Tuesday, October 30, 2018

ALAMA SITA ZA MWENYE ENZI MUNGU PART 3

Asalaam Aleiykum

وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦ يُرِيڪُمُ ٱلۡبَرۡقَ خَوۡفً۬ا وَطَمَعً۬ا وَيُنَزِّلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً۬ فَيُحۡىِۦ بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآ‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَعۡقِلُونَ 
Na katika Ishara zake (Za kuonesha nguvu zake) Ni kukuonesheni umeme kwa (Kukutieni)Khofu na Tamaa (Ya kuja mvua),Na kuyateremsha maji kutoka mawinguni, kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake, Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanofahamu.
Ni ishara ya Umeme inayomshitua Mwanaadamu ndio maana hata ukifa kwa umeme au umenasa kidogo kwenye Umeme  wanasema (Electric Shock), limetumika neno la kufufuliwa ili upate kujua mfano huo wa kufufuliwa ardhi na wewe umekuhusu, kama unafahamu sawa sawa au umeishughulisha akili utafahamu kuwa Ardhi inaishi kama unavoishi wewe, kwanini isiwe hivyo wakati wewe Mwenyewe Ardhi tupu, na ndio ukichunguza kwa undani utaona tafauti baina yako na (Body)Mwili wako, mnafanya kazi mbili tafauti, (Body) yako inafanya kazi zake (Automatic) na wewe Mwenyewe ni (Manual)lakini bado hujazipata fahamu hizo.
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَن تَقُومَ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ بِأَمۡرِهِۦ‌ۚ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمۡ دَعۡوَةً۬ مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ إِذَآ أَنتُمۡ تَخۡرُجُونَ
Na katika Ishara zake(Za kuonesha uwezo wake)Ni kuwa Mbingu na Ardhi zimesimama Kwa Amri yake, kisha atakapokuiteni wito mmoja tu (Nyote) mtatoka Ardhini.Ikiwa unafikiri, au una ujuzi, pengine unasikia au unafahamu basi katika Ulimwengu huu kuna sheria Mbili za Maumbile nazo ni (Levitation na Gravitation) ndio zilofanya Mbingu na Ardhi kusimama katika hesabu zake, Na itakapopulizwa hilo Baragumu (Sonic sound). Kumbuka hivi sasa Meumbwa kutokana na hiyo Ardhi na litakapopigwa parapanda hiyo hiyo Ardhi ndio itakukusanya tena kukupa (Body)mpya ili usimame Mbele ya Mollah wako. Huo ndio uwezo wa Mwenye enzi Mungu na ndizo Alama anazotupa ili tuzingatie tupate kumkumbuka yeye Muumba wetu.

No comments:

Post a Comment