Sunday, August 23, 2015

MARA UMEUSAHAU MARA UMEUKUMBUKA PART 2

Asalaam Aleiykum

Unasahau Kutii Amri zake, Unasahau kumkumbuka hata kwenye hiyo Sala unashindwa kumkumbuka, na hiyo ndio hali yetu sote (Isipokua wachache)sasa ikiwa wewe umo katika kundi hili la (Mara Umeusahau Mara Umeukumbuka)unatakiwa sasa ujifanyie Matibabu, Vipi yanapatikana Matibabu hayo?, Ndio nakwambia kachukue dawa kwenye (Sura ya Fussilat aya ya 30 na 31)

إِنَّ ٱلَّذِينَ قَالُواْ رَبُّنَا ٱللَّهُ ثُمَّ ٱسۡتَقَـٰمُواْ تَتَنَزَّلُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕڪَةُ أَلَّا تَخَافُواْ وَلَا تَحۡزَنُواْ وَأَبۡشِرُواْ بِٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِى كُنتُمۡ تُوعَدُونَ 
"Wale waliosema, Mollah wetu ni Mwenye enzi Mungu, kisha wakenda mwendo mzuri, hao huwateremkia Malaika(Na kuwaambia)Msiogope wala Msihuzunike na Furahini kwa pepo mliyokua mkihaidiwa"

نَحۡنُ أَوۡلِيَآؤُكُمۡ فِى ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِى ٱلۡأَخِرَةِ‌ۖ وَلَكُمۡ فِيهَا مَا تَشۡتَهِىٓ أَنفُسُكُمۡ وَلَكُمۡ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ 
"Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya Dunia na (Huku)Akhera, Na Humo mtapata vitu vinavyopendwa na Nafsi zenu, Na Humo mtapata mtakavyovitaka".
Kwa wale walosema Mollah wetu ndie Mlezi halafu wakafata Amri zote ziloteremshwa, basi wakisema na kukamata huo msimamo wa mwendo mzuri, upi msimamo wenyewe? wakuto kusahau amri zake, na kumkumbuka Yeye Mollah wako kwa kadir ya uwezo wako, basi cha kwanza kinachofatia unaondoshewa usahaulivu na kubaki na hali ya kukumbuka daima, kwani wakati wa kusahau ndio wakati unaotenda Dhanmbi, lakini ukiwa katika hali ya kukumbuka hutendi dhanmbi abadan, na huo ndio "Uislam" mimi na wewe hatukua na haja ya kusema kauli hiyo kwa kuwa tumezaliwa ndani ya Uislam, lakini jee tumeishi Kiislam?.
Wacha basi nikujulishe maana na kusudio ya kauli hiyo, Kauli hii inatamkwa na yoyote yule ambaye Roho yake iko tayari Ku(Surrender) ni kauli ya badiliko la (conciousness)yako kuwa sasa mimi nishagonga ukuta, hapa nilipofika basi tena, na sasa nimekubali nafata amri zote wala sitoiacha hata moja Mollah wangu, mwanzo ni umo tu ndani ya Uislam ila sasa umeamua kuwa na Imani thabit ya Kiislam.
Umeamua kuanzia sasa kutambua Kiroho kuwa Mollah wako ndio alokuumba na kuanzia sasa unamuachia kila kitu yeye ndio awe mlezi wa matokeo yake, Sasa Roho hii yenye kuona haya inafikia vipi kugundua hilo?. Inatafakari Roho yako kwa nguvu za Fikra na kuzingatia(Mfano) Ufalme wa maisha ya Vinyama, kama Ndege au Kuku umtizame kwa undani kabisa utaona hata vinyama hivyo vina Family zao, vina makaazi yao, vina tafauta riziki kama mimi, vinalisha watoto wao, na wanyama wengine wananyonyesha, Mpaka Samaki hali kadhalika,vikiumwa ndie Yeye Mollah wangu anaviponesha,Vinyama hivi vinacheza kwa Furaha, vinalala kama ninavolala, ukiona hali hiyo kwa kutumia Roho yako na siyo Akili yako,Ndio unasema vyote hivi viko kwenye Rehma, Baraka na Neema ya Mwenye enzi Mungu, Nini hali yangu mimi nilopewa uwezo wa kumjua Mollah wangu? Mbona (Mara Nimemsahau Mara Nimemkumbuka)Basi ukigundua Ufalme huo lazima ujiulize kuwa hao hawakupewa uchaguzi huu, na mimi nimepewa uchaguzi wa Ima kusahau au kuchagua kukumbuka, basi kutokana na hali hiyo sasa Mollah wangu nakuachia kila jambo langu wewe ndio uwe Muamuzi wake, Na mimi nasimama kwenye njia ilonyooka yenye haki.
Huko ndio kukiri kwa Roho(Kauli ilotajwa mwanzo wa Aya), na kuamini kwa vitendo kuwa hakuna kinachotendeka isipokua kwa uwezo wa Allah, na unatakiwa useme kwa kutumia Roho yako na sio ulimi wako, basi ukiweza kutamka katika Roho yako ukawa umenuia kuisimamia Haki, Basi hapo hapo unateremshiwa (Body Guard) Kwanini inaitwa (Bodyguard) kwa sababu dhumuni kubwa ni kuulinda huo Mwili, lakini hao wanakua wa Kibinaadamu wanalinda nje lakini (Malaika) wao wanakulinda nje na ndani, vipi wanafanya hivyo?
endelea part3

No comments:

Post a Comment