Saturday, December 15, 2018

DALILI ZA KURUDI PEPONI PART 3

Asalaam Aleiykum

Dalili za unapokwenda, unapewa hapa hapa Ulimwenguni, Kwa kawaida Wanaadamu tumepewa uwezo fulani wa kuona na kusikia kwa kiasi maalum, na kitu chengine ambacho kiko katika hizo (Six sense) Ni Harufu lakini hii inatupotea kwa haraka katika Ulimwengu huu tunaoishi sisi, Lakini siku ya kutolewa Roho kitu cha Mwanzo kurejeshewa ni hiyo harufu ndio itakayokujulisha kwamba sasa unarejea Peponi au unakwenda Motoni, huna haja ya kusubiri, aya inasemaje katika sura ya Waqqiah (88-89)
"فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ "
"Basi akiwa (Mtu huyo anayekufa) Ni Miongoni mwa Wale walokaribishwa (Na Mwenye enzi Mungu). Wepi walokaribishwa, Walokaribishwa ni wale walokua karibu wakigonga Mlango wa Akhera, Kukoje kuwa Karibu na Ufalme wa Mwenye enzi Mungu, Ni kule kutenda Mema, Kufanya Ibada, kutoa sadaka, kuwa na tabia njema, kuishi na binaadamu wenzio kwa vizuri, hapo ndio unafunguliwa Mlango na kukaribishwa katika Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu, utajua siku gani kama umekaribishwa, siku ile ya kuja kutolewa Roho yako, nini kitatokea?".

"فَرَوۡحٌ۬ وَرَيۡحَانٌ۬ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ۬" 
Basi ni Raha(Kubwa)Na Manukato(Mazuri) Na Mabustani yenye Neema.
Naam Hiyo ndio habari, Siku ya Kutolewa Roho ni siku ya (Furaha au Raha kubwa)usiyopata kuiona, Siku zote unajiona unafurahi, unacheza ngoma,muziki na hivi na vile, zote hizo sio furaha(Sababu zinatokea kwenye Akili), kwani furaha na raha ya kweli inatokea kwenye Roho, na wewe na mimi tuko kwenye misukosuko mikubwa hatuwezi kupata Raha, tunaonja chembe ya Raha, nayo ni katika tendo la Ndoa(sex) ndio maana unakwenda tena na tena ili upate hali hiyo, unagusa kitu chenye kuitwa (Bliss)kwa sekunde tu, ikisha unarudi katika hali yako ya tafran, lakini wakati wa kutolewa Roho kama ulikuwa mtu Mwema basi unapewa hali kama hiyo mara (Billion)furaha tupu, unakufa unaona raha, unakufa huku unacheka, Na dalili mnaziona wakati mnajitaarisha katika tendo la ndoa kwa wenye kujua siri na wasiojua yanafanyika mataarisho ya harufu nzuri, unajua kwanini ?, kwa sababu wakati ule mnakwenda kuyagusa maji ya uhai, na kama utakua (Alert) utapata (experience) vipi unakua (Sensitive) katika jambo la harufu, kwa sababu wakati ule Roho inashiriki, ndio maana huna (Control) na Roho ni yenye kupenda harufu nzuri, harufu nzuri inafatana na (Bliss).
Ndio utaona yanawekwa Manukato mazuri mazuri,nyudi zinachomwa, na hivyo ndio vyakula vya Roho, Kwa hiyo na siku ya kutolewa Roho yako, Elewa Mwenye Enzi Mungu sio kaupamba Ulimwengu huu kwa Mataa pekee bali na Manukato mazuri mazuri, Na wewe ukitolewa Roho unaanza kusikia Harufu nzuri za Manukato(Na Ukiwa maiti pia unatiwa harufu nzuri kwenye Mwili wako kwa ajili ya kuzikwa), Tahadhari sana ukimalizikia uhai wako unasikia harufu mbaya, ogopa dalili hizo jua huna marejeo mazuri, ndio utaona macho yanatutoka, khofu imetujaa kwa kuwa tunajua wapi tunamalizikia, Na jambo la tatu unaondoshewa pazia, huna haja ya kusubiri, ukiondoshwa upeo wa kuona ndio hapo unaanza kuona yaliyopo huko,(Ndio  yule sahaba alivofunguliwa maono ya peponi wakati wa kutoka roho yake akasema,"Bora ingekua mbali, kwa ajili ya ule wema alomfanyia mtu wa kumbeba, na kile kipande cha mkate akasema bora ungekua mzima, na ile nguo akasema bora ingekua mpya)hayo ndio mambo alooneshwa akawa anapiga kelele, pengine alikua akipewa mfano kwa sisi wenye uhai sasa hivi tuyafanye, kama angetoa mkate mzima baada ya kupewa nyumba ya chini peponi, angepewa kasri ya dhahabu peponi.
Naam kwa hiyo dalili zinaanza hapa hapa wakati wa kutoka Roho yako. Na kama ulikuwa Mtu mwema wa kheri za kawaida aya ya 90-91 inofatia inasema unapata "usalama". Mollah wetu tujaalie katika hao, wala usitunyime ladha za kuionja pepo yako na mazuri yalioko huko.
Amin

1 comment: