Asalaam Aleiykum
Binaadamu tunaishi katika kiza kikubwa cha (Sahau) Ndani ya kiza hiki tunavishana vyeo vya kila aina, vyengine vya utajiri, umasikini, ushujaa, uhodari, na kadhalika lakini tunasahau Udhaifu wetu sisi kuwa hatuwezi kutenda lolote bila kupewa fursa hiyo na Mwenye enzi Mungu. Walimwengu tunajinasibu na mambo mengi tuyafanyao lakini tunasahau kuwa sio sisi wenye kutenda, Na linalotufanya kusahau ni kile kiburi cha sisi kumsahau yule alotuumba akatujaalia uwezo wa kutenda.
Kuna mambo mingi ya mfano ambayo kila ukenda (Deep)kwa kuyatafakari utajikuta kuwa sisi wanaadamu ni viumbe dhaifu kabisa na wenye kumtegemea Mollah wetu kwa kila kitu.
Hakuna kitu chenye kunipa furaha kama nikitafakari na kuisoma sura ya (Al-Qalam)aya ya 1-2, "Naapa kwa Kalamu, Na wayaandikayo (Kwa kalamu hiyo)""Kwa Neema ya Mollah wako wewe si Mwendawazimu".
Sasa nikiangalia Akili naona ni kitengo maalum cha Mwanaadamu kuwasiliana na Ulimwengu wa Nje, Na hii ni Neema kubwa kutoka kwa Mollah wetu, Na wala haukua huu ni wenda wazimu, ila wazimu tunajitia wenyewe pale tunapokwenda kinyume na kuandika yasotakiwa(Ita Dhanmbi, haramu)utaamua Mwenyewe mimi niko naogelea kwenye darsa ya Ajabu ya Maisha na hapa leo nakutana na ajabu hizo ambazo nimechagua ni (Share) na wewe.
Naam Ikiwa Akili kazi yake kuandika na kurekodi, basi lazima vipatikane vitu vyengine vyenye kuwasiliana na Akili(Medium)au vipeleka habari. Ukiwa unakubaliana na mimi tuendelee part 2 tupate habari zaidi ya (Ajabu ya Maisha).
No comments:
Post a Comment