Sunday, August 23, 2015

MARA UMEUSAHAU MARA UMEUKUMBUKA PART 1

Asalaam Aleiykum

Unapokwenda Hospital jambo la mwanzo unafanyiwa uchunguzi wa vipimo ili upate kujulikana unaumwa nini, Na Mimi leo katika darsa ya leo nimekuja na (Thermometer)langu ili nipate kukupima, nipate kujua na kukujulisha jee maradhi haya ya (Mara umeusahau mara umeukumbuka)unayo?. Na kama unayo basi wakati wa kupewa dawa ya kuyaondosha ushafika.
Sasa ni kitu gani hicho mara umekisahau mara umekikumbuka, maradhi haya unaweza kuyaita kwa majina mengi, lakini nakupa (mfano)wa matatu haya ambayo yatakuwezesha kujua kama kweli umekamatwa na maradhi haya. Sasa yaite upendavyo lakini la mwanzo kabisa ni Mollah wako, halafu linafatia Uislam wako na la tatu ni huo Ucha Mungu wako, hivyo ndio vitu ambavyo (Mara unavikumbuka mara unavisahau).
Sasa wacha tuangalie kabla ya kufanya uganguzi ni vipi Maradhi haya yamekuzunguka, Tuchukue (Mfano)wa kwanza(Uislam wako)umeutizama kwa makini katika mwenendo wako wa maisha, huoni kama unalivaa na kulivua koti hilo la (Uislam),Vipi inakua hali hiyo?, Ukenda kinyume na Amri yoyote ya Mollah wako wakati ule unakua (Umeusahau Uislam wako)Mfano:Umetoa au kupokea Rushwa, Unaiba kwa Mtu au kwa Watu au Serekalini, Uzinifu, Ukijaa Chuki, Ukisema Uongo, Kutegemea Waganga, Na Mengi mengineyo ya Ufisadi wakati huo wote unakua (Mara Umeusahau) Kwanini nikasema Mara, kwa sababu Mara nyengine Unakumbuka unarejea kwa kufanya Toba ndio nikaita (Mara Unaukumbuka)Uislam wako.
Hiyo ndio hali tulonayo sote, tumo kwenye kuyumba na lengine ama niite la pili ni hili kwenye(Ucha Mungu)wako, utafanya Ibada , utakua Mtiifu, Lakini wacha upate mtihani kidogo au Mtu akukwae, jiangalie vipi unavua ngozi ya kondoo, Watu wanakushangaa mbona kageuka chui, ana nini huyu? Huyu si Mcha Mungu, mbona hataki kusaidia wenzie, mbona matusi yanamiminika, umesahau kuwa wewe wiki ilopita ulikua (Mcha Mungu), vipi wiki hii hutaki kumsamehe Mtu, hutaki kuzungumza na Mtu, na ukifikwa na Mtihani wa kukosa cheo au Mali, au kula hasara au umekosa Mke au hujaipata kazi unayoitaka, hapo ndio mama wee unatizama Mbinguni kwa hasira, uso umeukunja, sala zote za sunna unaacha(Mara Umeusahau Mara Umeukumbuka).
Na Jambo la Tatu ni hilo la Mollah wako ambaye amekufanyia hisani ya kukuumba ukiwa Muislam, kutokana na yeye ukashuhudia hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokua yeye Mollah wangu Mlezi, Na kwa kila kitu changu mimi na (Surrender)Nasilimu, Nakua Muislam kwa vitendo na mwenendo wa Tabia sasa Inakuaje (Mara Unamsahau mara Unamkumbuka)?
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment