Asalaam Aleiykum
Mungu kampa Zawadi Mbili Mwanaadamu kwa ajili ya Mapenzi alonayo kwa viumbe vyake, Zawadi ya kwanza ni Maisha ya Umauti, Kwa ajili hiyo ndio utaona mtoto akizaliwa kitu cha mwanzo anatafuta kuvuta pumzi, Na kama hajavuta pumzi utaona madaktari wanavo hangaika kuhakikisha mtoto anahema, Napenda ufahamu Pumzi ni daraja la kuishi.
Halafu zawadi ya pili ni uhai, Na jambo hili la uhai linamalizika kwa kitendo cha mwisho cha Binaadamu kutoa pumzi. Kutokana na mifano hiyo miwili yanapatikana katika umri wetu wote mazoezi ya kufa, Kuna alama mbili ambazo ikiwa utazingatia utaziona (Mtoto kitendo cha kwanza kuvuta pumzi, na Mtu mzima anapokufa kitendo cha mwisho anachofanya ni kutoa pumzi)za mwisho.
Kutokana na mifano hiyo inapatikana Alama ya kuzaliwa kwako na kufa kwako. Tuko katika Ulimwengu huu kila mmoja wetu ni Marehemu mtarajiwa, kama utajua ukweli huo basi utakua huna haja ya kukimbia ukweli huo ulotuzunguka kila pembe ya maisha yetu.
Naam ikiwa ukweli ni huo mimi na wewe tumejiandaa vipi na tukio hili la Umauti, Sasa kama bado unapuuza tukio hili au unakimbia kadhia hii ya mazoezi ya kufa basi nakuletea Alama ya pili nayo ni Usingizi. Aliposema Mwenye Enzi Mungu anachukua Roho za Waja wake wakati wamelala, Unashangaa na kupata wasiwasi inakuaje, hali kama hiyo?, ukaleta ubishi mbona nikilala naendelea kuhema Roho inachukuliwa vipi?. Tuko katika darsa ya (Mazoezi ya Kufa) Na mimi nakupeleka katika uvutaji wa Pumzi, jaribu kuzifata pumzi zako mwanzo mpaka mwisho zinapoishia, hapo kuna kitu utagundua iwe siri yako Mwenyewe, iko (Gap) ambayo pumzi zishakwisha lakini wewe hujafa ukiweza kuigundua ukaipata (Gap) hiyo hapo utakutana na kile kisichokufa.
Naam tunaendelea na darsa yetu, tuko katika alama ya pili kama wewe unaendelea kuleta ubishi unafahamishwa mbona hata machine inafanya kazi hiyo ya kuuweka mwili wako usioze, ukaendelea kuhema, mpaka madaktari wakasema sasa tuzime machine. Kwa hiyo Roho yako haitegemei kuhema, kuhema ni kazi ya Mwili na Akili yako.
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment