Sunday, September 6, 2015

MAISHA BILA YA DHANMBI PART 1

Asalaam Aleiykum

Nakuchukua katika Safari hii adhimu wanayo kwenda  watu kidogo sana na mara chache sana, Safari yenyewe ni hii ya kiumbe kuweza kufanikiwa kuishi bila ya Dhanmbi, Swali la kujiuliza jee inawezekana kuishi katika hali hiyo?, Na kama inawezekana waloweza walifanya vipi?, Na nini faida yake?.
Kuweza kuyajua hayo inabidi twende (Deep)kwenye Darsa yetu ya leo tupate kuyachambua mambo, kwa bahati nzuri mengine yatakua mepya kwako, lakini upya wake utakupa muangaza wa vipi kulishughulikia tendo hilo la kuishi bila ya Dhanmbi, Nisije nikasema hivyo Mtu akaona ni rahisi jambo hili, ni gumu sana lakini linawezekana kwa kujizoesha na kulifanyia mazoezi tendo hili la kuishi bila ya Dhanmbi.
Na Iwapo utafanikiwa kuyafata maelekezo kwa ukamilifu ukaipata hali hiyo ya kuishi bila ya dhanmbi basi unakua ni Kiumbe ulofuzu kwa vitendo na unapata dalili zitokazo Mbinguni kwa uhakika zinaonekana waziwazi. Mpaka ukifika Umri wa kuijua Dhanmbi basi unajua sambamba kwamba dhanmbi ni (Chaguo), kama hujachagua dhanmbi unabaki katika hali gani?, napenda unifahamu bila ya chaguo hakuna Dhanmbi, Na hiyo ndio (Nature)yako.
Sasa kama hujachagua Dhanmbi unabaki katika hali gani, kuna hali tatu za mpito kiumbe lazima uzipite, Hali ya kwanza ni ile ya (Choiceless Awareness), Na ya pili ni (Machenical Awareness) na ya tatu ni hiyo ya (Awareness), Labda niseme kwa maana ya Kiswahili kifupi ni (Fahamu).
Sasa Tafsiri yangu mimi neno hili maana yake ni (Kujua kwa Kuona), najua utasema huyo anaanza, bora nikupe mfano wa haraka ili tupate kufahamiana, "Kisa kimo ndani ya Quraan"Malaika walipoambiwa na Mollah wao niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnavijua, walikua wanaviona lakini hawavijui mpaka Nabii Adam a.s akwaambia hichi ni kitu fulani", Kwa hiyo unaweza kujua kuendesha gari lakini ukapofuka macho ukawa huwezi kuendesha tena na hapo inakua (Part of awareness) Fahamu imeondoshwa na huwezi kuendesha tena hiyo gari, Na huo ndio mfano wa mnyama mbuzi anafugwa anampa mkulima maziwa lakini hana fahamu kua kuna siku atachinjwa awe kiburudisho cha karamu. Tumo katika darsa ya (Kuishi bila ya Dhanmbi)nakupa mifano hii ili nikupe picha ya (Akili) uweze kujua vipi utaishi bila ya Dhanmbi.
Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment