Sunday, September 20, 2015

JUU MIUJIZA CHINI MIUJIZA PART 3

Asalaam Aleiykum


يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ۬ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَـٰكُمۡ شُعُوبً۬ا وَقَبَآٮِٕلَ لِتَعَارَفُوٓاْ‌ۚ إِنَّ أَڪۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَٮٰكُمۡ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ۬

"Enyi Wanaadamu kwa hakika tumekuumbeni (Nyote)kwa (Yule)Mwanaume (Mmoja) (Adam)na Yule Mwanamke (Mmoja)(Hawa)Na tumekufanyeni Mataifa na Makabila (Mbali mbali) ili Mjuane, Hakika mbora wenu Mbele ya Mwenye enzi Mungu ni yule amchaye(Ampendaye)Mollah  zaidi katika nyinyi, kwa yakini Mwenye enzi Mungu ni Mjuzi na Mwenye habari(za Mambo yote)"
Utaona katika aya hiyo hapo juu limeingia neno kujaaliwa siku zote nasema kujaaliwa ni(Temprary)kunaondoka, na kitendo hicho ni cha muda, na vikiondoka vitendo hivyo wewe unabakia mweupe, ikiondoshwa Kabila na kufanana unarejea kwenye hiyo (Singularity) kama vile mtoto umzae Mombasa akalelewe Arusha anakuwa hana fahamu yoyote ya wazee wake wala kabila lake, kwa hiyo ndio ikasemwa hiyo (Jaala) ni ya kujuana na kutafautishana tu, ila mwenye cheo na utukufu miongoni mwenu ni yule atoacha majivuno ya Kabila na kujuana juana akarejea kwenye hiyo Nafsi moja kwa ajili ya mapenzi ya Mwenye enzi Mungu.
Na hili la mapenzi ya utiifu kwa Mollah wetu ndilo lenye kutukutanisha sote katika kisimamo cha Arafa, hapo ndipo penye ule usawa wa Tajiri na Masikini, Mgonjwa na Mwenye afya kila mmoja kabeba jumba lake la Ardhi(Nafsi)moja zimekusanyika mbele ya Ufalme wa Mwenye enzi Mungu na kutamka maneno haya.
"Labaika Allah Humma Labaika""Laa sharika laka Labaika"
Unaitikia umati wa Nafsi moja, lakini kuitikia huko lazima furaha yake iwe unajua ndani ya nafsi yako kujua na kuamini kuwa "Nimeitikia wito wako Mollah wangu nikijua Wewe huna Mshirika" Nimekubali na ninathibitisha kwa yakini sote tulosimama hapa ni nafsi moja "Inokushukuru Wewe na kuzisifu neema zako za huu uhai na kila ulichotukirimu hakika kimetokana na Ufalme wako usiokua na Mshirika".
Hapo ndipo penye kukusanywa Nafsi ilotakasika safi isiyo na madhanmbi na ile ilo chafu ilojaa Madhanmbi na kusafishwa kwa pamoja na uwezo wa Mwenye enzi Mungu hapo ndipo inapokutana Miujiza kutoka Juu ikakutana na Miujiza ya chini. Na kama ukiikosa nafasi hiyo ukawa umeshghulika na (Wassup) itakua umesimama lakini unakosa mambo mengi, lakini ikiwa utatulia hapo utaona mambo ya ajabu ambayo utashindwa kuhadithia, katika mkusanyiko huo kuna nguvu inayotawala ambayo haina mfano, cha kufanya hapo ni kuzidi kuongeza dua ili uipate miujiza ya juu na ya chini.

No comments:

Post a Comment