Asalaam Aleiykum
Cha Msingi kama walivosema hao Wanazuoni turejee kwenye zama zilopita kwenye Mapenzi, Imani, na Huruma. Mwenye Enzi Mungu anasema katika sura ya (Anfal aya ya 53).
ذَٲلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ لَمۡ يَكُ مُغَيِّرً۬ا نِّعۡمَةً أَنۡعَمَهَا عَلَىٰ قَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِہِمۡۙ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ۬
"Hayo ni kwa sababu Mwenye enzi Mungu habadilishi kabisa neema alizowaneemesha watu, hata wabadilishe wao yaliyomo nyoyoni mwao, Na hakika Mwenye enzi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kulijua kila (Jambo)".
Na kweli tumebadilisha kila kitu kwenye Ulimwengu wa leo,
Tizama kwenye nyoyo yako kiko nini?, kama umeshika Dini basi umejaa chuki, ghadhabu na ukatili, na kama umeshika Dunia basi ni (sex) wizi, dhuluma hakuna jengine ama uko pembeni ya kushoto au katikati ya kushoto lakini mwiko kwako kuwepo upande wa kulia.
neema ndio zimeondoshwa, hakuna tena neema ya mapenzi wala imani au huruma. Sasa ukitaka kubadilika lazima ujue nini Mapenzi, na yanatokea wapi?.
Quraan (Al-Room aya ya 21)
وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ
"Na katika ishara zake nikuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, na amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri".
Lazima uwe Mtu Mwenye kufikiri vipi utayapata mapenzi, na kwanini kitu hicho kitajwe kuwa utulivu, sababu kama huna mapenzi unateseka ndio nikaita(Split Mind)Mchafu koge. Na Bila shaka zimo ishara, ishara zenyewe lazima utulie, ndio utaona nini raha ya mapenzi, nini faida ya huruma, na nini busara za Imani, ukiweza kuyajua hayo unaweza kurudi kama zamani, au ukaishi na mazuri yaliyokuweko wakati huo.
Kama tulivo ona katika hiyo (Aya) kuwa mapenzi yanatokea kwa Mwenyewe Muumba wa Mbingu na Ardhi, kuna kitu kinatokea ndani ya (Ufalme wa Uhai wako)unaoitwa(Being),Kitu hichi mapenzi,huruma na imani hakipatikani kwa ukamilifu mpaka utimize masharti yake, utajiuliza masharti gani hayo?. Kwa kifupi ni (Taqwa) Kwa lugha ya mzunguko ni uwe (Pure)huna chuki au hamaki, sio (corrupted)na mambo yoyote machafu au dhuluma, kusema uongo, uzinifu na kiburi, (au soma darsa ya pepo ya dunia katika yale mambo 10 niloyataja uyawache)ukiwa huna vitu hivyo ndio Mollah wako anakuteremshia zawadi yake kutoka Mbinguni nayo ni hiyo (Tatu kwa moja).
Matatizo yanatokea unapoamua kujichafua na kugawanya hiyo zawadi na kuifanya ya mafungu tafauti, Mapenzi yakishuka huwa yanakuja (Full pack) ndio ikasemwa kama utakua Mja mwema ukatulia ukawa hufanyi machafu yoyote basi ukioa au kuolewa moja kwa moja unateremshiwa zawadi hii ya mapenzi.
Sasa Mapenzi yanatokea wakati gani?
Wakati ule Akili(Mind)inapokutana na (Heart)Moyo, kwanini nikaitaja Akili mwanzo kwa sababu Akili ni ngumu sana kukiri, mpaka ikakubali kushuka chini na kukutana na moyo hapo ndio inapatikana hiyo (Surrender)unakua (Muslim + Muumin) kwa wakati mmoja, unatokezea mripuko wa wewe kupotea, na penzi pekee kutawala maisha yako. Basi neema ilioje ikiwa wawili nyie mepata kupokea hiyo zawadi kwa pamoja, Hakika huyu anamuona mwenzie (Lulu Maknoon) na wewe unamuona mwenzio (Mukhaladun) mnapotea kabisa katika Ulimwengu huu na kuishi Ulimwengu mwengine kabisa, basi nini habari yetu sisi ikiwa viwili hivyo yaani Moyo na Akili vikiungana na hicho kitu cha tatu ambacho ni Roho, hapo kinazaliwa kitu kipya kabisa, inapatikana sasa (Unity). Mapenzi yanabebwa na Moyo, Imani inabebwa na Akili, na huruma inabebwa na Roho vikiungana vitatu hivyo au ukipata nafasi kuviunganisha basi hapo hapo matatizo yote yanakwisha.
Unakua mtu wa aina nyengine kabisa, tamaa inapotea kabisa katika maisha yako, unakua maridhia,unampenda kila mtu, na watu wanakupenda isipokua wale wenye matatizo, wao watakushangaa lakini wewe Mwenyewe unajua nini kimetokea ila unakua huna amri katika hiyo (Unity) ilotokezea, hapo tena Sala zako zinabadilika, Maisha yako yanabadilika, Unapata Nuru, na hiyo Nuru huwa inamurika kila mtu kwa mapenzi yako, kwa ukarimu wako, kwa huruma zako, kwa usaidizi wako, kwa usafi wako wa nafsi, pamoja na Ucha Mungu wako, na wala husubiri tena mpaka ufe ndio uombewe kaburi lako litiwe nuru, ukipata zawadi hiyo ndiyo ushapata chanzo cha Afya na Furaha ya maisha ya Duniani na Akhera.
Hapo tena Mapenzi yako yanakua ya aina nyengine kabisa unabadilika kukipenda kile kisicho onekana na hiyo ndio Imani, Na pia unageuka kuvipenda vyote vyenye kuonekana na hiyo ndio Huruma na yote hayo mzizi wake ni mapenzi na huo ndio Ucha Mungu na ndio Mwenendo wa kila mwenye kuifata Dini ya haki.
No comments:
Post a Comment