Asalaam Aleiykum
Siku katika masiku ya mahudhurio yangu kwenye maziko nilifatwa na Mtu baada ya kuzika na kwa Mfadhaiko mkubwa akaniuliza hivyo Mzee wangu ndio kalala pale kaburini?, Hivi ndio utakua mwisho wetu wote sisi?, hivi tutakaa Kaburini kwa Muda gani?, Na nini habari ya lile dongo unalofunikwa nalo?. Nijulishe Mzee wangu ana hali gani sasa hivi. Nikamwambia uwepo wako ni ishara ya Mwenye enzi Mungu lakini kwa kuwa Akili yako imeshughulika na mambo mengine huzioni Ishara hizo, kwa wale wenye kufahamu Ishara za Mwenye enzi Mungu wanaelewa siku ya kuzaliwa(au Kutunga mimba)unaletwa na Malaika, Na siku ya kufa kwako pia unachukuliwa na Malaika.
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ۬ ثُمَّ إِذَآ أَنتُم بَشَرٌ۬ تَنتَشِرُونَ
Na Katika Ishara zake (Za kuonyesha uwepo wake)Ni huku kukuumbeni kwa udongo, kisha mekua watu mnaonea (Kutapakaa kila sehemu).
Mwanaadamu (Nature)yako ni udongo kwa hiyo usishughulike sana wakati unakwenda kwenye (Re-Cycle Process) Umeumbwa kwa udongo na unarudi kwenye hali ile ile ya udongo, wewe ni udongo kama lilivo jabali, ukuta, mti lakini najua khofu yako iko pahala pamoja, vipi itakua utakapofukiwa kwenye Ardhi, ndio maana Mtume s.a.w akahimiza nendeni makaburini, hudhurieni maziko, ukipata ufunuo wakuwa udongo unafukiwa wewe unabaki, Utapata nafuu fulani, utapata unyenyekevu kwenye Moyo wako wakutafuta Nani huyu Mwenye kubaki, Na Nani huyo Mwenye kujua kama anabaki, Na akibaki anakwenda wapi, Ukipata kuigundua hiyo (Separation) ndio utajua nini dini,Nani Mwenye Enzi Mungu, sio kusoma haisaidii lazima upate (Feeling) hizo wewe Mwenyewe, ujiulize nani huyu Mwenye wasiwasi wa kuzikwa, halafu ujiulize nini itakua habari yangu mimi, jibu langu kwa yule mtu likawa hivi, Ama kuhusu (Body)yako kweli inaoza chini ya Ardhi, lakini kuna kitu chengine Adhimu, kuna hiyo (Spirit)au Roho ndio wanopanda nayo Malaika na kuipeleka inapotakiwa(Huko Barzaq), kwa hiyo Binaadamu vitu viwili (Udongo)ni guo au jumba la kukaa hiyo Roho , na cha Pili ni hiyo Roho ndio yenye dhamana yote ya Maisha yako.
Naam na Ishara ya Pili ni hii:
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ
Na Katika Ishara zake (Za kuonyesha Ihsani zake juu yenu) Ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye ameyajaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri.
Watu gani wenye kufikiri ni wale walogundua kuwa huyu Mwenzangu ni nusu ya mimi, Nabii Adam alikua na Bibi Hawa Mbinguni wakafukuzwa ikisha wakapoteana, Na wewe na huyo ulonaye pia mlipoteana, Na sasa mekutana mpo pamoja na hizo ni ishara kubwa kama utazingatia, jiulize kwanini unaacha watu wote mpaka unamuoa fulani, imekuaje habari hiyo, mekutana vipi?, kwanini ikawa huyo ulonaye, Na katika Ishara zake mwanzo yanazuka mapenzi yakimalizika inabakia Rehma au ita huruma, unajua nini huruma?, Mapenzi ni Furaha, huruma ni kujitolea bila ya Masharti kama wafanyavo waume kwa wake zao na wake kwa waume zao.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment