Asalaam Aleiykum
Kuna kitu kila Mwanaadamu anakitafuta kwa kuwa kimempotea, Kitu hichi uwe Kiongozi au Jambazi, Uwe Mkarim au Uwe Katili Mwenye kuwatesa wenzio, Uwe Tajiri Mwenye kumiminika Mapesa kitu hichi sote kimetukaa moyoni na ndio lengo letu muhimu kufanikiwa kukipata.
Watu wengi wanakitafuta kitu hiki kwa njia nyingi tafauti, Na ndio maana utaona unatafuta Utajiri ukiupata mwisho wake unaona hauna faida yoyote na Bado kuna kitu (Missing), Ukitafuta Mke aliye mzuri au Mume aliye (Handsome) ukishampata unaona bado kuna kitu (Missing), Ukipata cheo ukawa Rais au Mbunge au Waziri ukishafanikiwa unaona bado kuna kitu (Missing) sasa sababu za kukitafuta kitu hichi ni tafauti lakini lengo lililojificha ndani ya nafsi ya kila mmoja wetu ni lile lile moja la kukipata hicho kitu, na hiyo ndio (Nature) yetu hata kama utaleta sababu nyenginee.
Fanya ufanyavyo lakini hamu yako na matarijio ni kitu hicho na hakuna chengine, ndio Maana upesi ukiwa Mzee au ukiwa Mgonjwa unakua na Huzuni unaona sasa Mauti yashakaribia na wewe huna hakika kama utakipata kitu hicho au litatokea tukio lengine usilotarajia, ndio maana watu wote wakati wa kufa wanakua wenye kukata tamaa kwa sababu hawajakipata kitu hichi, sababu kwenye Ulimwengu huu ulikua umeshughulika na mambo mengine chungu nzima.
Sasa kwanini ikawa sote tunataraji kitu hichi wakati hatukijui, Jawabu linafatia kitu hichi tunakijua lakini tumekisahau, hatukijui nini kitu hichi katika Ulimwengu huu wa Ardhini, Lakini ndani ya Nafsi zetu tunakikumbuka kitu hichi kipo ndio maana tunafanya jitihada ya kukipata tena. Kumbuka tumeumbwa kwa Nafsi moja iliyotokana na Baba yetu Adam a.s ambayo makaazi yake yalianzia Peponi, (Al-Baqarah 35)
وَقُلۡنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
"Na tulisema (kumwambia) Ewe Adam kaa wewe na Mkeo katika Bustani hii (peponi), Na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu, msije kuwa miongoni mwa waliodhulumu"(nafsi zao kwa kuziacha Amri za Mwenye enzi Mungu).
Huko ndiko nafsi ilipoonja hicho kitu kinachoitwa (Bliss) au (Joy) ya Peponi na hilo pekee ndilo Walimwengu wote tunalotaraji tulipate lakini njia yake ni ngumu, na hakuna jambo la rahisi usijidanganye, masharti yake yana vishindo, sio kwa kusema tu ukadhani utaipata tunza hii, inatakiwa ufanye bidii kubwa na mapenzi ya kudumu utakapoigundua Njia hiyo ya Mcha Mungu.
Endelea Part 2
Sunday, December 14, 2014
NJIA YA MCHA MUNGU PART 2
Asalaam Aleiykum
Kwa hali tulo nayo sasa hivi sote tumo katika kiza, kila Mtu anapapasa vipi ataiona njia hii, Tunapigana vikumbo Misikitini lakini ni wachache wenye kuigundua njia hii, toa sadaka, jenga visima, jenga misikiti yote hayo ni bure unafanya (Business) ya kuipata njia hii kwa (Cheap)Elewa kitu hichi hakinunuliwi na pesa abadan, kinanunuliwa kwa nafsi yako na wala sivengine, kama huna Ucha Mungu wewe Muflis, na haipatikani ila mpaka uigundue njia hii ikisha Udumu nayo, Na wengi wanaigundua njia hii lakini kila mara inawapotea.
Kwanini Unapotea ? Kutaka kujua kwanini unapotea ndio Darsa yetu inatuchukua katika safari muhimu ili upate kujua (Drugs) au vile vishawishi vinavyo tupoteza na kama unaweza kuviacha basi basi hayo ni mafanikio yako, hata siku ya kufa kwako utakua ni mwenye furaha badala ya huzuni. Jambo hili ni vigumu sana na pia ni Rahisi sana, kati yake kunakaa maamuzi yako ya kuutaka Ucha Mungu.
Jee Unataka kubakia kwenye njia hiyo, Wewe unataka zawadi Maalumu ya Mollah wako ya (Bliss) idumu na wewe milele, basi ikiwa unalitaka hilo kwanza itabidi tujitizame sisi Binaadamu Umbile letu likoje?, Halafu tuanze na kazi ya Mataarisho ya kwenda kwenye njia ya Ucha Mungu.
Mwanaadamu umetokana na Ardhi, Na kila kitu chako ulichoumbiwa kinaitegemea hiyo hiyo Ardhi ili upate kuishi kwenye Ulimwengu huu, Na ukiangalia (System) yako yote Mwanaadamu ina mwenendo wa kula kama tutavyoona katika uchambuzi wetu, Unaona vipi ukila ukashiba hali yako inavokua namna gani, Unapumzika unataka kulala, na mambo mengine ya matamanio ya Kilimwengu, hicho ndio chakula cha kukuweka hai, halafu kuna chakula chengine chenye kukufanya kuishi.
Napenda Uwelewe kuwa Hai na Kuishi ni mambo mawili tafauti, (Mfano)Mgonjwa yuko kwenye (Coma) yuko Hai lakini Haishi, kwa hiyo kuishi kunategemea matendo, Na hayo matendo ndio hicho chakula cha Pili, Tahadhari sana katika hicho chakula cha pili unakula nini?(Banii Israel 36)
"وَلَا تَقۡفُ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۚ إِنَّ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡبَصَرَ وَٱلۡفُؤَادَ كُلُّ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ كَانَ عَنۡهُ مَسۡـُٔولاً۬ "
Wala usifate usiyo na Elimu nayo, Hakika Masikio na Macho na Moyo hivyo vyote vitaulizwa.
Sasa Jitizame unaifata wewe njia ya Ucha Mungu kwa matendo?, Au unafata yale usokua na Elimu nayo(Unapinga Amri za Mwenye Enzi Mungu) yepi hayo unayoyafata wewe?, Sasa unapata dawa kama hii usiitupe japo chungu imeze itakuponesha ni (Gurantee)n hakuna alomeza kidonge hiki akawa asipone.
Tafauti yako Wewe na Mcha Mungu ni ndogo sana, ni kama hivi yeye anajua, wewe hujui, Yeye anayo (Torch) Wewe huna unapita kujipiga na makuta huoni kitu, Yeye ana Elimu yenye manufaa wewe unafata Elimu isiyo na manufaa, Na ukifata Elimu isiyokua na manufaa inakupoteza ima iwe kwenye Dini au Dunia unakua (Split Mind) kama kwenye Dini unaamua kupiga marufuku vitu vyote unasema (Haram) na kama umezama kwenye Dunia vitu vyote unaona Halali unakua huna elimu ya kuvitenganisha, sababu elimu zote unofata ni za kusikia, labda umesikia fulani kasema hivi, au umehadithiwa, Sasa katika Njia hii ya Mwenye Enzi Mungu unatakiwa umfate kwa Makini Mcha Mungu yeye yuko mbele wewe uko nyuma ili upate kuweka Alama pale utakapobakia peke yako ujue wapi pakupita na wapi pakuepuka.
Endelea part 3

NJIA YA MCHA MUNGU PART 3
Asalaam Aleiykum
Katika Njia hii Mcha Mungu katika kutufahamisha hatumii neno (haramu) ila anatumia neno(Haifai) halafu wewe mwenyewe ndio utaamua unautaka Ucha Mungu au huutaki, Kwa kuwa huo Ucha Mungu unakuja kwa njia ya Mapenzi, Na mapenzi hayalazimishwi ila inatakiwa hiyari.
Naam hichi chakula cha Pili ndio hicho kilotajwa katika hiyo aya kuwa Masikio, Macho, na Moyo vyote vitaulizwa, sasa jitizame unakula nini kupitia vitu hivyo?, hakuna mengine ila unakula wewe kwa kusikiliza Maasi yote kutwa nzima, Uongo na Matusi, nyimbo vyote vinakwenda kufanya makaazi kwenye Moyo wako, mpaka unakua vitu hivyo (Automatic) katika mazuungumzo yako, jitizame ukiulizwa japo saa, mtu anakuuliza saa ngapi basi ikiwa tano na dakika tatu, utamwambia na dakika saba, ukimgomba mtoto lazima tusi japo jepesi litakutoka, basi elewa mambo hayo yanaishi moyoni, Yanafanyiwa (Process) moyoni, hiyo ndio huduma ya kwanza kwa kile chakula unachokula, nini kinafanyika ? Matusi na Music kazi yake kubwa ikipita katika Moyo ni kwenda kusimamisha Mshipa wa Matamanio, Ndio maana (Music) au Nyimbo ikipigwa unatingishika sababu ishajenga jukwaa moyoni.
Kuna kitu ndani ya Nafsi yako kina nyanyuka kama Nyoka (Cobra) anavyonyanyuka akipigiwa firimbi, Lakini hili la (Music) wewe hulioni, tafauti yako na (Cobra) inakua hasikii lakini anaona, wewe huoni ila unasikia, Na (Energy) hii ikishanyanyuliwa si Rahisi kupanda juu tena inateremka bondeni ndio maana mawazo mabaya mabaya yanakujia, upo kwenye Sala umerukuu unasoma sura ya (Fatiha), hivyo ndio athari za kusikiliza (Music), Ndio maana utaona kwenye (Dance) watu wanakatika viuno kuashiria kuwa sasa Furaha ya matamanio ishashuka kiunoni, Nyimbo iko kichwani na matamanio yashateremka kiuononi sasa lete mdundo tukimaliza tukakate matamanio.
Na hapo kama wapo wenye kushuhudia, Macho yanakula mpaka kuvimbiwa, Balaa tupu, hii anacheza vile, duuh sauti ile inakuaje lazima nimfatilie, Balaa kubwa wakati ule, muda ukiwa huyaoni yale basi unaamua ukaangalie TV ili uendelee kula kila aina ya maasi, Macho yanakula kila Maasi, Watu wanatembea Utupu, na ghasia zote za (Advertisement) na ikisha ukenda kulala huna usingizi ila moyo unakaa kwenye shift, unaanza kuchambua kwa njia ya ndoto kipi nitapike, kiporo gani nikale kesho, ikisha huyo ukiamka asubuhi unaanza tena, na kama hutizami unakula japo kwa kugusa lakini mwenyewe hujitambui unapeana mikono na wanawake na hivi na vile huku unaendelea kula kwa njia ya matamanio.
Kwa njia hiyo ndivyo tunavyo shiba chakula cha Dhanmbi, Na kwa hilo tutakwenda kuulizwa kwanini hamjafata njia ya Ucha Mungu.
Ipi Njia Hiyo?
Njia yenyewe ni Rahisi sana na pia ni vigumu sana lakini ukiamua unaweza kufanikiwa, ufanye nini ? anza kidogo kidogo kupunguza kusikiliza maasi, nyimbo, matusi, uongo, punguza kutizama mambo ya maasi na kusoma mambo mambo ya habari za kipuuzi, kidogo kidogo ukifanikiwa kuyapunguza mambo hayo utaona Muangaza unaanza kutokea kwenye Moyo, (Torch) ya Ucha Mungu inaanza kukuonesha njia, ni kama chumba chenye kiza ukaleta (Kibatari) au (Taa) na huo muangaza ni kuacha hayo matendo niliyoyataja hapo juu, na siku utakapo pata Muangaza ukawa (Full) katika chumba chako cha moyo, hapo utakua tayari huna wasiwasi unaweza kutizama TV lakini Moyoni kuna (adhkari ya Mollah wako)unaweza kukaa na watu wanatukana lakini matusi yao hayaingii moyoni mwako, unaweza kusikiliza nyimbo lakini hazifiki moyoni mwako zinapita kama sauti nyengine tu, sasa hivi si unasikia ndege, treni, gari lakini yote hayo hayaingii moyoni mwako na siku utakayopata (Taa) ya Ucha Mungu utakua na hali kama hiyo, hapo tena utabadilika utakua hukai katika mambo hayo, hutizami mambo hayo, husikilizi mambo hayo, lakini huyaogopi kwa sababu hayakai moyoni mwako, hayana nafasi tena ya kukutawala, ila wewe umeyatawala, na huo ndio Ukhalifa, huo ndio Ucha Mungu. Tunamuomba Mollah atujaalie kutufiksha katika njia hiyo.

Sunday, December 7, 2014
ELIMU ZA AJABU PART 4
Asalaam Aleiykum
Tunaendelea kutafuta kuifahamu japo kwa uchache elimu hii ya kuruka, na hakuna chengine kitotupa taarifa ya jambo hili ila tumuulize Mfalme wa (Mysticism) Nabii Suleiman a.s yeye alipewa nini? Quraan Sura ya (Saba aya ya 12)
وَلِسُلَيۡمَـٰنَ ٱلرِّيحَ غُدُوُّهَا شَہۡرٌ۬ وَرَوَاحُهَا شَہۡرٌ۬ۖ وَأَسَلۡنَا لَهُ ۥ عَيۡنَ ٱلۡقِطۡرِۖ وَمِنَ ٱلۡجِنِّ مَن يَعۡمَلُ بَيۡنَ يَدَيۡهِ بِإِذۡنِ رَبِّهِۖۦ وَمَن يَزِغۡ مِنۡہُمۡ عَنۡ أَمۡرِنَا نُذِقۡهُ مِنۡ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ
"Na Kwa Suleiman(Tulimpa amri ya elimu ya)Upepo(Uliokwenda)Safari yake ya asubuhi(Kasi yake ni mwendo)wa mwezi mmoja, Na Safari yake ya jioni(Kasi yake ni mwendo wa)mwezi mmoja, Na tukamyayushia chem chem ya Shaba, Na katika Majini(Kulikuwapo)waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mwenye Enzi Mungu wake, Na kila anyejitenga(Akataka kutoroka)na amri yetu miongoni mwao tunamuonjesha adhabu ya moto uwakao."
Hivi ndivo tunavyojulishwa na Quraan kuwa jambo hilo lipo na linawezekana na wapo mpaka leo wanopewa taaluma hiyo adhimu ya kuweza (Kupaa angani), Walipewa pia Baadhi ya majini na Binaadamu katika zama hizo elimu tafauti kama tutakavo soma tukiendelea kuzichambua elimu hizi za Ajabu.
Sasa wacha tuiangalie Elimu hii ya kuruka au kupaa kama ndege ikoje, kwanza itatubidi tujiulize kwanini ukatajwa upepo? jee habari hizi zinatujulisha ndege za zama hizo? jee (Technology)hiyo bado ipo, Jawabu naam elimu hii bado ipo japo walo nayo kwa zama hizi wachache sana.
Nini Upepo? Upepo ni (Transport system)ya Ardhi yetu hii, Upepo kwa njia ya Rehma za Mwenye enzi Mungu ndio wenye kusafirisha maji kwa njia ya mawingu yakatolewa sehemu moja kupelekwa sehemu nyengine(Mvua) Upepo unasafirisha Mimea, upepo ndio tegemeo la vyombo vyote vya usafiri wa nchi kavu, majini na angani, hivyo vyote vinategemea upepo kwa njia tafauti kuweza kutekeleza kazi zake.
Na hizi Pepo zipo tafauti zipo za Misimu ya (Local, National, na Inaternational)zipo zinazoletwa kwa ghafla na zipo zinazodumu katika njia zake daima, zipo pepo hii za masafa marefu na masafa mafupi, zipo za juu sana na katikati pia na chini kabisa ambazo vyombo vyetu vya usafiri kama Jahazi ndivyo vinautegemea baada ya kubeba Marobota ya katani, na vyuma na saruji ikisha wakafunga kipande cha kitambaa hao kuelekea Mombasa kwa kutegemea upepo ambao hawana Amri nao wala kuwa na ujuzi nao sasa nini habari yako wewe kama utapata Elimu hii ya upepo na nini cha kufanya?.
Endelea Part 5

ELIMU ZA AJABU PART 5
Asalaam Aleiykum
Halafu kuna upepo mwengine ambao mmeugundua karne hii tulonayo labda miaka 40 na ushei ambao upo takriban ya masafa ni kama (Mile) Saba kwa juu, mkauita (Jet Stream)ambao unaizunguka dunia ambapo hata hizi ndege zirukazo zinautegemea katika kuruka nk, Kwa hiyo wakati wa Nabii Suleiman a.s na yeye alipata Elimu ya kufahamishwa (Mystic Stream)na mpaka leo wapo wenye kuigundua Elimu hii ya Kuruka ama kwa kuitafuta au kwa bahati unakumbana nayo, kwa hiyo zile hadithi ulokua unasikia Walii fulani kaachwa Mangapwani au Bagamoyo mkamkuta kafika mjini mwanzo bila ya gari usije ukashangaa.
Nini Kinatokea huyo katumia Elimu yake ya siri ya kupaa hewani, na safari hii ni nzuri hata kupita hizi safari za ndege au hiyo gari unayopanda. Na kwanini isiwe hivyo wakati wale wanoishi nchi za Ulaya wanajua kuwa Mtu anatengeneza (Kishada) au (Kite) au (Hang Glider) akenda kwenye Kilima au kichuguu na kujifunga mgongoni au kwenye mabega na kujiachia akacheza angani kwa masaa huku akipunga mkono, Kwa hiyo Elimu ya Kuruka ipo inatakiwa utekeleze masharti yake ili uweze kuimiliki, na ntalisema hili sharti moja na kuyaacha mengine ili watu wasije wakadhurika, Sharti lenyewe kwanza lazima umiliki elimu ya (Levitation) katika Ulimwengu huu zipo Elimu mbili moja inayotuweka kwenye Ardhi ambayo ni (Gravitation) na hii ya pili ni hiyo (Levitation) ya kupaa ukiweza kunyanyuka ukaugundua Upepo wa (Mystic Jet stream) na wewe utakua unafanya safari zako bila ya wasiwasi, lakini kikwazo chenyewe huwezi kupata elimu ya (Levitation) mpaka uipate elimu ya kupotea, ndani ya elimu hiyo ndio wanaishi Majini kama inavotaja aya ya 27 sura ya (Al-Aaraf)mpaka inapoishia.
إِنَّهُ ۥ يَرَٮٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُ ۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَہُمۡۗ
"Hakika yeye(Ibilis) pamoja na Kabila yake wanakuoneni, na hali ya kuwa(Nyinyi) hamuwaoni".
Hiyo ndio Elimu ya Ulimwengu wa majini wanaishi ndani yake kwa kutoonekana, hiyo ndio elimu ya kupotea, ipo kama vile mithili ya moto mwanzo unakua haupo na mara unauwasha unatokezea, ikisha ukiuzima unapotea sasa jiulize mwanzo ulikua wapi? na sasa umekwenda wapi?, ukijua jawabu lake basi utakua ushaanza kuipata elimu hii ya kupaa, ndio maana ukaambiwa Majini kwao Rahisi kuruka kwa kuwa wameumbwa kwa Moto Baridi, na wewe potea ukakutane na moto baridi ukoje? Potea ukakutane na elimu hii ya (Levitation), itakua Rahisi kuanza kusafiri kama wafanyavyo Mawalii (Mystic) na baadhi ya wengine wenye kutumia elimu hizi kwa ufisadi.
Endelea part 6

ELIMU ZA AJABU PART 6
Asalaam Aleiykum
Tunaendelea kupata habari hizi za elimu ya kuruka na napenda kukumbusha uelewe safari hii inafanyika nyakati za usiku, kwa kuwa ndio wakati muafaka wa kuingia katika (zone) ya (Levitation).
Ama kuhusu Elimu ya kupotea hii ni vigumu kufahamika kutokana na uhusiano wake wa karibu na Sayansi ya zama hizi, kama umeshawahi kusikia Sayansi ya (Time Travel)ambayo inazungumzwa na Wanasayansi wa kileo basi hiyo ndio elimu ya kupotea, ambayo wanasayansi wa kisasa wameigundua inawezekana lakini bado hawajajua inafanyika vipi, Na ndiyo ilotumika wakati wa Nabii Suleiman a.s kama ilivyotajwa katika Quraan sura ya (Naml) aya ya 38 mpaka 40,
قَالَ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمَلَؤُاْ أَيُّكُمۡ يَأۡتِينِى بِعَرۡشِہَا قَبۡلَ أَن يَأۡتُونِى مُسۡلِمِينَ
(Nabii Suleiman a.s akawakusanya wazee wa Baraza lake la Hekima)"akasema Enyi Wakuu ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha kusilimu.
قَالَ عِفۡرِيتٌ۬ مِّنَ ٱلۡجِنِّ أَنَا۟ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَۖ وَإِنِّى عَلَيۡهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌ۬
Mjasiri(Ifrit) mmoja wa Majini akasema"Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo(Ulipokaa) na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni Muaminifu.
قَالَ ٱلَّذِى عِندَهُ ۥ عِلۡمٌ۬ مِّنَ ٱلۡكِتَـٰبِ أَنَا۟ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن يَرۡتَدَّ إِلَيۡكَ طَرۡفُكَۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسۡتَقِرًّا عِندَهُ ۥ قَالَ هَـٰذَا مِن فَضۡلِ رَبِّى لِيَبۡلُوَنِىٓ ءَأَشۡكُرُ أَمۡ أَكۡفُرُۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّى غَنِىٌّ۬ كَرِيمٌ۬
Akasema Yule aliyekuwa na (Elimu) Ya kitabu, Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako(Kufumba na kufumbua) Basi alipokiona kimewekwa mbele yake alinena, Haya ni kwa fadhila za Mollah wangu, ili anijaribu nitashukuru au (nitakuwa mwizi wa Fadhila)Kukufuru, Na anaye shukuru, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake, na anayekufuru, kwa hakika Mollah wangu ni Mkwasi na Karimu.
Hiyo ndio Elimu ya Kitabu, elimu ya kuukunja (Wakati na Sehemu)(Appear and Dis-Appear) sio Mazingaombwe(Uchawi) Mnahadithiwa habari hizi za Mawalii(Mystic) mlokua mkisikia wanatiwa Gerezani lakini Usiku wanalala nyumbani, sala ya Alfajiri anasali msikitini halafu huyo anarejea (Mahabusu). Na Ukiipata Elimu hii ndio ushapata elimu ya kuonana na Majini na mambo mengine ya Ajabu, Unaweza sasa kuingia na kutoka Ughaibuni bila ya Mtu kujua, unaweza hata kumsoma Mtu Akili nini anawaza, Ametukuka Mwenye Enzi Mungu Mwenye kutukirimu elimu hizi za Ajabu.
Ama kuhusu Elimu ya kutibu wengine wanadhani huyo anataka kutibu Malaria akiwa mbali, kusudio langu ni kuzungumzia Elimu yenye kutibu tafrani hususan zenye kuhusiana na dhiki za Moyo na Akili, Na hili ni tendo ambalo wanaweza kufanya wale walopewa Hijaza na Mollah wao hata wakiwa mbali kwa kutumia sauti zao wakaponesha baadhi ya maradhi na kuondosha misukosuko ya dhiki za Moyo, ni jambo linalowezekana, kwanini lisiwezekane wakati unaweza kumsikia mtu kwenye simu aliyeko mbali bila ya waya kukamatana, na kama akikwambia nyumba yako imeungua unaanza kutokwa na machozi, na akikwambia nakulipa deni lako unajawa na furaha, nini kinatokezea? kinachotokezea hapo ndicho kile kile(Chenye kutokezea kwenye Dua), Na yule mwenye kujua kuponesha akajua kuitumia (Universal Mind)Ambayo hii tutaizungumza siku za mbele kwenye (Majaaliwa) basi anaweza kukutibu hata akiwa mbali, kwani maradhi ni yale yale anayotibu aliye karibu, au anayeomba aliyekaribu yote yanategemeana na mfumo wa (Dua) ndio maana wengine wanarekodiwa (CD) na kutibiwa, ni jambo linalowezekana na wala halina (Mushkeli wowote).
Ama kuhusu Elimu ya Kungara hii sitokwenda ndani sana kutokana vielelezo vyake ni virefu, lakini nitasema kwa kifupi Elimu hii inategemea vipi utaweza (kujikurubisha) au kuji(Tune) na mionzi ya Jua, na ukiweza kupata taaluma hii na wewe utakua unangara kama (Taa) na ukiwa mwanasiasa au Mtu wa kupenda vyeo hapo tena chaguzi zote unashinda wewe, na kila atokua karibu yako atakua mwenye kuvutiwa na wewe, lakini elimu hii ina kasoro zake na mbili katika kasoro hizo (Watu watakuwa wanavutiwa na wewe kimatamanio) Na kama huwezi kujizuia utakua na wapenzi hata elfu, na kasoro ya pili utakua katika hali ya umoto baridi (Mithili ya Majini), kwa hiyo utakua unaishi katika Ulimengu wa (Hasira) nyakati zote kwa kuwa sio (Nature yako).
Ama hii Elimu ya kutisha ni kama hiyo ya kungara ila hii imeambatana na (usiku) Giza, si unaona kila mtu anaogopa giza, ukiweza kuambatana ukaingia ndani ya (Dark matter)ukauingia usiku ukakuvaa, basi utakua unatisha mpaka watoto wako wakikuona watakukimbia, lakini ukifunikwa na mionzi ya giza tahadhari kwani utakumbwa na uvivu usiweze hata kunyanyuka kitandani, sababu kiza kinaletewa watu kupumzika na wewe unakitumia wakati wa mchana, kiza kishaondoka wewe umebaki na kivuli chake unatishia watu, hizo ni baadhi ya elimu za ajabu ambazo ziko nyingi, Na kama inavosema aya ikiwa utazitumia kwa manufaa ya uzuri basi ni fadhila kubwa kutoka kwa Mollah wako, lakini ukizitumia kwa ufisadi basi utakua umeangamia na kukufuru kukubwa, kwa sababu utakua unazitumia kinyume cha sheria.
Haya ni kwa ajili ya kukujulisheni uwapo wa Elimu hizi lakini cha muhimu zaidi ni kumuabudu Mollah wako na umuachie Mwenyewe ikiwa Kakupa Elimu hizi basi zitumie kwa manufaa na ukinyimwa basi shukuru wala usihangaike sababu utakua unanusuriwa na mengi. "Na wala hatukukupeni Elimu zetu isipoua kwa Uchache tu".

Subscribe to:
Posts (Atom)