Asalaam Aleiykum
Binaadamu hapo ulipo una mizigo mingi, dawa haiwezi kufanya kazi kirahisi mpaka uipunguze ili uwache nafasi (empty)mapenzi yaje kukaa sio kupita kwenye moyo wako, Utafanyaje?.Cha kwanza kukumbuka wewe ni (Kinyama)Niseseme hivyo ukaona natukana, ikisema (Biology)ndio inafundisha, Kumbuka sote ni Vinyama, tafauti yetu sisi tumepewa mitihani, na makosa au kutofaulu katika Mtihani huo ndio kuna kunyima mapenzi na furaha.
Sasa ikiwa umewakosea Viumbe wenzio basi jambo la mwanzo kulifanya kaombe msamaha kwa kila ulomkosea unayemkumbuka , kumbuka mwanzoni mwa Darsa tumezungumzia jambo la (Kujua) kwa hiyo ukenda kwa Mtu kwa moyo mkunjufu, ikawa (sincere and humble)bila ya jeuri, ukakiri kwa kujua kosa lako na yeye alokukosea akajua kwa njia ya haki kweli umekuja kuomba msamaha hapo inakua kazi imemalizika, mzigo umeshatua,(Kujua inageuka kujulikana)na tatizo hilo linamalizika nafasi inakua(Empty).
Ikifikia hali kama hiyo basi jua kama atakusamehe sawa na kama hajakusamehe huo unakua ugonjwa wa Roho yake, Ikisha geuka nyumbani kwako kwa Mkeo au Mumeo huko ndiko kwenye shina la matatizo yote ya kukunyima Raha, fanya siku maalum ugeuke Babu jinga umuweke kitako Mwenzio umuombe Samahani, mwambie macho yameniponza lakini kuanzia leo sitizami nje ntakua naangalia ndani, nilikua nakupuuza wewe (soul mate)wangu kwa hilo nisamehe, Mpaka watoto waombe samahani usipande Kiburi ndicho chenye kukuzuia usiyapate mapenzi na Furaha ya Roho, anza kutumia wakati wako na Mkeo, Wanao, cheza na familia yako, msaidie watoto na kazi za nyumbani, usione aibu ukiambiwa kupiga deki piga, fanya chai mfanyie chai,zoa taka zizoe, Wallahi ukiwa unafanya kwa Ridhaa yako kidogo kidogo kuna mambo yataanza kukushukia moyoni mwako utashangaa yanatokea wapi, ifanye siri yako, ukibubujikwa na machozi usijizuie yaache yatoke.
Basi zidisha furaha na watoto wako, usiwafanye wakuogope, kuwa nao karibu, wafanye marafiki zako, kidogo kidogo utaanza kuona unapona Furaha inarudi kwenye Roho yako, alama za kukunja uso zinapotea, utaanza kujua nini maana ya Samahani, Samahani haina maana yoyote huku nje, lakini ndani ina thamani kubwa, Samahani ndio hiyo (Emptiness)nini kinyume cha (Emptiness)ni hiyo (Fullyness)Samahani imejaa mapenzi ndani mwake, kwani hujawahi kusamehewa ukajiona unakuwaje?.
Mwalimu akikusamehe au mzazi unahisi nini?, Jee Mtu akikusamehe Deni unakua katika hali gani, sasa ikiwa Mwanaadamu mwenzio anakupa furaha ya dharura kama hiyo nini habari yetu sisi unaposamehewa na Mollah wako?.
Mollah ambaye amewapa mapenzi yake wanomuasi kuliko wewe, anawapa majambazi na wahalifu, anawapa wauaji na wanaodhulumu, hali gani inakua inakua kama wewe utakaa msikitini au nyumbani kwako chumbani ikawa unakumbuka Dhanmbi moja baada ya nyengine na kila ukikumbuka basi unasali Rakaa mbili za Sala ya Toba, usifanye uvivu kabisa, na kila ukisimama Utamuomba Mollah wako kama hivi "Ewe Rabbi Mollah wangu hakika mimi kwa yakini nimefeli Mtihani wako, Na najua kwa yakini nimefanyaa jinsi kadhaa wa kadhaa, basi kwa dhati ya uwezo wako uloniumbia mimi nakuomba Mollah wangu unisamehe", utaomba hivyo ndani ya kila sijda.
Baada ya kufanya hayo kwa kadir ya uwezo wako wa kukumbuka makosa yako, na ikiwa maombi yako ilikua ya Ikhlas basi baada ya siku chache au hata zisifike utajikuta umerejea kwenye(Emptiness)kama (Mtoto)huna mzigo, na hapo tena ndipo utajua (Kilichofanyika kimefanyika)huwezi ku-(reverse)na ukijua hivyo muda huo huo ushapata matibabu(Depression)zinaondoka kwenye Roho.Furaha inaanza kukuteremkia na furaha ikiteremka wakati wowote mapenzi yanaweza kukushukia, unachotakiwa hivi sasa usubiri kwa kusali, Usubiri kwa kuwakumbatia na kuwasaidia mayatima,usubiri kwa kuwalisha masikini, na ghafla utajikuta umejaa mapenzi na huo ndio Ucha Mungu, na huyo ndio Mja Mwema, na hayo ndio matibabu ya Roho ambayo ukiyapata utakua na furaha mpaka siku yako ya kuondoka kwenye Ulimwengu huu.
Tunamuomba Mollah wetu atujaalie tuyapate mapenzi na Furaha zitokazo kwake na zidumu kwenye Roho zetu.
No comments:
Post a Comment