Asalaam Aleiykum
Najua unataka niseme kwa ufupi useme nishafahamu, vipi utafahamu hatujayapita hayo mafungu matatu ya (Awareness)Fahamu tukajua inakuaje, lazima tujiulize jee tuna uwezo wa kupita kwenye hizo daraja tatu?, Jawabu ndio uwezo upo tena kwa uchaguzi wako mwenyewe, hapa itabidi uwe makini katika kusoma kwako usije ukakosa kugundua siri iliyomo kwenye darsa hii, usije ukakikosa hicho chenye kukufanya uishi (Maisha bila ya Dhanmbi)iwapo utanifahamu.
Naam naanza kukileta kitu hicho kidogo kidogo kwa kukuuliza kwani wewe hujawahi "Kuamka usingizini ghafla kwa sekunde chache ukawa hujijui wewe nani na uko wapi"ikawa unaanza kuogopa, halafu fahamu zinakujia unafurahi, basi hapo kuna kitu unatakiwa ukigundue, unatakiwa ujiulize huyo anayejua na kuona"sijui niko wapi"na"Mbona sifikiri chochote"huyo ni nani?.
Ukigundua huyo ni nani basi hizo ndio (Level)za (Awareness)nilizozitaja hapo mwanzoni hiyo inojua na kuona na kujiuliza mwanzo, hiyo ndio wewe(Pure Being)na hiyo ndio aloitaja Mollah wako kwenye sura ya (Qiyama aya ya 14 na 15)
"بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ۬ "
"Bali Mwanaadamu ni shahidi juu ya nafsi yake".
Huo ushahidi ndio msingi wa darsa yetu na huo ndio hiyo (Awareness)Fahamu ambayo kwa ujanja wako unailetea aya inofata.
"وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُ ۥ "
"Ingawa unatoa dharura"
Ikiwa umenifatilia kwa makini utaziona hapo zimetajwa hizo awamu za fahamu nilizozitaja mwanzoni, ya kwanza ni ile ya (Pure Being) na ya Pili ni ile ya (Awareness) na ya tatu ni hiyo ya dharura ya (Machenical Awareness)au ya kuleta nyudhuru katika kuitumia hiyo Fahamu yako.
Sasa tuendelee na uchambuzi wetu tujue vipi tutaishi bila ya Dhanmbi, kuna watu wana wasiwasi kuhusu kutizamwa na Malaika wawili katika shughuli za maisha yao, wengine wanalipinga hilo la Malaika wawili kuandika matendo yako, Mimi leo nawaambia wewe mwenyewe unaweza kujiangalia kila kitu na kuishi bila ya dhanmbi, sasa tatizo liko wapi?, tatizo limetokea tokea wakati ule tulipooneshwa sehemu zetu za (Siri)na hapo imetumika (Symbol)sura ya (Aaraf aya ya 27)
يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّڪُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡہُمَا لِبَاسَہُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٲتِہِمَآۗ
"Enyi wanaadamu Shetani asikutieni katika matata(Fitina), kama alivowatoa wazee wenu katika pepo, akawavua nguo zao ili kuwaonyesha tupu zao,(Mpaka mwisho wa aya)"
Kuna mambo ya kuzingatiwa hapo usije ukadhani hee kuvua nguo tu ndio kumenifanya nifukuzwe peponi? Sasa nguo zipi hizo walizovuliwa?, wacha tutembee kwenye bustani tuchume faida mbili tatu ili ukiondoka hapa upate kujua mambo mapya ya kuyafanyia kazi.
Mwenye enzi Mungu kataja kwenye aya ya nyuma yake aya ya (26)kwa kusema "Enyi wanaadamu hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu, na nguo za pambo, na nguo za Ucha (Mungu)Utawa ndio bora, hayo ni katika ishara za Mwenye enzi Mungu ili wapate kukumbuka".
Hapo ndio makusudio ya hilo guo la Ucha Mungu(Innocence)ukivuliwa guo hilo ndio unapoanza kutenda makosa yote, kwa sababu ukiangalia mambo yote yanatokana na huko kuonekana kwa (tupu) au tuite (sex) kila kitu kina mahusiano na hilo, magonvi yote, utafutaji wa Mali mbio zote zinaongozwa na jambo hilo, ndio maana ukaambiwa kitu cha mwanzo kikatajwa hicho, na ukenda (Deep) utagundua ni hiyo fahamu ambayo (Ukibaleghe)au ukifikia(Puberty) tu fahamu zako zinakua nyengine kabisa, na hilo ndilo linotupelekea kuonyeshwa (Tupu)zao, na kumbuka ukioneshwa (Tupu yako)kwa kujua (Raha za Ufanyaji kazi yake)Maono hayo yanakua ni ya nje kwa hiyo kuanzia hapo ulipo(Baleghe) hukutizama tena ndani, kila mmoja wetu anatizama
nje, na hatizami Mtu mwenyewe ila anatumia Kioo, na hicho Kioo ni hao Watu(Mfano)Imam anauliza watu nimesalisha vizuri, Sheikh anauliza wasikilizaji mawaidha yangu mazuri, watu wananipenda, Jitizame wewe Mwenyewe unavotegemea watu wakusifu, shuruti wakwambie fulani mtu mzuri, lakini ukisikia wamesema Mtu mbaya hapo hapo unaingiwa na maradhi, kwanini wamesema hivyo, Kioo Kiminicheza?, tuyatizame maisha yetu yote ili tupate kujijua sisi ni nani, lakini Mwanaadamu anaogopa kuifata aya akajitizama nafsi yake kwa sababu anajua akianza kujiangalia atakosa uhondo, bora alale aendelee kuishi na Dhanmbi, wakati njia ya kuishi bila ya dhanmbi ipo? sasa ufanye nini?
Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment