Saturday, December 15, 2018

DALILI ZA KURUDI PEPONI PART 2

Asalaam Aleiykum

Kwa kuwa kila Mmoja wetu kashaonja Pepo kupitia Kwa Baba yetu Nabii Adam a.s ndio maana tunapenda Raha na Kuchukia Karaha, Raha ndio (Nature) yetu, Karaha au madhila au mateso ni jambo lenye kutokezea tu, lakini husikii hata siku moja mtu kazoea shida, shida haizoeleki, lakini Raha inazoeleka na ndio kawaida ya Mwanaadamu, kutokana wakati fulani Nafsi hii ilikuwepo Peponi, kutokana na Ubishi wetu au ita utundu au ushawishi ndio tukajikuta tuko kwenye Ulimwengu huu ili tuonje Mambo ya kilimwengu yawe Mtihani wetu wa kututizama tunaendelea na jeuri yetu au tutamtii Mollah wetu na kurejea kwenye makaazi yetu ya salama yaliyopo Peponi, Na ikiwa bado tunaendelea na ile jeuri yetu basi tutajikuta hata huko upande wa pili (Akhera) Bado makaazi yetu ni Motoni.
Na  Moto ni mgumu zaidi kuliko mifano ya mateso tuyapatayo hapa Ulimwenguni, Mwanaadamu hachukui dhiki, jitizame hapa Ulimwenguni ikikufika dhiki au mateso unakuaje, Tizama Maradhi yakikufika unakua ghali gani, au madhila yakiwasili unakuaje, sasa hayo ni majaribio tu ya Ulimwengu huu nini habari yako wewe na mimi kuhusu Adhabu yake Mwenye Enzi Mungu ambayo ni kubwa zaidi kuliko shida hizi za Ulimwengu.
Lakini Mwenye Enzi Mungu si Mwenye kutaka kuwaadhibu viumbe vyake ndio maana kaweka milango ya Toba wazi mpaka mwisho wa Uhai wako ili apate kukusamehe, lakini kama hutaki hiyo ni shauri yako, Na matatizo yote yanakuja pale ukenda mbali na Njia ya Mwenye Enzi Mungu, ndio Maana tukapewa Sala tano ili ziweze kutukumbusha, ndio maana katika hiyo Sala tumepewa sura tunaisoma kila mara maneno haya."Wewe tu ndio tunakuabudu, Na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada". Kila tukikosea tunaomba toba na kutaka muongozo kutoka kwako, tukishikwa na maradhi, tukiwa kwenye hatari au khofu wewe pekee ndie tunakutegemea.
Na tunapokwenda kinyume na maagizo yako tukateleza basi husema, "Tuongoze njia ilonyooka""Njia ya wale Uliowaneemesha, siyo (Ya wale Walokasirikiwa, wala (Ya) wale waliopotea.
Wepi walokasirikiwa ni wale wamo kwenye dini lakini matendo yao ni maovu, Na walopotea ni wale ambao hawana habari na njia ya Mwenye enzi Mungu kabisaa.
Sasa unapokua hufati Amri za Mwenye enzi Mungu ndio unakua humo katika hiyo njia ilonyooka, Lakini ukiwa katika njia ilonyooka ukiambiwa usile tunda huli, ndio itakapofika siku ya kutolewa Roho?.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment