Saturday, December 15, 2018

DALILI ZA KURUDI PEPONI PART 1

Asalaam Aleiykum

Zanzibar kuna msemo zamani ukitumika unasema "kavunja ukuta wa watu kwa harufu ya chakula kitamu". Maneno mazito yameficha maana kubwa yenye mazingatio kwa wenye uwezo wa kufikiri.
neno la mwanzo kabisa limetumika kuvunja ukuta,, inatuonesha lazima mvunjaji alikua na bidii, kafanya jitihada kubwa mpaka kuweza kuuvunja Ukuta, Ukuta wenyewe siwake, na sababu gani ilomfanya avunje?, Ni harufu tu ya chakula kitamu, swali kakijuaje kama chakula kitamu, hapo inaashiria kuwa lazima kawahi kukila chakula hicho ndio maana alivosikia tu harufu yake akaamua kuuvunja ukuta wa watu.
Ikiwa Ukuta Umevunjwa kwa ajili ya harufu ya chakula kitamu tu, hapo inaonesha mvunjaji lazima kashawahi kukionja chakula ndio maana akachukua juhudi za kuuvunja Ukuta huo, Basi katika hali kama hiyo na sisi Binaadamu tunatakiwa tufanye juhudi za kuuvunja Ukuta wa Shetani ili tupate kurudi peponi. Nikisema kuingia peponi ntakua nimekosea katika lugha ya kitaalamu iloambatana na ufahamu, lugha sahihi ya kutumika ni kurejea Peponi, kwa sababu Jinsi yetu kila Mmoja kashaonja Pepo, kilichotufanya tusahau ni kazi ya Shetani ambayo anaendelea kutusahaulisha kwamba hapo mwanzo alitutoa Peponi, Sasa nini kinachotufanya tuikumbuke Pepo?.
Endelea Part 2

DALILI ZA KURUDI PEPONI PART 2

Asalaam Aleiykum

Kwa kuwa kila Mmoja wetu kashaonja Pepo kupitia Kwa Baba yetu Nabii Adam a.s ndio maana tunapenda Raha na Kuchukia Karaha, Raha ndio (Nature) yetu, Karaha au madhila au mateso ni jambo lenye kutokezea tu, lakini husikii hata siku moja mtu kazoea shida, shida haizoeleki, lakini Raha inazoeleka na ndio kawaida ya Mwanaadamu, kutokana wakati fulani Nafsi hii ilikuwepo Peponi, kutokana na Ubishi wetu au ita utundu au ushawishi ndio tukajikuta tuko kwenye Ulimwengu huu ili tuonje Mambo ya kilimwengu yawe Mtihani wetu wa kututizama tunaendelea na jeuri yetu au tutamtii Mollah wetu na kurejea kwenye makaazi yetu ya salama yaliyopo Peponi, Na ikiwa bado tunaendelea na ile jeuri yetu basi tutajikuta hata huko upande wa pili (Akhera) Bado makaazi yetu ni Motoni.
Na  Moto ni mgumu zaidi kuliko mifano ya mateso tuyapatayo hapa Ulimwenguni, Mwanaadamu hachukui dhiki, jitizame hapa Ulimwenguni ikikufika dhiki au mateso unakuaje, Tizama Maradhi yakikufika unakua ghali gani, au madhila yakiwasili unakuaje, sasa hayo ni majaribio tu ya Ulimwengu huu nini habari yako wewe na mimi kuhusu Adhabu yake Mwenye Enzi Mungu ambayo ni kubwa zaidi kuliko shida hizi za Ulimwengu.
Lakini Mwenye Enzi Mungu si Mwenye kutaka kuwaadhibu viumbe vyake ndio maana kaweka milango ya Toba wazi mpaka mwisho wa Uhai wako ili apate kukusamehe, lakini kama hutaki hiyo ni shauri yako, Na matatizo yote yanakuja pale ukenda mbali na Njia ya Mwenye Enzi Mungu, ndio Maana tukapewa Sala tano ili ziweze kutukumbusha, ndio maana katika hiyo Sala tumepewa sura tunaisoma kila mara maneno haya."Wewe tu ndio tunakuabudu, Na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada". Kila tukikosea tunaomba toba na kutaka muongozo kutoka kwako, tukishikwa na maradhi, tukiwa kwenye hatari au khofu wewe pekee ndie tunakutegemea.
Na tunapokwenda kinyume na maagizo yako tukateleza basi husema, "Tuongoze njia ilonyooka""Njia ya wale Uliowaneemesha, siyo (Ya wale Walokasirikiwa, wala (Ya) wale waliopotea.
Wepi walokasirikiwa ni wale wamo kwenye dini lakini matendo yao ni maovu, Na walopotea ni wale ambao hawana habari na njia ya Mwenye enzi Mungu kabisaa.
Sasa unapokua hufati Amri za Mwenye enzi Mungu ndio unakua humo katika hiyo njia ilonyooka, Lakini ukiwa katika njia ilonyooka ukiambiwa usile tunda huli, ndio itakapofika siku ya kutolewa Roho?.
Endelea part 3

DALILI ZA KURUDI PEPONI PART 3

Asalaam Aleiykum

Dalili za unapokwenda, unapewa hapa hapa Ulimwenguni, Kwa kawaida Wanaadamu tumepewa uwezo fulani wa kuona na kusikia kwa kiasi maalum, na kitu chengine ambacho kiko katika hizo (Six sense) Ni Harufu lakini hii inatupotea kwa haraka katika Ulimwengu huu tunaoishi sisi, Lakini siku ya kutolewa Roho kitu cha Mwanzo kurejeshewa ni hiyo harufu ndio itakayokujulisha kwamba sasa unarejea Peponi au unakwenda Motoni, huna haja ya kusubiri, aya inasemaje katika sura ya Waqqiah (88-89)
"فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ "
"Basi akiwa (Mtu huyo anayekufa) Ni Miongoni mwa Wale walokaribishwa (Na Mwenye enzi Mungu). Wepi walokaribishwa, Walokaribishwa ni wale walokua karibu wakigonga Mlango wa Akhera, Kukoje kuwa Karibu na Ufalme wa Mwenye enzi Mungu, Ni kule kutenda Mema, Kufanya Ibada, kutoa sadaka, kuwa na tabia njema, kuishi na binaadamu wenzio kwa vizuri, hapo ndio unafunguliwa Mlango na kukaribishwa katika Ufalme wa Mwenye Enzi Mungu, utajua siku gani kama umekaribishwa, siku ile ya kuja kutolewa Roho yako, nini kitatokea?".

"فَرَوۡحٌ۬ وَرَيۡحَانٌ۬ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ۬" 
Basi ni Raha(Kubwa)Na Manukato(Mazuri) Na Mabustani yenye Neema.
Naam Hiyo ndio habari, Siku ya Kutolewa Roho ni siku ya (Furaha au Raha kubwa)usiyopata kuiona, Siku zote unajiona unafurahi, unacheza ngoma,muziki na hivi na vile, zote hizo sio furaha(Sababu zinatokea kwenye Akili), kwani furaha na raha ya kweli inatokea kwenye Roho, na wewe na mimi tuko kwenye misukosuko mikubwa hatuwezi kupata Raha, tunaonja chembe ya Raha, nayo ni katika tendo la Ndoa(sex) ndio maana unakwenda tena na tena ili upate hali hiyo, unagusa kitu chenye kuitwa (Bliss)kwa sekunde tu, ikisha unarudi katika hali yako ya tafran, lakini wakati wa kutolewa Roho kama ulikuwa mtu Mwema basi unapewa hali kama hiyo mara (Billion)furaha tupu, unakufa unaona raha, unakufa huku unacheka, Na dalili mnaziona wakati mnajitaarisha katika tendo la ndoa kwa wenye kujua siri na wasiojua yanafanyika mataarisho ya harufu nzuri, unajua kwanini ?, kwa sababu wakati ule mnakwenda kuyagusa maji ya uhai, na kama utakua (Alert) utapata (experience) vipi unakua (Sensitive) katika jambo la harufu, kwa sababu wakati ule Roho inashiriki, ndio maana huna (Control) na Roho ni yenye kupenda harufu nzuri, harufu nzuri inafatana na (Bliss).
Ndio utaona yanawekwa Manukato mazuri mazuri,nyudi zinachomwa, na hivyo ndio vyakula vya Roho, Kwa hiyo na siku ya kutolewa Roho yako, Elewa Mwenye Enzi Mungu sio kaupamba Ulimwengu huu kwa Mataa pekee bali na Manukato mazuri mazuri, Na wewe ukitolewa Roho unaanza kusikia Harufu nzuri za Manukato(Na Ukiwa maiti pia unatiwa harufu nzuri kwenye Mwili wako kwa ajili ya kuzikwa), Tahadhari sana ukimalizikia uhai wako unasikia harufu mbaya, ogopa dalili hizo jua huna marejeo mazuri, ndio utaona macho yanatutoka, khofu imetujaa kwa kuwa tunajua wapi tunamalizikia, Na jambo la tatu unaondoshewa pazia, huna haja ya kusubiri, ukiondoshwa upeo wa kuona ndio hapo unaanza kuona yaliyopo huko,(Ndio  yule sahaba alivofunguliwa maono ya peponi wakati wa kutoka roho yake akasema,"Bora ingekua mbali, kwa ajili ya ule wema alomfanyia mtu wa kumbeba, na kile kipande cha mkate akasema bora ungekua mzima, na ile nguo akasema bora ingekua mpya)hayo ndio mambo alooneshwa akawa anapiga kelele, pengine alikua akipewa mfano kwa sisi wenye uhai sasa hivi tuyafanye, kama angetoa mkate mzima baada ya kupewa nyumba ya chini peponi, angepewa kasri ya dhahabu peponi.
Naam kwa hiyo dalili zinaanza hapa hapa wakati wa kutoka Roho yako. Na kama ulikuwa Mtu mwema wa kheri za kawaida aya ya 90-91 inofatia inasema unapata "usalama". Mollah wetu tujaalie katika hao, wala usitunyime ladha za kuionja pepo yako na mazuri yalioko huko.
Amin