Friday, August 31, 2018

SHAHIDI WA SHUHUDA PART 1

Asalaam Aleiykum

Jee umeshawahi kukutana na Shahidi wa Shuhuda?.
Basi ikiwa hujakutana nae Wacha nikuchukue katika safari ili tukamtafute huyu Shuhuda, Kwanini nikaitaja Safari kwa sababu safari ni muhimu sana katika kugundua mambo mepya, usikubali kukaa sehemu moja utakua hugundui au kujifunza mambo mepya, Ndio Maana Nabii Musa a.s akaambiwa nenda kwa Mja wetu tulompa elimu, Na wewe usikae pahala pamoja na ukasoma kitabu kimoja utakuja kuondoka Ulimwenguni hapa huna faida hata moja, nenda kasome pita ukitafuta huku na kule asaa kuna siku na wewe utafunguliwa Mlango wa Shuhuda, Na utakapo ingia katika Jumba la Shuhuda unakua Mtu Mwengine kabisa. Kila Mmoja wetu anao uwezekano huo ila tunashindana kati juhudi ya kuutafuta mji huu wa Shuhuda.
Leo nimeanza darsa yangu kwa kukuletea mfano wa safari, Ikiwa wewe Mweupe au Mweusi ntakupeleka Mji usika ili usipoteze lengo, Basi wacha tuanze na Mtu Mweusi kama nilivyo mimi, Kama wewe Mweusi Fikiria nimekutoa Tanzania nimekupeleka (Nigeria)katikati ya Jiji la lagos, huna Jina, hujui lugha, wala mtu yoyote yule, Na wala hao watu hawakujui umetokea wapi, (Label)zote zimepotea, Nini Habari yako itakua katika mji huo wa kigeni?. Hilo litakujulisha jambo moja kwamba kwenye Kwenye Ulimwengu huu Wewe umekuja huna Jina, huna Lugha, Hujui chochote, Ama kuhusu majina unapewa na Wazazi wako (Label)kama begi vile, ili ukitaka kutumwa au kusomeshwa wapate kukutambua, ikisha wanakurithisha na Lugha ili mpate kuwasiliana wanaita (Mother Tongue) vikikamilika hivyo sasa wanakupeleka (School)huko Shule ndipo unakwenda kuliwa nyama, umechunguza wewe kwamba huko (School) ndio unatumia masaa mengi kuliko nyumbani, hapo tena wanaijaza Akili yako mpaka ikijaa, wanakukabidhi kwenye Jamii ambako nako inafanyika kazi ya wewe Uishi vipi, kunaigia fujo ya kila aina mpaka unachagua kujijua na kujinata mie (Fulani) au nimetoka nchi fulani.
endelea part 2

SHAHIDI WA SHUHUDA PART 2

Asalaam Aleiykum

Ukifika hapo "Mwenye enzi Mungu" anakuzindua ili ikuondoke Ari na kiburi na jeuri ilokuingia anakukumbusha (Quraan-Hujarat aya 13).
"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ۬ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَـٰكُمۡ شُعُوبً۬ا وَقَبَآٮِٕلَ لِتَعَارَفُوٓاْ‌ۚ إِنَّ أَڪۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَٮٰكُمۡ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ۬ "
Enyi Watu Kwa hakika tumekuumbeni(nyote) Kwa Mwanaume(Mmoja Adam)Na Mwanamke (Mmoja Hawa) Na tumekufanyieni Mataifa na Makabila(Mbali mbali) ili mjuane, Hakika ahishimiwaye sana Miongoni mwenu Mbele ya Mwenye enzi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenye enzi Mungu ni mjuzi, Mwenye habari (za Mambo yote).
Naam Maneno yana mazingatio makubwa, Unajulishwa wewe ni kiumbe ima uwe mwanamke au mwanaume hapa kwenye Ulimwengu huu huna chako, vyote vimezibitiwa na Mollah wako, umekuja Ulimwenguni hapa huna hata jina, na hayo mlopewa Utaifa au huo Ukabila wako ni njia ya kukufanya mjuane, msije mkapigana vikumbo, kwa sababu nyinyi ni viumbe, Umekuja Ulimwenguni hapa hata nguo hukuvaa, hushangai pale mtoto akizaliwa anaitwa nani? (Nameless)ni Mgeni au kiumbe kilovamia Dunia hii na kime(Surrender)kiumbe hiki kuna watu wata (Take care)Basi Nakukumbusha na siku yako ya kufa pia kuna Viumbe upande wa pili wana (Take care) tena kama ulivokuja mara ya mwanzo.
Hivyo vitu ulivyo navyo ni kwa Matumizi ya (Temprory) kwenye Ulimwengu huu, Sasa unatakiwa ufanye nini khasa ikiwa hivi vyote ni vitu vya mpito, Hapo ndio inaingia Maana ya Dini. Dini Mafundisho yake utafute Ukaribu na Mollah wako, ndio inaitwa (Taqwa)lakini vipi utapata ukaribu na Mollah wako wakati hupo karibu hata kwako Mwenyewe, Kuipata (Taqwa) lazima uwe umefika katika ( A state) au hali ya Ushuhuda, sasa swali vipi unakutana na hali hiyo ya Ushuhuda, ndipo unapoambiwa Shahidi kashuhudia.
Endelea part 3

SHAHIDI WA SHUHUDA PART 3

Asalaam Aleiykum

Hapa sasa ndio tunaingia katika Muujiza wetu wa Shuhuda, Wewe Binaadamu ni (unique Being)Na katika hiyo (Being)yako ndio inapatikana (Taqwa)lakini lazima ujue au ufate (Process)zake ndio ufanikiwe, Sasa tuingie kwenye Darsa, Mnyama au Wewe nyote mkizaliwa mnapata sifa au sehemu ya kuona na kusikia, ndio maana utaona Mtoto anapita katika (Process)ya kuuliza hichi nini, yule nani, Kwa hiyo katika njia ya Shahidi anapatikana na Shuhuda.
Ntafafanua ili mpate kunifahamu, Wewe hapo ulipo ukitizama kitu unagawika mafungu mawili, mtazamaji na chenye kutizamwa, lakini huwezi kufahamu lazima kiingie cha tatu hapo, Nayo ndio hiyo Akili, kwa hiyo utaona Akili ni neema kubwa ya kuweza kutujulisha sisi hicho chenye kutizamwa ni kitu gani, ndio maana kama huna Akili utasikia lakini hujui umesikia nini, na utaona pia hujui umeona nini, Ndio maana Akili ikaitwa Neema Kubwa kutoka kwa Mollah wetu, Lakini sasa matatizo yetu tunabaki kwenye Akili, na hapo ndipo sote tuna haribikiwa, kwa sababu Akili ni yenye kukusanya Mambo na kutufundisha tu ndio kazi yake, ndio wengi tunasalia hapo, ikisha tunzunguka baina ya (Past and Future), Lakini ukizinduka utaelewa kiko kitu cha nne, tena nakwambia kwa uhakika hichi cha nne siwezi kukizungumzia sijui nini, lakini naweza kusema nimekutana nacho na miujiza yake haielezeki, ila ntakufahamisha ikiwa utanifahamu basi na wewe utafanya kazi ya kukitafuta hakiji kwa jitihada zako ila kwa Rehma za Mwenye enzi Mungu akitaka kukuonesha, na hicho ni kitu cha Nne ndio hiyo Shuhuda, ukipata hicho hutobaki kuwa Binaadamu wa kawaida maisha yako yatabadilika.
Sasa kumbuka ile aya ilotaja Mollah wako alipowaambia Malaika anataka kuumba Mwanaadamu, ikisha akamfundisha majina, rudi pale kabla ya kufundishwa, hiyo ndio (Being) yako, hapo ndipo inapoishi Taqwa, Kuna anaye tizama, kinachotizamwa ikisha inaingia Akili kutafisiri, sasa jiulize huyu wa Nne Mwenye kuyajua hayo yote nani?. ukiweza kufahamu utakua ushaingia kwenye Taqwa, na hapo ndio (Bliss)hutoki tena, na hayo ndio makaazi yako, hapo ndio nyumbani, lakini tumetoka haturudi mpaka siku ile ya kufa, ukirudi sasa hivi utakua furahani, utatoka msibani, madhila yatakupungua, dhanmbi hutendi tena, hamu zitakatika, katika hali hiyo haijui maradhi, kama vile isivojua kuzeeka, jichunguze kuna nyakati unajiona (Body) imezeeka lakini wewe bado hiyo ndio Shuhuda ipate hiyo upate Taqwa.