Sunday, August 9, 2015

ZAWADI KUTOKA MBINGUNI PART 2

Asalaam Aleiykum

Katika zama hizo  kulikua hakuna magonvi ya dini wala madhehebu, Hakuna ubaguzi huyu Mkiristo au huyu Baniani au yule nani, nakumbuka mpaka vijana wa Kikiristo  walikua wakila halua misikitini mwetu, sisi tukisoma vitabu vyao na wao wakisoma vitabu vyetu, tulikua hatujui hata maana ya madhehebu ndio nini?.
Tukiona wazee wetu wakichanganyika na watu wa kila aina, wakishirikiana katika kila jambo, Watu walikua wame (Surrender) mambo na hukumu zote wamemuachia Mollah Muumbaji, Heshima na adabu zikitawala wakati huo, Watu walikua wakijizuia na Machafu na Uzinifu, Na ukijizuia na Uzinifu unakua unaondosha jambo la (Sex) kutoka chini na linakwenda juu kwenye Akili(Mind)na kugeuka (Romantic), ndio maana utaona Watu wa zamani Nyimbo zao, Mashairi vyote vizuri mpaka lugha yao ilikua na (Romancy) ndani yake.
Sasa wacha tuanze Darsa yetu kukijua nini kilotokea baada ya hapo hata mambo yakenda (Wrong) au kuharibika. Kilotokea baada ya hapo hakielezeki kwa maneno matupu, amekuja (Ibilis) na kutuonesha Mti wa elimu, akatwambia mkila tunda lake mtakua wasomi, Naam tukaonja tunda lile na ndio lilipotufikisha hapa tulipo leo, jambo la kwanza tulolifanya ni kuondosha yale yote yalo wafanya Umma wa wakati huo (Usilimu) au (Surrender).
Haijambo wazee wetu waliridhia matakwa ya Mwenye enzi Mungu, wakapata kitu tunaweza kuita (Romantic way of life), Sasa nini tulopata sisi tulosoma, elimu zetu zimetupeleka kuondosha yale yote yalokua yamewafunga na kuwalea Umma hizo zilopita, nini kimetokezea?, Hakuna tulichokipata ila ni (Split Mind) mgawanyiko wa Akili, ukiacha kufungumana na Mollah wako unapata mambo haya mawili ima werevu wako na Elimu usoijua itakupanda juu ikupe kiburi, au itashuka chini ikusahaulishe Mollah wako na igeuke (Sexually), ndio maana unaona sasa tumegawika makundi mawili .
Kundi la kwanza limejifunga kwenye (Sex) na kundi la pili limejifunga kwenye (Disturb Mind) na kujiona wao ndio wako (Perfect) katika mahusiano na Mwenye enzi Mungu wao, yote hayo ni matatizo na mashaka makubwa, maradhi yameingia kwa wenye kufata dini na wenye kuendekeza dunia, sijui nani ato mtibu mwenzie. Kwa sababu Mwanaadamu akijifunga kwenye (Ngono)basi Maisha yake yanakua sawa na mnyama, mnyama hana mapenzi inakua tafauti yako wewe unajificha na mnyama anafanya hadharani, lakini huko kujificha kwako kunakua kimwili(Body) lakini kwenye Akili(Mind)unakua kama Mnyama, ukilishiriki jambo hilo kila kitu kinaondoshwa unakua huna Mapenzi, Imani wala Huruma.
Na hili kundi letu sisi wenye kujifanya tuna funguo za Pepo na kutoa Hukumu ndio tunamilikiwa na chuki na (Confused Mind) tunaanza kupata (Haluccination) huyu ndie huyu sie, tunapata ugonjwa wa Kiburi hatujui nini Mapenzi, nini Imani na nini Huruma. Vipi leo uwe Mtu wa Dini halafu uwe katili, huoni kama sote tunateseka, ndio mwisho tunaishia kujidhuru wenyewe au kuwadhuru watu wengine wasio na hatia.
Swali la kujiuliza mbona huko nyuma hayakuwepo mambo haya katika Ulingo wa Dini?.Kwanini tuteseke?, hivo hakuna njia nyengine za kujivua kwenye mateso haya?, jawabu njia nyengine ipo nayo ni kujitahidi uyapate mambo haya matatu"Mapenzi""Imani"na "Huruma" utakua umepata zawadi itokayo Mbinguni na hutoteseka tena.
Endelea part 3


No comments:

Post a Comment