Sunday, August 9, 2015

ZAWADI KUTOKA MBINGUNI PART 1

Asalaam Aleiykum

Mwenye enzi Mungu ni mwenye kumimina Zawadi za kila aina kwa waje wake, ziko nyingi kubwa na ndogo za kila aina, lakini leo nataka kuzizungumza hizi tatu zenye kumfanya Mwanaadamu awe furahani, awe kila saa na dakika yumo kwenye hicho kitu kiitwacho (Bliss) ikiwa ataweza kuyapata mambo matatu haya kwa pamoja. basi atakua Mwenye kufuzu kuliko kukubwa,
Mambo yenyewe ni "Mapenzi", "Imani", na "Huruma".
Nikiangalia Jamii wakati huu tulo nao yananijaa masikitiko moyoni kuona sio watu wengi wenye kuzipata neema hizo tatu zilizo muhimu, Nini kimetokezea?.
Naweza kuhadithia lakini siwezi kufanya tathmin ya mambo yalivo haribika katika kipindi kifupi cha miaka 40 ilopita, Sisi tuloshuhudia mwisho mwisho tulikuta bado japo kwa uchache "Mapenzi, Imani na Huruma"zimo kwenye nyoyo za watu, Na ulikua ukiwauliza walikua hawana jawabu la kukupa, isipokua wanakujibu tulishikana, tulikua kama ndugu, tukisaidiana, tukipendana, hilo ndio lilikua jawabu lao.
Ukumbuke uzuri enzi hizo elimu ya Dini ilikua haipatikani kirahisi, si watu wengi walokua wakisoma madrsa au kusikiliza mawaidha, sasa nini kilikuwepo wakati huo?. Kilokuwepo wakati huo ni hicho kitu kiitwacho "Imani", Na huwezi kujua kama kilikuwepo mpaka uisome aya hii iliyomo kwenye sura ya (Hujurat aya ya 14)

قَالَتِ ٱلۡأَعۡرَابُ ءَامَنَّا‌ۖ قُل لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ وَلَـٰكِن قُولُوٓاْ أَسۡلَمۡنَا وَلَمَّا يَدۡخُلِ ٱلۡإِيمَـٰنُ فِى قُلُوبِكُمۡ‌ۖ وَإِن تُطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُ ۥ لَا يَلِتۡكُم مِّنۡ أَعۡمَـٰلِكُمۡ شَيۡـًٔا‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ
"Walisema Waarab (Wanokaa jangwani)tumeamini, sema (Uwaambie)hamjaamini, lakini semeni tumesilimu, maana Imani haijaingia vyema nyoyoni mwenu bado. Na mkimtii Mwenye enzi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu(Thawabu), kwa yakini Mwenye enzi Mungu ni mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu."
Katika mtizamo wa aya hiyo inaonekana Kusilimu kuna kuja mwanzo(Surrender) na ukisilimu tu unapewa zawadi itokayo Mbinguni nazo ni moja katika hizo tatu(Na ukiona huna katika hizo tatu basi jijue huja Surrender)Nawauliza baadhi ya Masheikh, hivyo wewe Sheikh mzima hebu nipe ukweli mbona naona tabia zako zina Mushkeli, hivyo katika matatu hayo kuna chochote kilichotokezea katika nafsi yako, Jawabu hakuna, utawaona Masheikh mawaidha makali, maneno mengi lakini hajawahi katika nafsi yake kupata Mapenzi, Imani wala Huruma, hao ndio Masheikh wana hali gani Maamuma?.
Naam wakati huo ulopita ndio ulokua wakati wa hizo (Bidda hassan)zimekithiri, ulikua wakati wa (Madhikiri, wakati wa Maulid, wakati wa Mahitima, wakati wa Manyiradi) wakati huo ndio ule watu walofungamana na Hadith sahihi ya Bwana Mtume s.a.w ilosema "Yoyote yule atakae leta jambo zuri katika Uislam atapata ujira wake kwa jambo hilo". Nimefurahi hivi karibuni kuwasikia wanazuoni Wakubwa wa Kiislam kwenye Baraza la Eid lilofanyika Abu Dhabi wametoa wito au (Fatwa) wakitaka turejee kwenye zile zama za (Bidda hassan), kuliko kubakia kwenye nakama na Moto tulo nao hivi sasa wa uharibifu wa Dini hii ya Kiislam, Makala hiyo iloandikwa kwenye (AP-na Yahoo tarehe 19 July ninayo au mtu anaweza kufatilia akasoma mwenyewe).
Naam Tunaendelea na Darsa yetu ya kutaka kuelewa  wapi vitu vitatu hivi vinatokea, tunajikumbusha zama zilopita watu wakiwa wame(Surrender) walipata zawadi gani kutoka mbinguni?.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment