa tuangalie kwanini jambo hili lililetwa?.
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment