Tuesday, July 5, 2016

WAFALME WA PEPONI PART 1

Asalaam Aleiykum

Zipate darsa zenye kufungua maono yako ili usije kushangaa katika mambo usoyajua yakakuletea balaa za ubishi, Soma kwa uangalifu ili upate maelekezo yatoridhisha nafsi yako kuhusiana na huo upande wa pili unaokwenda kuishi. Pia napenda uelewe hayawafiki mafunzo haya Matajiri wala Wanasiasa kwa kuwa hawana haja nayo, Na pia ukiwa na uchu wa kutafuta mali inakua vigumu mafunzo kama haya kukufikia. 
Kwanini ikawa hivyo?(Quran-145-Al-Imran)

وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَنْ تَمُوتَ إِلاَّ بِإِذْنِ الله كِتَابًا مُّؤَجَّلاً وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ 
"Na Nafsi yoyote haitoweza kufa ila kwa amri ya Mwenye enzi Mungu(na) kwa ajali iliyowekewa, Na Anayetaka malipo ya duniani tutampa hapa (hapa), Na anayetaka malipo ya Akhera tutampa huko (huko), Na kwa yakini tutawalipa wanaoshukuru".
Kwanini aya imeanza na kutajwa mauti? kwa sababu humkuti tajiri au mtu yoyote mwenye harakati nyingi za maisha akataka kujua habari hizi, akajiuliza kwanini kaumbwa, lini atakufa? upande wa pili ukoje, nini wajibu wake, ajabu gani za maisha, kwanini anaishi, na akimaliza maisha haya itakuaje, hataki kabisa maswali haya yamzonge katika shughuli zake za utafutaji wa mali.
Mtu kama huyu utakua naye Msikitini, kipindi cha Sala hakimpiti lakini hana akifanyacho ila mazoea ya mazoezi ya viungo, Sala haipatikani kabisa. Kutokana na hali hiyo Mtu huyo awe wewe au mimi anajiweka mbali na pepo.
Sasa wepi watakayoipata hiyo pepo, zama katika hii darsa angalau uchungulie mfano wa pepo au maana yake ikoje. Naam nani wanoingia? aya hapo juu imeanza vizuri sana imetaja "hakuna Nafsi itokufa ila kwa Idhini ya Mwenye enzi Mungu" Hapo ni kuoneshwa yupo Mfalme Mwenye kukumiliki na hufi hata ujitupe ghorofa mia ila atake yeye, na si hivyo tu bali umeshapangiwa kifo hicho na kimo ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa.
Watakao ingia katika hiyo Pepo ni Maskini, Nisije kusema Maskini ukaanza kushangiria na kujiona namie nimo sababu sina nyumba, sina pesa, sipati chakula kwa kawaida, Maskini Mwenyewe sio wewe, kwa sababu wewe na Tajiri hamna tafauti, nyote mkenda kusali maombi yenu yaleyale, Mmoja anaomba apewe utajiri, na Mwengine anaomba azidishiwe utajiri, mali yake isipungue, Mwanawe apasi Mtihani, anaomba asitumbuliwe jipu, apandishwe cheo, Mkewe au Mumewe asichepuke, jirani anyimwe bahati, wewe itizame sala yako utadhani unakwenda kwa (Mganga wa Kienyeji) Kumbe umehudhuria kwa Yule alokupa uhai.
Sasa basi Masikini wepi walokusudiwa hapo, itabidi hapa tuvuke bahari twende ngambo ya pili tukaazime maneno yalotamkwa na Nabii Isa a.s au (Yesu)ndani ya (Injili) pale aliposema:
(Bless are the poor in spirit:for theirs is the kingdom of heaven-Matthew:5:3).
Wamebarikiwa wale masikini wa Kiroho:Kwao wao upo(Urithi) Ufalme wa Mwenye enzi Mungu.
Nini maana ya maneno haya? na upi huo Ufalme wa Mwenye enzi Mungu?, Na kwanini Ufalme huo utakua wao?, Basi kwanza kabla ya kugusa mambo hayo itatubidi tuujue Ufalme wenyewe ulokusudiwa ni upi?, Umo katika darsa ya Wafalme wa Pepo nakutaka uilekeze Akili yako katika kitabu Kitukufu  chenye ukweli ndani yake ili kikujulishe vipi utakua Ufalme huo.
Endelea part 2 





No comments:

Post a Comment