Friday, May 4, 2018

DARSA YA RAMADHAN PART 2

Asalaam Aleiykum

Mwanaadamu ukijua cheo chako kikubwa ulichopewa na Mwenye Enzi Mungu utakua furahani Milele, ndio maana (Ibilisi)akasema laa siwezi kumsujudia kiumbe huyo. Tizama vipi Mwanaadamu thamani yako ilivyo, ndio sasa katika Mwezi huu wa Ramadhan unaitwa, lakini sio wote wenye kuitwa ila wale (Masikini kwenye Ibada)wale wenye kuutaka Ucha Mungu ndio watakao rithi Ufalme au Pepo ya Mwenye enzi Mungu.
Kwanini ikawa hawa tu ndio watarithi kwa sababu wao wameamini, ndio maana aya ya kuamrisha kufunga haikusema Waislamu kwa sababu lazima iwepo Imani ndio uweze kufunga, sasa hawa wenye kuamini wanakubali kwa karibu zaidi Mwenye enzi Mungu yupo na Amri zake zipo lakini hawajui vipi kuipata yakini hiyo, ndio imeletwa Ramadhan ili utoke kwenye Imani upige hatua ya kwenda kwenye Taqwa au (Uthibitisho).
Na hiyo ni (Stage)ya Pili kabla ya kuingia ile ya tatu ya (Ushuhuda au Shahid) au wengine wanaita (Truth). Kwa hiyo hapo Wanaitwa "Enyi Mloamini"Njooni mpate kufundishwa nyinyi hamjui kitu, kuna mambo mawili ndani ya hii Ramadhan, yepi mambo hayo Mawili?, Umo kwenye darsa ya Ramadhan fanya hima ujiandae uwape habari njema na wenzio ili na wao wapate faida ya kufunga.
Ama hilo jambo la kwanza ndio hilo Wasomi wanalipigia kelele, funga utapata Afya, funga Mwili(Body)inajitibu yenyewe, kila kitu kinaambatana na body, (Unakumbuka kule Mwanzo Mwenye enzi Mungu aliposema Ntamuumba kwa udongo mkavu unotoa sauti)basi naam hiyo ni sehemu katika sehemu moja ya hii kuamrishwa kufunga, ila kuna sehemu hii ya pili wengi hawajui, hawajapata (Ushahidi)(Truth)Na hichi cha pili ndio sababu kuu ya Ramadhan.
Kitu gani hichi cha pili?.
Kumbuka Miezi yote kumi na moja umezama kwenye mambo ya dunia, umemsahau Mollah wako, ndio katika Mwezi huu Mmoja Mollah wako kakuita "Ewe Kiumbe"changu rudi kwa Mwezi huu mmoja uwe na mimi, Nini (Saum)? Saum ni (Union with god) hiyo ndio Taqwa, Khalifa anakutana na Mfalme wake.
Nini kitapatikana iwapo Khalifa huyu atafunga inavotakiwa?.
Hapa itabidi nieleze faida itakayo patikana hapa Ulimwenguni, Ama ile ya Akhera ajuwae yeye Mollah wetu, Ama hapa Ulimwenguni zipo faida Mbili, ya kwanza  yule Mwenye kupata (Union)na Mollah wake, na hiyo ya pili ya yule Mwenye kupata (Total Union).
Ama yule Mwenye kupata (Union)tu, yule atakua kapata hiyo Taqwa, na huyo pekee ndie Mwenye kuweza kuhadithia lakini kwa dalili tu naweza kukwambia yanatokezea (Mapenzi)kwenye nafsi yako na mfano wake (Kaisome aya ya 177 sura ya Baqarah)ndio utajua, sio mapenzi haya ya kawaida ya kumpenda Mwanamke au vitu bali inakuwa (Total love) hiyo ndio Taqwa, inakuaje, wewe unajua vipi mapenzi yanavoingia katika Akili, sasa Taqwa ndio inakua mapenzi ya Mollah wako na wewe ndio unaingia katika ile aya ya "Wanaomkumbuka Mollah wakiwa wamesimama, wamekaa mpaka wakiwa wamelala" ukiipata hali kama hiyo hapo ndio Taqwa inakua ime (Happen) na hicho ndio kinachotakiwa katika Ramadhan ukipate(Focus)yako yote iwe kwa Mollah wako.
Hazikutoki fikra za Mollah wako hata mara moja na uwepo kokote pale, uwepo Mpirani au senema uwepo harusini au kwenye futari Mollah wako haondoki tena kwenye mawazo yako, ikikuta hali kama hiyo basi utaona unafatiwa na furaha na manukato ya kheri unangara kwa wanaadamu wenzio.
Ama yule Mwenye kupata (Total Union)Yeye anapotea kabisa anakua mtu mwengine kabisa, kauli zake ni zengine kabisa, Nuru yake ni nyengine kabisa(Feeling)zake nyengine anaishi kwenye (Bliss)utamuona (Something of beyond happen) kitu chenyewe ni hiyo ilotajwa  kwenye sura ya (Al-Qadir).
"إِنَّآ أَنزَلۡنَـٰهُ فِى لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ "
"Hakika Tumeiteremsha(Quraan) kwenye Usiku wa Heshima(Wa Nguvu)"(Usiku wa Ramadhan)
Nini hicho kiloteremshwa katika usiku huo ni hii Quraan, aliyoteremshiwa Bwana Mtume s.a.w. lakini kuna mengine yamo humo huwa yanateremshwa ambayo nitafafanua yametajwa kwenye sura hiyo.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment