Asalaam Aleiykum
Sasa litizame Neno kuoneshwa (Tupu zao)hiyo ni (Symbol), Tulikua hatujui tukapewa (Fahamu)au(Knowledge)lakini cha muhimu kwa mara ya mwanzo tuliweza kujitizama (Nafsi)zetu, na tokea hapo sio Watu wengi walo rudi nyuma kujitizama tena nafsi yake, Imeingia tafaruku ya kuzitafuta Raha za Dunia Mtu yuko tayari kuchupa Motoni lakini asikose Raha za muda mfupi.
Kitu cha kukiangalia hapa ni lile tukio, lakini naomba tulitizame (Kisomi)sio(Kivitendo)kutokana na kuoneshwa huko inatulazimu tuelewe kwamba(Fahamu)zetu zina uwezo wa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, Tuna uwezo wa kuona nje na kuona ndani kwa wakati mmoja, Unaweza kukitizama kitu nje na ukajiona wewe Mwenye kutizama, hiyo naita mimi (Double take)zinoangalia nje ni Fahamu na zinoangalia ndani ni Fahamu.
Sasa ukiweza kuangalia vyote viwili kwa wakati mmoja hiyo ndio (Awareness)na hiyo ndio itakufanya (Uishi bila ya Dhanmbi), Sasa ufanye vipi kuipata hali hiyo?, kwa sababu mpaka umri ulofikia mafundisho mengi yameshaingia katika kichwa chako huna haja tena yakuleta nyudhuru tena, kila kitu kimo ndani ya (Mind)yako, kwa hiyo Sasa inabidi uanze kufuta yale yote yaloandikwa kichwani mwako, vipi utafuta?, kwanza lazima uelewe (Mind) yako ina mtindo wa kurejea mambo, sababu ni kama (computer)haina jambo jipya, kwa hiyo ukijichunguza utajikuta hata hizo dhanmbi zako sio mpya ila za kurejea rejea.
Sasa kuanzia leo Dhanmbi zako wewe unazijua, kama atakujia Mwanamke au Mwanamme katika jambo la la Matamanio, basi usimtizame huyo alokujia pekee jitizame na wewe nini kinatokezea ndani yako, kumbuka kila kwenye (Action) lazima iwepo(Re-Action) Na vyote viwili wewe unavishuhudia, na hiyo ndio maana ya kila "Mwanaadamu anaiona Nafsi yake".
Basi ukishalijua hilo sasa ukitaka kupokea Rushwa mtizame mtoaji jitizame na wewe ni kimaanisha tizama (Mind)yako nini kinatokea?, Ukisema Uongo pia wakati unausema itizame nafsi yako inavodanganya, hata ukiwa unalewa umekamata chupa basi jiangalie mvinyo unavokwenda ndani, ukipata hamaki tizama nini kinatokea ndani yako, ikiwa unakwiba umebobea kwenye wizi basi wakati unakwiba tizama ndani huyu nani anofanya wizi huu, na pia ukiwa unazini au kufanya maasi yoyote yale usisahau kujikumbuka na wewe mfanyaji, kuna wakati ukijikumbuka kuwa wewe ndio mfanyaji ghafla utasita na hutotenda tena hilo tukio na hapo ndio Akili inapotea.
Najua nikisema (Akili) inapotea kuna watu watashtuka, Naam lazima ushituke, Akili kupotea ni mambo makubwa inabidi nikufahamishe vizuri usije kikakupata kisa kama kilichonipata mimi huko kwetu Tanzania.(Ngoja nikupe mkasa huo japo kidogo)nilikua mapumzikoni nyumbani nikawa nimekaa na vijana kwenye baraza"Akapita kijana nikaambiwa mzee unamuona huyu kijana kapoteza saa"mimi nikamuonea huruma nikasema twendeni tukamsaidie nikawa wa mwanzo kunyanyuka"wale vijana nilokaa nao wakaona maskini sasa tumepata wagonjwa wawili"hiyo ni kwa sababu mimi sikuelewa kupoteza saa kumbe ni maradhi ya Akili", basi wacha nifafanue vizuri tusije sote tukapoteza maana.
Huku kupotea kwa Akili kuko kwa aina mbili, Aina ya kwanza Akili inakwenda Ardhini na kukaa kwenye(Body), ndio utasikia kazama ama ana wazimu wa kutafuta mali, au ana wazimu wa wanawake au wa wanaume, au utasikia pombe imemuharibu Akili, na mwisho utasikia kapata maradhi ya wazimu au akili imeshindwa kuchukua amerukwa na Akili, na Akili ikiruka ndio Mja haponi tena, kwani inakua Akili ishapotea lakini sio kwa hiyari .
Aina ya pili nakuomba uifahamu kwa uangalifu Akili ipo lakini unaipotea, au unakwenda (Beyond)unakua tafauti na Akili yako, au unakua (Master) na hiyo ndio tafauti yake, na huyu Mwenye kui(Master)ina maana akili yake imekwenda(Mbinguni)juu, na huko ndio (Kumcha Mungu)Na huyo ndie Mwenye kuangalia Nafsi yake ambaye anaishi bila ya (Dhanmbi), kila kitu anakiona (clear)mnapata mifano midogo midogo, kwani wewe kuna mambo mangapi umeyawacha unajua kwanini?umekwenda (Beyond)lakini bila ya kujijua, unaacha ulevi, unaacha uzinifu (something happen)lakini hujijui, nifanyacho mimi sasa hivi ni kukumbusha tu, lakini isiwe umeacha mambo hayo kwa ajili ya maradhi au sababu zengine huwezi kufanya, kwani ukifanya hivyo bado utakuwepo Ardhini, bado huioni nafsi yako, bado unatufanyia ujanja ujanja,unaacha mbele za watu lakini kwenye Akili yako kutwa unazini, unasema uongo,unalewa, unatakiwa uwache kwa kuipotea akili yako kwa kwenda (Mbinguni)(Beyond)Mcha Mungu ikimbie Akili hiyo mpaka watu wakikutizama wanajua siku hizi hachezi mchiriku, hatizami senema za mambo machafu, kaacha kusema uongo na mengi mengineyo. Vipi utafanya hilo ni kwa kuamua kwenda (Beyond). Ufanye vipi?
Kumbuka katika chochote chenye kutendeka kuna mambo matatu yanatokea, (Mfano)unataka kufanya Uzinifu, Mwanamke au Mwanamme kashakuja unataka kufanya kitendo, jambo la kwanza mtizame huyo "alokuja"(1)Halafu kuna Akili yako ilojaa Shauku(2), na Jambo la tatu(3) na hilo ndio muhimu ukiweza kulikumbuka hilo lenye kuona hayo mawili ya mwanzo hilo ndio wewe", Ukiweza kulikumbuka hilo bila ya kuleta dharura ya kulisahau au kulipuuza hapo ndio utafanikiwa kuigundua au kuifahamu maana ya kila "Mja ni Mwenye kuiona Nafsi yake", na hiyo ndio (Pure Being). Na hapo utaweza kuishi bila ya dhanmbi, na hicho ndicho chenye Mapenzi, Afya, Furaha na matumaini.
Hicho ndio kile kisichoguswa na Maradhi wala kero na hata dhiki, na hii ndio maana ya "Tafsiri ya hizo aya mbili""Bali Mwanaadamu ni Mwenye kuiona Nafsi yake""Japo analeta Nyudhuru".
Nakupa dawa uifanyie kazi, lakini kama utaendelea kununua (Kaseti)zikupe nyudhuru za mawaidha mazuri basi endelea, lakini hii ndio haki na huu ndio ukweli.
No comments:
Post a Comment