Asalaam Aleiykum
Sala nzima inageuka (Break Dance) utaona Mtu anahangaika lazima vidole vyako na vyake vigusane, akikukosa vidole analifata goti, akikosa goti anayumba kwenye Bega lazima akuguse, nyote wawili mnakua hamna sala ila mnakazi ya kukimbiana na "Ibilis" kakaa nyuma hana haja hata ya kupita anakuchekeni kwa mambo ya kipuuzi.
Sasa nini umeamrishwa ufanye ukiingia ndani ya hiyo Sala(Kumbuka mwanzo imetajwa uhifadhi) Na sasa aya iliyomo kwenye sura ya (Muuminoon aya 2)inasema
"ٱلَّذِينَ هُمۡ فِى صَلَاتِہِمۡ خَـٰشِعُونَ"
Ambao katika Sala zao huwa ni wanyenyekevu.
Unyenyekevu ulotajwa hapo ni ule wa mazingira ya sala yako, inatakiwa katika muda wote wakati umo katika hiyo Sala matendo yako yote yadumu ndani katika hiyo Sala, Bila ya kuwachia wazo lolote kuingia na kukutoa katika hali hiyo ya Sala yako, Ukiwa kwenye Kisimamo, kwenye Rukuu au Sijda uwe unamkumbuka Mollah wako kwa Tasbih zote.
Kwanini ujizoeshe hali hiyo kwa sababu ukichunguza utaona kila kitu kinakuja wakati wa kuanza sala,kwa sababu wakati ule unapata utulivu,na huo ndio wenye kutakiwa ukikurubia kwa Mollah wako, sasa cha kufanya kwanza ni kuizoesha hiyo (mind) au Akili izoee hali ya kumsabahi Mollah wako, usivunjike moyo mwanzoni itashindikana, huwezi kuishinda akili mara moja, na wala usibishane nayo kwa sababu ukifanya hivyo kushindana na Akili ndio utakaribisha magazeti kwenye Sala yako, vyama vya siasa vitakuja hapo, lakini ukifanya kwa taratibu zake za kuizoesha Akili Tasbih za kumkumbuka na kumtaja Mollah wako utaanza kuona kichwani hakuji tena mambo machafu, hukumbuki biashara wala madeni, hapo tena utakuwa tayari kuleta unyenyekevu na utulivu ndani ya Sala yako, Utaona Mwenyewe Kisimamo chako kimeanza kuwa kirefu, Rukuu zako na Sijda zako zinakua ndefu zenye utulivu, Na ukiipata hali hiyo ndio unakua ushaanza kwenda (Deep) na ukenda (Deep) kuna mambo mengi yanatokezea ndani ya hiyo Sala.
Kumbuka Sala ni Maombi, siku utakayoipata sala yako vema utanyamaza kimya, Na siku hiyo ndio utaacha kupeleka maombi yako ya Biashara, sijui ushinde kesi, mwanao apate visa, afanye uzuri mtihani wake, kazini upande cheo,Jirani aharibikiwe, vyote hivyo vitasimama kwa sababu siku hiyo utanyamaza kimya kwa kuwa umegundua kile ambacho Akili (Mind)yako ikiongea, hicho kitu kinanyamaza, Wewe ukinyamaza hicho kitu kinaongea, kuanzia hapo kila ukiingia kwenye sala na kutoka utakua ukisema "kile nilokipoteza miaka yote nimekiona ndani ya Sala", sasa sitaki maasi, sasa sitaki machafu ila nasadikisha Mollah wangu pekee ndie anostahiki kuabudiwa, na kuanzia hapo utaanza kuhifadhi kila kipindi cha Sala zako.
No comments:
Post a Comment