Sunday, September 20, 2015

JUU MIUJIZA CHINI MIUJIZA PART 1

Asalaam Aleiykum

Napenda kuwapa taarifa wale wenye kufatilia darsa zangu kutokana na shughuli za Kifamilia, Kijamii na Kikazi huenda mkashuhudia upungufu wa Darsa zangu, hilo limetokana na ongezeko la shughuli za uwajibikaji wangu katika hayo mambo matatu niloyataja, na asije akadhania mtu hii ndio darsa yangu ya mwisho au akaona Bahari imekauka Inshaallah penye Uhai tutaendelea kupeana yale ambayo Mollah wangu ananipa mimi nijifunze kwa ushirika na nyinyi.
Naam ikiwa wiki hii tunashuhudia kilele cha Ibada ya Hajj wacha na sisi wenye kutamani tulizungumze tukio hili kwa undani wa hali ya juu kabisa na upeo mwengine tafauti na ule ulozoea, Kwanini nikasema hivyo, kwa sababu mimi ntakufahamisha tukio moja tu ambalo litabadilisha muono wako na uangalizi wa mambo ya Ibada hii kwa Jumla, Na kama utakua utagundua mapya yakaingia katika fahamu yako, basi ijue hiyo ndio Darsa. Sasa nini maana ya neno hili Darsa?, Neno hili limetokana kwenye Lugha ya Kihindi kumaanisha Mkusanyiko wa kuwa karibu na Mwenye enzi Mungu.
Kama utaniuliza mimi nini Hajj ntakwambia Hajj ni ile siku ya Mkusanyiko wa Arafa, ukikosa Arafa  huna Hijja, lazima ukahijji tena. Sasa kwanini Ikawa Arafa hii ndio inatuchukua kwenye Darsa yetu ya leo ya (Juu Miujiza chini Miujiza). Pata faida hii na wewe ukoge kwenye Bahari ya Miujiza ili ubadilike uwe Mtu wa aina nyengine kabisa, yajue mambo ili na wewe ukenda (Makka) ujue kumbe (Juu Miujiza chini Miujiza)Na kama ilivo desturi yangu naazima aya mbili kuizungumzia hiyo Miujiza ya Arafa.
Najua itakua tafauti na zile ulizozoea kuzisikia  zikiizungumza Ibada hii ya Hajj, lakini ni lazima wengine tupite njia tafauti ili nipate kufika kwenye ufalme wa fahamu yako.Na hii itakufanya kila ukiisikia aya hii itakukumbusha mengi kama inavofanya kwangu mimi inazidi kunipeleka (Deep)na mwisho wake siujui, basi ikiwa unataka kuungana na mimi endelea part 2

No comments:

Post a Comment