Asalaam Aleiykum
Binaadamu ukipata bahati ya kwenda (Beyond) ya viwili hivyo utafika pahala yaani (Akili na Sense) utapata maarifa ya kuwa (Super Being) kwanini nikasema maarifa kwa sababu Akili haipo tena, sense hazipo tena, unabahatika wakati Mwengine kwenye usingizi wako, ukajiona unapaa unakwenda sehemu za ajabu lakini kama nilivosema unakua hujui nini kimetokea, hujui ni kweli au ndoto, lakini umeona mambo ya ajabu na unashindwa kuyaeleza, na tafauti ni hii ukiweza kuhadithia basi ujue ni ndoto, na ukishindwa kuhadithia basi ni hiyo daraja ya (super being).
Mambo hayo hayo unayaokutana nayo yakawa hayana maelezo, hujui useme nini na hayo hayo yako kwenye huu mfano hai, ambao kwa sasa unafahamu unaishi lakini hujui (Source)yako ya maisha, hujawahi hata siku moja kufanya maulizo ya maisha yako, wewe na mnyama mnaishi sawa sawa, tafauti moja mnyama hajui kama atakufa wewe unajua, lakini hujapata kujiuliza nini haya maajabu ya uhai, nini (source)yake kwanini na lala nikiamka?.
Ukipata Ushujaa wa kuanza kwenda katika maulizo hayo ya nini uhai, ndipo utajikuta kwamba wewe sichochote, unaishi ndani ya hiyo "(Qadir)ya Mwenye enzi Mungu alosema akitaka jambo liwe linakuwa". Utaanza kujua kidogo kidogo kumbe mimi hata uwezo wa kuhema sina ila Mwenye enzi Mungu wangu ndio Mwenye kunifanyia Neema hii ya kuvuta pumzi, utauona udhaifu wako, hata kuzaliwa kwako utaelewa kuwa umeletwa hapa duniani, utaacha kufanya (Birthday)zote, utashangaa ukijua kumbe kukutana kwa watu wawili kwa njia ya mapenzi ndio limetokea tukio la mimi kuja Ulimwenguni humu. Utafahamu uzuri zaidi ikiwa pumzi mpaka atake Mwenye enzi Mungu basi na huo Utajiri au Akili ulizonazo basi (Source)yake ni Mwenye enzi Mungu, yeye ndio anosababisha kila jambo katika Ulimwengu huu.
Ukiona unajenga majumba, unasaidia Maskini, unanunua magari basi ujue sio wewe kuna (Source)inayokuwezesha ili uwe hivo, Kwa Mapenzi ya Mollah wako umechaguliwa wewe kwa muda kushika madaraka hayo, ndio maana kuna msemo (Tumekuja bila ya kitu na tutaondoka bila ya kitu).La Muhimu (Find yourself) halafu ishi katika (Being)yako, hapo ndio kwenye makaazi ya Taqwa, hutegemei Akili tena katika kuishi ila Unamtegemea Mollah wako, hapo Kiburi kitaondoka, chuki haikai tena, Tamaa huna tena, mahitaji ya dunia utayapa mgongo, na kila kitakachotokea utakua unajua kwa uhakika kimetoka kwa Mollah wako na utakua Mwepesi wa kupokea, utakua umeunganisha maisha yako baina ya Ardhi na Mbingu una (Dis-Appear) ungali uhai, na hiyo ndio (Bliss).
No comments:
Post a Comment