SASA SIKU ZOTE WEWE UNASHEREKEA SIKU YAKO YA KUZALIWA UKIWA HAI HII (DEATH DAY) HAPA ULIMWENGUNI WANASHEHEREKEA NDUGU ZAKO, MARAFIKI ZAKO NA WENGINEO JAPO SHEREHE ZENYEWE ZINA TAFAUTI, TAMADUNI ZENGINE WANAPIGA NGOMA, WENGINE WANAPEANA KAHAWA NA HALUA ZOTE NI SHEREHE NENDA KWENYE HIYO MISIBA UTAJUA KUTOKANA NA MAZUNGUMZO YAO YALOJAA UTANI, MAZUNGUMZO YA MPIRA NA KIDUNIA, WANOPATA MSIBA AMBAO NAO HAWAWEZI KUSHEHEREKEA NI WACHACHE MNO AMBAO KWA SASA LABDA KWA SABABU WATAKOSA HUDUMA ZAKO IWE PESA MALI NYENGINE WAO WAKO KWENYE FIKRA WATAWEZAJE KUMUDU GHARAMA ZA MAISHA, KWANINI IKAWA HIVYO?.
IMEKUA HIVYO KUTOKANA NA WEWE KUWEKEWA SIKU ZAKO TATU ZA HUZUNI, BAADA YA HAPO UNASAHAULIKA KABISA, HIYO IMETOKANA NA SABABU YA UELEWA ILIYOPO MOYONI KUWA WEWE NI MGENI NA SASA USHAKWENDA ZAKO, HAINA HAJA YA KUOMBOLEZA SANA, NANI AKAE AKILILIA (BODY)YAKO WAKATI ANAJUA HATA HIYO (BODY)SIO YAKO NUSU KUTOKA KWA MAMA NA NUSU KUTOKA KWA BABA NA KILA MWAKA( 98%)INABADILIKA SASA WAMLILIE NANI NA WEWE HAUPO, UNACHOPEWA WEWE NI VAZI LA (TAQWA)NA LINABADILISHWA KILA SIKU, KILA MWEZI, NA KILA MWAKA, KWA HIYO JUMBA HILO WANALOZIKA SIO LA ZAMANI SIO LA UTOTONI WALA UJANANI, LINAPOCHOKA JUMBA HILO LIKAWA HALIBADILISHWI TENA(REPAIR) NDIO LINAKUFA, KUMBUKA KABLA YA KUFA KWAKE KUANZIA MIAKA YA 60 LINAPOSIMAMA KUFANYA UKARABATI NDIPO LINAANZA KUKARIBISHA MARADHI ILI UANZE SAFARI YAKO YA KUONDOKA KWENYE ULIMWENGU HUU. KUMBUKA KINACHO KUFA NA KUZIKWA NI KIWILIWILI CHAKO, SWALI LA KUJIULIZA SASA WEWE NANI NA UMETOKEA WAPI NA UNARUDI WAPI?. SWALI NI ZITO SANA KUPATA JAWABU LAKE INABIDI UJITUPE KWENYE BAADHI YA MAFUNDISHO NA UCHUNGUZI MPAKA UJIJUE WEWE NANI, UFIKE KWENYE (POINT)YA KUJUA HILO JINA SI LAKO NI (TAG)KAMA YA (BAG) WAKATI UNA SAFIRI, SASA UKIONDOA JINA UNABAKI KUWA NANI?. NJIA YA KUANZIA NI LAZIMA UJIJUE JAPO KWA KAULI KUWA WEWE NI KITU KIMOJA ADHIMU NACHO NI HIYO (ROHO)AMBAYO KUTOKANA NA HIYO ROHO WEWE UMEKUJA HAPA ULIMWENGUNI NA KUTOKANA NA HIYO ROHO UNARUDI ULIPOTOKEA KWA MOLLAH WAKO.
SASA UTAJUAJE KAMA WEWE ROHO HII NDIO DHUMUNI YA DARSA HII KUKUPA ISHARA , KUMBUKA SIKUFUNDISHI , KWA SABABU HAKUNA MWENYE KUFUNDISHWA KUONA , HAKUNA MWENYE KUFUNDISHWA KUSIKIA NA WALA HAKUNA MWENYE KUFUNDISHWA KUTEMBEA, VYOTE HIVYO NI HAKI YAKO UMEFUNDUA MWENYEWE KUTOKA KWA MOLLAH WAKO NA HILI LA ROHO PIA NI HAKI YAKO UKIONDOSHA UVIVU JAPO GUMU ILA LINAWEZEKANA UKAFA UNAJIONA, UKAFA SHAHIDI, NA UKIPATA HILI LA ROHO USHAKUA KHALIFA WA ARDHI, USHAPATA UFALME WENYE HAZINA KUBWA KATIKA ULIMWENGU HUU. ILI KUKUASHIRIA UENDE WAPI ITABIDI UNIWIE RADHI NIKUPE KISA KIMOJA KILO NITOKEA MIE BINAFSI NA KAMA UKIELEWA KISA HICHI BASI KUNA MAFUNDISHO MAKUBWA NDANI YAKE, UTAPATA ISHARA NA MWISHO NTAKUPA DAWA UWAPE MA WENGINE WENYE MATATIZO YA USONGO WA AKILI AU WALE AMBAO WANASHIDA YA KULALA HAWAPATI USINGIZI, HATA KAMA HUJAIJUA HIYO ROHO YAKO HUTAMANI WEWE KULALA KAMA MTOTO MDOGO UKAWA UNARUDI KWENYE (SOURCE) YA UHAI WAKO KILA USIKU?.
No comments:
Post a Comment