Asalaam Aleiykum
Umo katika darsa ya Mazingatio ya kufa, na hicho ni kitendo pekee ambacho hakika kitatokea, kama ulivozaliwa na lazima upitie katika kadhia hii ya Umauti, sikusudii kukutisha hilo nawaachia Masheikh, mimi nakuandaa na Ukweli ulokuzunguka ili usikwepe majukumu yako, kwa sababu siku zote tunazani kifo kinatokea kwa wenzetu na sisi siku yetu iko mbali, hivyo sivyo siku zetu zishakaribia ila tunasubiri wakati.
Basi kama umo katika safari hii fupi ya maisha wacha sasa nikuchukue katika Alama ya tatu nayo ni kuzeeka kwako, Alama hiyo ni ile ya kupungua uwezo wa vitu ndani ya Mwili wako, na dalili zake ndio hayo Maradhi, au kwa lugha nyengine tunaita uzee. Kwa Matukio hayo utajiona kumbe unaishi baina ya Mauti na Uhai. Ukivuta pumzi uhai na ukitoa pumzi ni Mauti.
Sasa jiulize kwanini dini zote zinasisitiza uhudhurie Maziko au ukadhuru Makaburi, hapo kuna hekima gani, ushapata kujiuliza, jee unajua nini kinatokea, na kwanini ikawa lazima mazikoni au makaburini?. Nini siri ya Jambo hili, Umo katika mazoezi ya kufa pata habari kamili uwe katika walojiandaa, siku hii hata ikitokea ghfla ujue safari ishawadia, Kwanini Mauti, Nini Kitakukumbusha kwenye huyo Maiti?. Itabidi turudi kwenye Mahudhurio ya Mazishi, Watu wengi wanakwenda Mazikoni lakini wanakosa madhumuni halisi ya kitendo chenyewe cha kuzika. Utaona Masheikh wanakimbilia kuonesha kuwa wao wanajua kuzika, na wale walohudhuria wanakua wameshughulika kubadilishana number za simu, na hadith za mitaani, hapo tena utaona wanafanya haraka haraka na kumfukia maiti ikisha hao wanakwenda zao.
Sio lazima muoneshe misimamo au Iman zenu kwenye Miili ya watu wa watu, utaona wanawaambia watu kaeni kimya na kila mtu amuombee Maiti kimya kimya. Unajua maana ya kimya?(Be silent) hiyo ni (Meditation) unatakiwa ufanye mazoezi ndio uweze kukaa kimya, au unaweza kuwa kimya nje, ndani unatukana mwanzo mpaka mwisho, iangalie Akili yako kutwa inasema, kamata kalamu uandike, chukua dakika 10 tu halafu uone umeweza kukaa kimya?, ukiweza kukaa kimya basi nenda sasa ukaombe dua ya Ikhlas, na hivi ndivo tunavo wafanyia Maiti zetu tuna tupa na kwenda zetu, Alipoambiwa Mtume s.a.w akae kimya ni kwa ajili ya wale wanafiki wa dini, ndio ikateremka aya usiwaombee kwenye makaburi yao, lakini vyengine alikua akiomba tena kwa sauti, na masahaba wakubwa wakubwa walikua wakenda na kusoma Quraan juu ya Makaburi.
Sasa ukiwaambia watu kaeni kimya maana yake (Be Silent)maana yake kuwa kimya nje na ndani ndio utaweza kutoa dua ya Ikhlas vyenginevyo Matusi matupu, kwa sababu watu wamo kwenye mazungumzo ya kidunia, ghafla unawaambia kaeni kimya muombeeni dua Maiti ya (Sincere) jambo hilo haliwezekani kabisa.
Wacha niwaeleze kisa hapa ili na nyinyi mpate faida muhimu. Dua ya Ikhlas inatokea Moyoni kule kwenye kutokea machozi kwa mfano, Na wewe Moyoni umehama siku nyingi hata kulia huwezi tena,kutokana na mambo kadhaa uliyoyafanya unayajua mwenyewe, Nikupeni kisa cha Mwanangu siku moja nilimwambia Acha kutizama TV ili usali, kwa bahati Msala ulikua karibu na alikua kashatia Udhu, moja kwa moja akafunga Sala, Alivomaliza kusali nikamwambia mbona hujatia Nia ya Sala?, akanijibu tumefundishwa Nia haina nafasi katika Ulimi, wewe una nyanyuka na ufunge Sala.Nikataka kumfundisha kwa Lugha ya kijitu kizima lakini nikaona hatonifahamu.
Nilimuuliza wakati ulipokua unasali ulikua unafikiri nini?, Akanijibu nikwambie ukweli Baba nilikua naangalia ile film ndani ya Sala mwanzo mpaka mwisho, Na hayo ndio mafundisho yenu mnayopewa, Sasa pata faida ya Nia uijue kwa undani, kwa sababu watu watachukua kihadithi kimoja ndio watafanya dini nzima ime (Base) Na hadith hiyo, nasema hadith inaweza kuwa kweli au ya uongo au ya udhaifu, sasa mimi nakupa kitu cha ukweli unachoweza kukithibitisha Mwenyewe bila ya Hadith.Kwanini ikaletwa Nia, Nifahamishe vizuri hapa ifahamike, Ukiwa wewe ni Mcha Mungu huna haja ya Nia, Kwa sababu Wewe unaishi kwenye moyo, Na kuishi kwenye moyo ndio Taqwa. Ama kwa sisi tunoishi kwenye Akili, ndio wenye hekima kwa huruma zao wakatupa zawadi ya Nia kwa ajili ya kukata mazungumzo, au nyimbo, au matusi, ndio ikawa unasema nanuia kusali Sala fulani kwa sauti ya kujisikia mwenyewe rakaa fulani na mimi ni Maamuma au Imam, hiyo ni nyenzo ya kukufanya uweze kuingia na kushuka kwenye moyo ili uwe (Hadhir)(Alert) upate chembe ya unyenyekevu. Sasa vipi na wewe utaifahamu siri hii . Endelea part 3
No comments:
Post a Comment