Asalaam Aleiykum,
Vipi sasa huko kufa ukiwa hai, mfano wake kama vile mbegu unavoitia ndani ya ardhi ikisha unakaa kwa muda mpaka mmea unaanza kuchipua(kutokeza)lakini mwanzo lazima mbegu ife ndio uchomoze huo mti uchipue, na wewe umeshatupa mbegu ya Taqwa katika ardhi ya Ramadhani unayo nafasi sasa uipalilie mbegu yako au usubiri Ramadhani ya 29 uikate kate, uamuzi ni wako wewe, kwa lugha ya ufupi nilivosema ufe nime maanisha ubadilike kabisa katika mwenendo wa Tabia zako ufanye u-turn, upotee kabisa chukua ahadi Ramadhani inakwisha lakini kwangu itaendelea mwaka mzima, nitadumu na mwezi huu katika nyanja zote za maisha yangu, kila siku kwangu mimi itakua Ramadhan, Uchukue ahadi yakua utawakimbia Marafiki zako wenye tabia mbaya na mbovu kabla wao hawajakukimbia wewe ikiwa umekufa au umepata maradhi, Na wale Marafiki zangu wema nitabakia nao kama kawaida lakini ndani mie nitakua kiumbe mwengine kabisa.
Uache mambo ya ulevi, ujizuie na mambo ya uzinifu, uwache kula mali ya haramu na rushwa, ujiepushe na mambo ya kipuuzi puuzi, fikra mbovu,tamaa ya utajiri,uridhike na alicho kukadiria Mollah wako,usipite ukawa unasengenya wenzako,uondoshe husda katika nafsi yako, na kiburi kikuondoke kabisa, ukikuta maskini unakaa nao na kula nao, ndio maana nikasema ufe kwani hivo vichache tu nilivovitaja vyote ni vifo ambavyo mwanaadamu itabidi upite unakufa kidogo kidogo unakufa taratibu ni lazima tabia zote hizi ziyayuke isibaki hata moja zikimalizika wewe utakua mtu wa aina nyengine hapo utakapo kuwepo hapo ndipo pana dhamana ya pepo na hapo tena utaiona (Nyota ya Jaha)kama unavo uona mbaa mwezi ingaravo.
Nini Laylatul Qadir?Jee ipo?Jee inaonekana?.
Jawabu wewe upo tayari kuiona,
إِنَّآ أَنزَلۡنَـٰهُ فِى لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ
"Hakika tumeiteremsha ndani ya usiku(Maalum)ulio mtukufu wa kadir"
Hebu tutizame nini kiza(usiku)ni(absence of light)au kutokuwepo kwa taa au (muangaza)ndio maana utaona mchana nyota hazionekani lakini zipo pale pale, lakini kilichoondoka ni kiza(usiku)kwa maana hiyo katika ufalme wa Mwenye-enzi-Mungu hakuna usiku wala mchana ila katika Ulimwengu wetu huu ndio kuna huo usiku na mchana, akauteua Mollah wako katika usiku huu wa (Qadir)kuiteremsha hii (Quraa'n)kwanini ikawa katika usiku huu kwa sababu hii Qura'an yenyewe ni (Nuru)na usiku huu ndani yake inatokea kuwa na utukufu wa hiyo (Nuru)ya Mwenye-enzi-Mungu yanachanganyika Mawili haya kupatikana huo ukweli wa Taa ya muongozo.
وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ
"Nini kitachokujulisha hiyo Laylatul Qadir"
Ndio mwanzo wa darsa hii nikasema itabidi kwanza yakukute mauti (ungali-hai)ili uijue hiyo maana yenyewe na uione kama unavotaraji, na vipi waloiona wakawa wanahadithia inagara sana na wewe miaka yote umesubiri hata siku moja hujaiona, mambo haya yakoje, napenda uelewe hayasemwi maneno yanohusiana na Mwenye-enzi-Mungu yakawa ndani yake hayana ukweli, wapo walouona usiku huu ndio wakahadithia, na wewe unayo nafasi hiyo lakini uko tayari kujitoa muhanga, kama nilivosema (Nuru)hii inataka mataarisho ambayo machache nimeyataja huko mwanzoni, sasa ikiwa jua huliwezi kulitizama vipi utaweza kuitizama hiyo (nuru)iliyomo katika hii Laylatul-Qadir, walipo ona (watawa wa Kikiristo)iliwafanya upofu, ikawa kiza wao wakaita(The dark night of the soul)Walipoona wacha Mungu wa Kiislamu wao wakaita(The light night of the soul)au nyota ya jaha, Nakujulisha yakuwa kila mtu anapita au anakuwemo katika usiku huu, lakini yategemea umekukuta katika hali gani?.
No comments:
Post a Comment