Tuesday, July 31, 2018

MAAJABU YA UHAI PART 2

Asalaam Aleiykum

Vitu hivyo vyenye kuwasiliana na Akili vimepewa jina na kuitwa ( 5 Sense)"Kuona, kusikia,kutaste,kunusa na kugusa" vyote hivi vina(Report)kwenye Akili, Akili kazi yake kuandika au kurecord, Sasa ikiwa Akili inapelekewa kila kitu ina maana Akili ni nyenzo kama nyenzo nyengine za kutendea kazi katika Mwili wako, Tukiweza kuitenga Akili au kuiweka pembeni lazima tukubaliane kuzifata hizo (Sense)tujue nazo zinapata wa nguvu au uwezo wa kuripoti kwa Akili.
Inatubidi tujiulize nini (Source) yake, iweje hata tunaweza kuona, kusikia, kuhisi,kugusa,kutest, ni lazima kuna (Original source)ambayo inatoa (Command) hizo, na kama ipo basi itakua ndio inotuma (Massage) kwenye (Sense) na (Sense) ndio inapeleka (Massage) kwenye Akili, Na ni lazima hii (Source) iwe (Advance) kuliko (Sense) kuliko Akili yenyewe, kazi kubwa Mwanaadamu inatakiwa uifanye kuijua hii (Original source) Na Maajabu ya hii (Source)daima imejificha.
Ukiweza kuifahamu hii (Source), kwanini nikasema kuifahamu, kwa sababu ningesema kuijua ingebidi nitumie Akili, vitu vyote vinojulikana unatumia Akili, lakini visivojulikana inatumika Fahamu, ndio maana yakaitwa Maajabu, kuna vitu vinatokea havikai kwenye (Memory) unashangaa ilikuaje ikatokea vile, hesabu, maana zote zinapotea, huna (Reason) kabisa ya kuhusisha kilochotokea na maisha ya kawaida unabaki kunyamaza kimya huko ndiko kufahamu.
Ukiona unajua basi hiyo imetokea katika dunia ya Akili, kumbuka siku zote kujua kumehusiana na Akili. Naam Kwa hiyo hicho ninachozungumza sio cha Ulimwengu huu, hiyo (Source) huwezi kuigusa, huwezi kuiona, huwezi kuihisi lakini unafahamu hii (Source) ni Mimi, kama vile ukiamka unavojifahamu nimeamka, lakini cha ajabu ukilala hujifahamu kama umelala?, unajua kwanini kwa sababu ukiamka unatumia Akili kujua kuwa umeamka, mara moja moja ukiamka ghafla, au umeshituka bado hujawasiliana na Akili utajikuta unajiuliza mie nani, niko wapi hapo hujapata (Contact) ya kujua, lakini unajifahamu mie kitu fulani(The Being).
Sasa utatupa shida ukitaka tukufahamishe wewe nani, kwa sababu wakati unalala (Sense) zinaondoka lakini wewe uko pale pale.
Endelea Part 3

No comments:

Post a Comment