Sunday, April 15, 2018

KIVULI CHA MAUTI PART 2

Asalaam Aleiykum

Unapotaka kufahamu ukweli wa Kivuli hicho kwanza lazima upite kwenye Muongozo wa kitabu cha Quraan aya ya pili iliyomo sura ya (Mulk) inayosema.
ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلاً۬‌ۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ
"Ambaye ameumba Mauti na uhai ili kukujaribuni, ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri, Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Msamaha".
Nakuomba zama au nenda (Deep)lazima utakutana na vitu viwili Maisha na Mauti, katikati ya mambo hayo mawili ndio kuna hicho kivuli, Sasa tuliza Akili yako nikuchukue kwenye Umahiri wa lugha ili upate kujua vipi unaishi katika viwili hivi. Napenda ufahamu kuna kitu kimoja hichi kiitwacho uhai, hiki wewe una uhakika nacho, ukiamka unajijua mimi niko hai, lakini nina hakika hujawahi kujiuliza nikilala nakwenda wapi, au niko katika hali gani, au naishi vipi?.
Nakuomba ukae ulizingatie swali hilo ambalo ndani yake kuna mazingatio makubwa kabisa ambayo sio ya Ulimwengu huu. Aya inasema "Yameumbwa Mauti na Uhai"Jee unaishi katika viwili hivi?, Na kama unaishi ile (Final)ambayo hurejei tena inaitwa nini?Ikiwa kuna Uhai au haya (Maisha)tunayoyajua basi elewa unaishi pia katika kitu kiitwacho(Mauti)ndio maana ukaambiwa viwili hivi vimeumbwa na vinaenda sambamba, kila ukenda kulala unakwenda katika hiyo awamu ya pili ya (Umauti), nisije kusema hivi ukaja kudhani zile ndoto zako ndio Ulimwengu wa (Mauti) huwezi kuufikia Ulimwengu huo mpaka upewe Hijjaza na Mollah wako, au ufanye mazoezi uweze kuuona usingizi wako.
Utakapoona usingizi wako ukashuhudia Mwili wako umelala na wewe tafauti na kiwiliwili chako una uangalia, hapo utajua nini maana ya hilo kusudio la "Kivuli cha Mauti", Ndio maana nikasema ukitegemea ndoto utakua bado unaishi kwenye Akili, Na itakua kama jua limepatwa giza limetanda, Na ukitaka kujua kwamba bado uko kwenye Akili zitizame ndoto zako zitakujulisha pale unapoota mtu wako alokufa, siku zote utamuona katika umri wa ujana au alivokua mtoto, Ni kwa sababu hiyo ndoto yako inatokea kwenye (Memory), Lakini ukimuona kwenye hali ambayo ya hivi sasa basi hapo itakua umekwenda(Beyond).
Nimesema kuna njia mbili za kuangalia hiki kivuli ama ile ya kwanza ni usingizi ambayo ni ngumu sana kwetu sisi kupata habari zake. Ama njia ya pili ni hii iliyomo kwenye sura ya.
Endelea part 3.

No comments:

Post a Comment