Sunday, August 23, 2015

MARA UMEUSAHAU MARA UMEUKUMBUKA PART 3

Asalaam Aleiykum

Imesemwa katika aya ya 31 sisi ni vipenzi vyako hapa Duniani, na huko kulindwa kwa ndani unaondoshewa khofu kwenye Akili yako, Mtu akija na (Kinyamkela chake)Shetani au Uchawi,unakingwa bila hata ya Mwenyewe kujua, habari ya utakula nini kwako haikugusi kabisa, utalala wapi vyote hivyo unaondoshewa, unakua huna khofu, hata Mauti unayakubali,unatambua wakati wangu ushafika wakurudi nyumbani.
Halafu tena unaondoshewa na hiyo huzuni, nayo ni hayo Maradhi kwenye mwili wako, kwani viwili hivi vikikukamata Mwili unaumwa, unahuzunika na huku khofu inakuingia unajiuliza ndio nakufa, kwa hiyo utaona ikatajwa kwenye aya ya 30(Unabashiriwa na Malaika wakati wa kutoka Roho usikhofu wala kuhuzunika) wewe huwaoni lakini unakhisi, vipi hisia zenyewe unazipata(Wakati inapoondoka khofu na huzuni, kinachobaki ni) (Bliss), lakini lazima upate huo msimamo wa kukumbuka daima.
Basi wacha nifunge darsa hii kwa kukupa dawa ambayo huwenda ikakusaidia kuupata huo msimamo wa kukumbuka moja kwa moja bila ya kusahau, Nini kinachotakiwa?, dawa ya kwanza kabisa ni ile ya kukumbuka, utafanya vipi? utakunya kwa siku mara moja, chukua jina la Mwenye enzi Mungu na maana yake(Kama hujui niulize)na utalitamka moyoni mwako kuanzia Sala ya alfajiri mpaka kuingia sala ya alfajiri nyengine, utayasoma majina yote 99 ya Mollah wako bila ya kukosa hata siku moja, itakuchukua miezi mitatu na siku 9, na ukiona bado hujapata huo msimamo wa kukumbuka ina maana bado unaendelea(Mara Umeusahau Mara Umeukumbuka) basi anza tena hiyo dawa na inshaallah kuna siku hutosahau tena na utakua ushafuzu, utajua Mwenyewe nini nimekusudia, utaangua kicheko kujiona umo katika hali ya kukumbuka daima, na hapo huna haja ya kutangaza na kila ukikaa utaangua kicheko cha furaha kwa kujiona hutendi dhanmbi na hapo utaigundua maana ya (Bliss) na ile tafsiri ya "Wale Walosema Hakika Mollah wetu ndie mlezi wetu", utakua unaishi Ulimwengu mwengine kabisa ambao kila Mja mwema anatarijiwa kuishi katika hali hiyo yenye furaha na afya, neema na baraka. Mollah atujaalie sote katika hilo.

No comments:

Post a Comment