Tuesday, October 30, 2018

ALAMA SITA ZA MWENYE ENZI MUNGU PART 2

Asalaam Aleiykum

وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦ خَلۡقُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَـٰفُ أَلۡسِنَتِڪُمۡ وَأَلۡوَٲنِكُمۡ‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّلۡعَـٰلِمِينَ
Na katika ishara zake(Za kuonesha uweza wake)Ni kuumba Mbingu na Ardhi, Na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu, Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi.
Sasa hivi tunapata Maalumati kutoka kwa wanasayansi vipi Mbingu ilivyo na Ardhi ilivyo. Ama kwa wenye ujuzi ni wale walotambua kuwa Mwenye enzi Mungu hana Lugha, lugha kakuumbieni nyinyi ili mpate kuwasiliana na hayo yamo kwenye (Utility)ya Akili, Na hilo la Rangi limo kwenye (Geographical Location). Wepi wenye ujuzi ni wale wenye kufanya utafiti(Wanasayansi).

وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦ مَنَامُكُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّہَارِ وَٱبۡتِغَآؤُكُم مِّن فَضۡلِهِۦۤ‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَسۡمَعُونَ
Na Katika Ishara zake(Za kuonesha hekima yake)Ni kulala kwenu usiku na (Kuamka)Mchana, Na kutafuta kwenu Fadhila yake, Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia. Hakuna Mwanaadamu anoweza kuepuka kulala, ukiweza kukaa macho baada ya miezi miwili utaanza kusema peke yako na ukifika mwezi wa tatu unakufa, Na yale maajabu yakutafuta riziki kwa wengine kupewa zaidi na wengine kupewa kidogo. Wepi wenye kusikia ni wale Waloamini dalili za Mwenye Enzi Mungu.

No comments:

Post a Comment