Sunday, September 30, 2018

MAZOEZI YA KUFA PART 1

Asalaam Aleiykum

Mungu kampa Zawadi Mbili Mwanaadamu kwa ajili ya Mapenzi alonayo kwa viumbe vyake, Zawadi ya kwanza ni Maisha ya Umauti, Kwa ajili hiyo ndio utaona mtoto akizaliwa kitu cha mwanzo anatafuta kuvuta pumzi, Na kama hajavuta pumzi utaona madaktari wanavo hangaika kuhakikisha mtoto anahema, Napenda ufahamu Pumzi ni daraja la kuishi.
Halafu zawadi ya pili ni uhai, Na jambo hili la uhai linamalizika kwa kitendo cha mwisho cha Binaadamu kutoa pumzi. Kutokana na mifano hiyo miwili yanapatikana katika umri wetu wote mazoezi ya kufa, Kuna alama mbili ambazo ikiwa utazingatia utaziona (Mtoto kitendo cha kwanza kuvuta pumzi, na Mtu mzima anapokufa kitendo cha mwisho anachofanya ni kutoa pumzi)za mwisho.
Kutokana na mifano hiyo inapatikana Alama ya kuzaliwa kwako na kufa kwako. Tuko katika Ulimwengu huu kila mmoja wetu ni Marehemu mtarajiwa, kama utajua ukweli huo basi utakua huna haja ya kukimbia ukweli huo ulotuzunguka kila pembe ya maisha yetu.
Naam ikiwa ukweli ni huo mimi na wewe tumejiandaa vipi na tukio hili la Umauti, Sasa kama bado unapuuza tukio hili au unakimbia kadhia hii ya mazoezi ya kufa basi nakuletea Alama ya pili nayo ni Usingizi. Aliposema Mwenye Enzi Mungu anachukua Roho za  Waja wake wakati wamelala, Unashangaa na kupata wasiwasi inakuaje, hali kama hiyo?, ukaleta ubishi mbona nikilala naendelea kuhema Roho inachukuliwa vipi?. Tuko katika darsa ya (Mazoezi ya Kufa) Na mimi nakupeleka katika uvutaji wa Pumzi, jaribu kuzifata pumzi zako mwanzo mpaka mwisho zinapoishia, hapo kuna kitu utagundua iwe siri yako Mwenyewe, iko (Gap) ambayo pumzi zishakwisha lakini wewe hujafa ukiweza kuigundua ukaipata (Gap) hiyo hapo utakutana na kile kisichokufa.
Naam tunaendelea na darsa yetu, tuko katika alama ya pili kama wewe unaendelea kuleta ubishi unafahamishwa mbona hata machine inafanya kazi hiyo ya kuuweka mwili wako usioze, ukaendelea kuhema, mpaka madaktari wakasema sasa tuzime machine. Kwa hiyo Roho yako haitegemei kuhema, kuhema ni kazi ya Mwili na Akili yako.
Endelea Part 2

MAZOEZI YA KUFA PART 2

Asalaam Aleiykum

Umo katika darsa ya Mazingatio ya kufa, na hicho ni kitendo pekee ambacho hakika kitatokea, kama ulivozaliwa na lazima upitie katika kadhia hii ya Umauti, sikusudii kukutisha hilo nawaachia Masheikh, mimi nakuandaa na Ukweli ulokuzunguka ili usikwepe majukumu yako, kwa sababu siku zote tunazani kifo kinatokea kwa wenzetu na sisi siku yetu iko mbali, hivyo sivyo siku zetu zishakaribia ila tunasubiri wakati.
Basi kama umo katika safari hii fupi ya maisha wacha sasa nikuchukue katika Alama ya tatu nayo ni kuzeeka kwako, Alama hiyo ni ile ya kupungua uwezo wa vitu ndani ya Mwili wako, na dalili zake ndio hayo Maradhi, au kwa lugha nyengine tunaita uzee. Kwa Matukio hayo utajiona kumbe unaishi baina ya Mauti na Uhai. Ukivuta pumzi uhai na ukitoa pumzi ni Mauti.
Sasa jiulize kwanini dini zote zinasisitiza uhudhurie Maziko au ukadhuru Makaburi, hapo kuna hekima gani, ushapata kujiuliza, jee unajua nini kinatokea, na kwanini ikawa lazima mazikoni au makaburini?. Nini siri ya Jambo hili, Umo katika mazoezi ya kufa pata habari kamili uwe katika walojiandaa, siku hii hata ikitokea ghfla ujue safari ishawadia, Kwanini Mauti, Nini Kitakukumbusha kwenye huyo Maiti?. Itabidi turudi kwenye Mahudhurio ya Mazishi, Watu wengi wanakwenda Mazikoni lakini wanakosa madhumuni halisi ya kitendo chenyewe cha kuzika. Utaona Masheikh wanakimbilia kuonesha kuwa wao wanajua kuzika, na wale walohudhuria wanakua wameshughulika kubadilishana number za simu, na hadith za mitaani, hapo tena utaona wanafanya haraka haraka na kumfukia maiti ikisha hao wanakwenda zao.
Sio lazima muoneshe misimamo au Iman zenu kwenye Miili ya watu wa watu, utaona wanawaambia watu kaeni kimya na kila mtu amuombee Maiti kimya kimya. Unajua maana ya kimya?(Be silent) hiyo ni (Meditation) unatakiwa ufanye mazoezi ndio uweze kukaa kimya, au unaweza kuwa kimya nje, ndani unatukana mwanzo mpaka mwisho, iangalie Akili yako kutwa inasema, kamata kalamu uandike, chukua dakika 10 tu halafu uone umeweza kukaa kimya?, ukiweza kukaa kimya basi nenda sasa ukaombe dua ya Ikhlas, na hivi ndivo tunavo wafanyia Maiti zetu tuna tupa na kwenda zetu, Alipoambiwa Mtume s.a.w akae kimya ni kwa ajili ya wale wanafiki wa dini, ndio ikateremka aya usiwaombee kwenye makaburi yao, lakini vyengine alikua akiomba tena kwa sauti, na masahaba wakubwa wakubwa walikua wakenda na kusoma Quraan juu ya Makaburi.
Sasa ukiwaambia watu kaeni kimya maana yake (Be Silent)maana yake kuwa kimya nje na ndani ndio utaweza kutoa dua ya Ikhlas vyenginevyo Matusi matupu, kwa sababu watu wamo kwenye mazungumzo ya kidunia, ghafla unawaambia kaeni kimya muombeeni dua Maiti ya (Sincere) jambo hilo haliwezekani kabisa.
Wacha niwaeleze kisa hapa ili na nyinyi mpate faida muhimu. Dua ya Ikhlas inatokea Moyoni kule kwenye kutokea machozi kwa mfano, Na wewe Moyoni umehama siku nyingi hata kulia huwezi tena,kutokana na mambo kadhaa uliyoyafanya unayajua mwenyewe, Nikupeni kisa cha Mwanangu siku moja nilimwambia  Acha kutizama TV ili usali, kwa bahati Msala ulikua karibu na alikua kashatia Udhu, moja kwa moja akafunga Sala, Alivomaliza kusali nikamwambia mbona hujatia Nia ya Sala?, akanijibu tumefundishwa Nia haina nafasi katika Ulimi, wewe una nyanyuka na ufunge Sala.Nikataka kumfundisha kwa Lugha ya kijitu kizima lakini nikaona hatonifahamu.
Nilimuuliza wakati ulipokua unasali ulikua unafikiri nini?, Akanijibu nikwambie ukweli Baba nilikua naangalia ile film ndani ya Sala mwanzo mpaka mwisho, Na hayo ndio mafundisho yenu mnayopewa, Sasa pata faida ya Nia uijue kwa undani, kwa sababu watu watachukua kihadithi kimoja ndio watafanya dini nzima ime (Base) Na hadith hiyo, nasema hadith inaweza kuwa kweli au ya uongo au ya udhaifu, sasa mimi nakupa kitu cha ukweli unachoweza kukithibitisha Mwenyewe bila ya Hadith.Kwanini ikaletwa Nia, Nifahamishe vizuri hapa ifahamike, Ukiwa wewe ni Mcha Mungu huna haja ya Nia, Kwa sababu Wewe unaishi kwenye moyo, Na kuishi kwenye moyo ndio Taqwa. Ama kwa sisi tunoishi kwenye Akili, ndio wenye hekima kwa huruma zao wakatupa zawadi ya Nia kwa ajili ya kukata mazungumzo, au nyimbo, au matusi, ndio ikawa unasema nanuia kusali Sala fulani kwa sauti ya kujisikia mwenyewe rakaa fulani na mimi ni Maamuma au Imam, hiyo ni nyenzo ya kukufanya uweze kuingia na kushuka kwenye moyo ili  uwe (Hadhir)(Alert) upate chembe ya unyenyekevu. Sasa vipi na wewe utaifahamu siri hii . Endelea part 3




MAZOEZI YA KUFA PART 3

Asalaam Aleiykum

Naam Nikamwambia Mwanangu nataka kukufundisha kitu, kwani unafahamu Mwanaadamu anasikia kwa kutumia nini? akanijibu masikio, Nikamwambia Tia Vidole vya kati masikioni uyazibe kabisa kwa nguvu, nikaanza kuongea, akanambia mwanzo ilikua (Silent)halafu (Very strange things happen)nikaanza kusikia kupitia kifuani, Nikamwambia hapo ndio inaptakiwa kutokea Nia, Dua na Sala yako, Na wewe Fanya (Experiment)utalijua hilo, Kama isivojulikana sauti inatokea wapi, Na huko kusikojulikana kunatakiwa kutoke Dua ya ikhlas, Kwa kuwa tumehama siku nyingi hatuna tena mapenzi kwenye nyoyo zetu, Na hususan wale wenye kuukimbilia Usheikh wajitahidi sana kuwa na mapenzi, yako mafundisho ntakupeni kama mtataka kurudi kwenye moyo, kama mtataka ku (Fall in love)Mfanye nini, Wacha nikufundishe njia hii labda unaweza kupata mapenzi, unaweza kuwa Mtu wa Taqwa, ufanye nini?.Mazoezi hayo mwanzo yatakushitua lakini hayana neno baada ya miezi utajiona vipi umebadilika, Raha kubwa itashuka juu ya nafsi yako, mazoezi haya yako ya aina mbili moja ni kurudi kwa hiyari nayo ni (Surrender) na ya pili (By force) ni Ku (Imagine)kila ukikumbuka jione huna(Imagine) (Kichwa).
Hapo utajiona vipi mawazo yanavotoweka, utaanza kuona ajabu baada ya kufikiri kwa Akili sasa unatumia moyo, kidogo kidogo utakua unashuka Moyoni, utaanza kupenda kila kitu, Wanyama, miti wanaadamu, Na hapo ndio utaanza kuupandisha mti wa Taqwa moyoni mwako, hapo ndio unaweza kuomba dua kwa ikhlas.
Naam tulikua tunachuma matunda ya fahamu sasa turejee kwenye darsa yetu ya Mazoezi ya kufa, kwanini makaburini, kwanini Maiti, ulipoambiwa uhudhurie viwili hivyo dhumuni ni kukufanya uzinduke na kukutana na kile chenye kuishi milele. Lakini mnakwenda Kuzika umebeba na duka lako, umebeba urafiki au hadith za mipira au za kisiasa. Kutokana na hali hiyo mambo muhimu yanakupita huyaoni kabisa. vipi unatakiwa ufanye ukenda kuzika, sio utupe maiti ikisha huyo ukimbie, Unatakiwa Fikra na mawazo yako yote yazingatie huyo maiti toka mwanzo mpaka mwisho anazikwa, upate nafasi uone vipi anatolewa, vipi anazikwa, vipi anafukiwa, nini kinatokea, ikiwa unakwenda mazikoni kikweli kweli basi itakua rahisi kwako wewe baada ya miezi kadhaa kugundua Almasi, kitu adhimu kabisa utakijua, kama mwanzo nilivokwambia kuna kitu baina ya kuvuta pumzi na kutoa na hapa makaburini, kiko kitu pia kama utakifatilia na kuzinduka, utaona (Energy) Maalum, utaona kinachozikwa ni kiwiliwili tu, Na wewe Kiburi kitakutoka kwa mara ya Mwanzo utakautana na kusutana na nafsi yako kwamba wewe ni (Nothingness)ukipata zawadi ya kuamka mazikoni(Your life)haitokua ile ile tena utagundua kitu muhimu sana, hutokubali tena kuondoka makaburini bila ya kuomba dua, utafunguliwa pazia na utapata kujua kwanini tunamsalia maiti, na huyu anosaliwa anafaidika vipi, hilo litakuandaa vizuri na mazoezi haya ya kufa, nakupa changa moto mengine kayatafute Mwenyewe Inshaallah Mwenye enzi Mungu atakufungulia kuyaona ili khofu ya kufa ikutoke kwa ajili ya matendo mema, kwa ajili ya kumpenda Mollah wako, nimekujulisha mawili matatu natumai yatakusaidia kwenye mazoezi yako. Nakuomba niombee kama ninavokuombea.
Mollah tupe takhfif wakati wa kutoka Roho zetu, tuletee Manukato mazuri ya Janat firdous yawe maliwazo yetu kwa ajili ya kukutana na Wewe,  utukutanishe na wenzetu walo wema, tudumishe kwenye Ibada utupe Mwisho Mwema, tuongoze katika njia ilonyooka kama ulivo waongoza walopita, wala usitutie Sheitani tukawa na viburi na kufanya mambo tusoyajua mpaka umetubainishia ukweli ulotoka kwako.
Amin