Sunday, September 20, 2015

JUU MIUJIZA CHINI MIUJIZA PART 1

Asalaam Aleiykum

Napenda kuwapa taarifa wale wenye kufatilia darsa zangu kutokana na shughuli za Kifamilia, Kijamii na Kikazi huenda mkashuhudia upungufu wa Darsa zangu, hilo limetokana na ongezeko la shughuli za uwajibikaji wangu katika hayo mambo matatu niloyataja, na asije akadhania mtu hii ndio darsa yangu ya mwisho au akaona Bahari imekauka Inshaallah penye Uhai tutaendelea kupeana yale ambayo Mollah wangu ananipa mimi nijifunze kwa ushirika na nyinyi.
Naam ikiwa wiki hii tunashuhudia kilele cha Ibada ya Hajj wacha na sisi wenye kutamani tulizungumze tukio hili kwa undani wa hali ya juu kabisa na upeo mwengine tafauti na ule ulozoea, Kwanini nikasema hivyo, kwa sababu mimi ntakufahamisha tukio moja tu ambalo litabadilisha muono wako na uangalizi wa mambo ya Ibada hii kwa Jumla, Na kama utakua utagundua mapya yakaingia katika fahamu yako, basi ijue hiyo ndio Darsa. Sasa nini maana ya neno hili Darsa?, Neno hili limetokana kwenye Lugha ya Kihindi kumaanisha Mkusanyiko wa kuwa karibu na Mwenye enzi Mungu.
Kama utaniuliza mimi nini Hajj ntakwambia Hajj ni ile siku ya Mkusanyiko wa Arafa, ukikosa Arafa  huna Hijja, lazima ukahijji tena. Sasa kwanini Ikawa Arafa hii ndio inatuchukua kwenye Darsa yetu ya leo ya (Juu Miujiza chini Miujiza). Pata faida hii na wewe ukoge kwenye Bahari ya Miujiza ili ubadilike uwe Mtu wa aina nyengine kabisa, yajue mambo ili na wewe ukenda (Makka) ujue kumbe (Juu Miujiza chini Miujiza)Na kama ilivo desturi yangu naazima aya mbili kuizungumzia hiyo Miujiza ya Arafa.
Najua itakua tafauti na zile ulizozoea kuzisikia  zikiizungumza Ibada hii ya Hajj, lakini ni lazima wengine tupite njia tafauti ili nipate kufika kwenye ufalme wa fahamu yako.Na hii itakufanya kila ukiisikia aya hii itakukumbusha mengi kama inavofanya kwangu mimi inazidi kunipeleka (Deep)na mwisho wake siujui, basi ikiwa unataka kuungana na mimi endelea part 2

JUU MIUJIZA CHINI MIUJIZA PART 2

Asalaam Aleiykum


يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٍ۬ وَٲحِدَةٍ۬ وَخَلَقَ مِنۡہَا زَوۡجَهَا وَبَثَّ مِنۡہُمَا رِجَالاً۬ كَثِيرً۬ا وَنِسَآءً۬‌ۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِى تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلۡأَرۡحَامَ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيۡكُمۡ رَقِيبً۬
"Enyi Wanaadamu Mcheni Mollah wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi moja, Na akamuumba Mkewe katika nafsi ile ile, Na akaeneza Wanaume wengi na Wanawake kutoka katika wawili hao, Na Mcheni Mwenye enzi Mungu ambaye kwake mnamuomba(na kuwafanyia)haki jamaa, na kile (Kilichokuhifadhi)hakika Mwenye enzi Mungu ni Mlinzi juu yenu."
Yameshuka Maneno ya Miujiza katika aya hii lakini inatakiwa Mwanaadamu ende (Deep) kuyatizama na kuyagundua kiini na chanzo cha maneno haya ili apate ufumbuzi, kwa njia ya kawaida kama Akili imekutulia unaona kila siku uchambuzi wa aya hiyo kwa juu juu, unaona wewe sote tulivo fanana kuanzia Pua, masikio, Macho, mikono, miguu, vidole na takriban kila kitu mimi na Mwengine yoyote hatuna tafauti, awe Mtu Mfalme au Rais awe na ukubwa wowote tumefanana kuanzia ndani mpaka nje hatuna tafauti, na hicho ndio hicho cha kutizamwa mwanzo ili upate uhakika wa mwanzo.
Hiyo ndio Ardhi aliyoumbiwa kila mmoja wetu na hilo ndilo la miujiza wa chini. Kuna jengine ambalo hili hulifahamu mpaka uende (Deep) kwenye ufalme wako wa Fahamu huko ndiko utakapo kutana na hilo la Muujiza wa Juu na hapo ndipo utakapo tambua hiyo maana ya (Nafsi moja) kwani Katika Ufalme huo ndiko iliko hiyo (Singularity)huko ndiko unakutana na ukweli ya kwamba kilichomo katika nafsi yangu na kwako ndio hicho hicho hatuna tafauti, kama tulivofanana nje na ndani tumefanana(Kutokana na yeye Adam tukamuumbia Hawa) tafauti yetu ni katika (Level) ni ya Nje, huyu Mwanamke yule Mwanamme lakini sote ni sawa kama ilivyo (Ardhi) mipaka iko Juu lakini chini (Ardhi) ni Moja, Bahari ikikauka tunakwenda kote kwa miguu, basi baada ya aya hiyo ndio ikafatia hii ya pili sura ya (Al hujraat 13)



يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ۬ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَـٰكُمۡ شُعُوبً۬ا وَقَبَآٮِٕلَ لِتَعَارَفُوٓاْ‌ۚ إِنَّ أَڪۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَٮٰكُمۡ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ۬ 


JUU MIUJIZA CHINI MIUJIZA PART 3

Asalaam Aleiykum


يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ۬ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَـٰكُمۡ شُعُوبً۬ا وَقَبَآٮِٕلَ لِتَعَارَفُوٓاْ‌ۚ إِنَّ أَڪۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَٮٰكُمۡ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ۬

"Enyi Wanaadamu kwa hakika tumekuumbeni (Nyote)kwa (Yule)Mwanaume (Mmoja) (Adam)na Yule Mwanamke (Mmoja)(Hawa)Na tumekufanyeni Mataifa na Makabila (Mbali mbali) ili Mjuane, Hakika mbora wenu Mbele ya Mwenye enzi Mungu ni yule amchaye(Ampendaye)Mollah  zaidi katika nyinyi, kwa yakini Mwenye enzi Mungu ni Mjuzi na Mwenye habari(za Mambo yote)"
Utaona katika aya hiyo hapo juu limeingia neno kujaaliwa siku zote nasema kujaaliwa ni(Temprary)kunaondoka, na kitendo hicho ni cha muda, na vikiondoka vitendo hivyo wewe unabakia mweupe, ikiondoshwa Kabila na kufanana unarejea kwenye hiyo (Singularity) kama vile mtoto umzae Mombasa akalelewe Arusha anakuwa hana fahamu yoyote ya wazee wake wala kabila lake, kwa hiyo ndio ikasemwa hiyo (Jaala) ni ya kujuana na kutafautishana tu, ila mwenye cheo na utukufu miongoni mwenu ni yule atoacha majivuno ya Kabila na kujuana juana akarejea kwenye hiyo Nafsi moja kwa ajili ya mapenzi ya Mwenye enzi Mungu.
Na hili la mapenzi ya utiifu kwa Mollah wetu ndilo lenye kutukutanisha sote katika kisimamo cha Arafa, hapo ndipo penye ule usawa wa Tajiri na Masikini, Mgonjwa na Mwenye afya kila mmoja kabeba jumba lake la Ardhi(Nafsi)moja zimekusanyika mbele ya Ufalme wa Mwenye enzi Mungu na kutamka maneno haya.
"Labaika Allah Humma Labaika""Laa sharika laka Labaika"
Unaitikia umati wa Nafsi moja, lakini kuitikia huko lazima furaha yake iwe unajua ndani ya nafsi yako kujua na kuamini kuwa "Nimeitikia wito wako Mollah wangu nikijua Wewe huna Mshirika" Nimekubali na ninathibitisha kwa yakini sote tulosimama hapa ni nafsi moja "Inokushukuru Wewe na kuzisifu neema zako za huu uhai na kila ulichotukirimu hakika kimetokana na Ufalme wako usiokua na Mshirika".
Hapo ndipo penye kukusanywa Nafsi ilotakasika safi isiyo na madhanmbi na ile ilo chafu ilojaa Madhanmbi na kusafishwa kwa pamoja na uwezo wa Mwenye enzi Mungu hapo ndipo inapokutana Miujiza kutoka Juu ikakutana na Miujiza ya chini. Na kama ukiikosa nafasi hiyo ukawa umeshghulika na (Wassup) itakua umesimama lakini unakosa mambo mengi, lakini ikiwa utatulia hapo utaona mambo ya ajabu ambayo utashindwa kuhadithia, katika mkusanyiko huo kuna nguvu inayotawala ambayo haina mfano, cha kufanya hapo ni kuzidi kuongeza dua ili uipate miujiza ya juu na ya chini.

Sunday, September 6, 2015

MAISHA BILA YA DHANMBI PART 1

Asalaam Aleiykum

Nakuchukua katika Safari hii adhimu wanayo kwenda  watu kidogo sana na mara chache sana, Safari yenyewe ni hii ya kiumbe kuweza kufanikiwa kuishi bila ya Dhanmbi, Swali la kujiuliza jee inawezekana kuishi katika hali hiyo?, Na kama inawezekana waloweza walifanya vipi?, Na nini faida yake?.
Kuweza kuyajua hayo inabidi twende (Deep)kwenye Darsa yetu ya leo tupate kuyachambua mambo, kwa bahati nzuri mengine yatakua mepya kwako, lakini upya wake utakupa muangaza wa vipi kulishughulikia tendo hilo la kuishi bila ya Dhanmbi, Nisije nikasema hivyo Mtu akaona ni rahisi jambo hili, ni gumu sana lakini linawezekana kwa kujizoesha na kulifanyia mazoezi tendo hili la kuishi bila ya Dhanmbi.
Na Iwapo utafanikiwa kuyafata maelekezo kwa ukamilifu ukaipata hali hiyo ya kuishi bila ya dhanmbi basi unakua ni Kiumbe ulofuzu kwa vitendo na unapata dalili zitokazo Mbinguni kwa uhakika zinaonekana waziwazi. Mpaka ukifika Umri wa kuijua Dhanmbi basi unajua sambamba kwamba dhanmbi ni (Chaguo), kama hujachagua dhanmbi unabaki katika hali gani?, napenda unifahamu bila ya chaguo hakuna Dhanmbi, Na hiyo ndio (Nature)yako.
Sasa kama hujachagua Dhanmbi unabaki katika hali gani, kuna hali tatu za mpito kiumbe lazima uzipite, Hali ya kwanza ni ile ya (Choiceless Awareness), Na ya pili ni (Machenical Awareness) na ya tatu ni hiyo ya (Awareness), Labda niseme kwa maana ya Kiswahili kifupi ni (Fahamu).
Sasa Tafsiri yangu mimi neno hili maana yake ni (Kujua kwa Kuona), najua utasema huyo anaanza, bora nikupe mfano wa haraka ili tupate kufahamiana, "Kisa kimo ndani ya Quraan"Malaika walipoambiwa na Mollah wao niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnavijua, walikua wanaviona lakini hawavijui mpaka Nabii Adam a.s akwaambia hichi ni kitu fulani", Kwa hiyo unaweza kujua kuendesha gari lakini ukapofuka macho ukawa huwezi kuendesha tena na hapo inakua (Part of awareness) Fahamu imeondoshwa na huwezi kuendesha tena hiyo gari, Na huo ndio mfano wa mnyama mbuzi anafugwa anampa mkulima maziwa lakini hana fahamu kua kuna siku atachinjwa awe kiburudisho cha karamu. Tumo katika darsa ya (Kuishi bila ya Dhanmbi)nakupa mifano hii ili nikupe picha ya (Akili) uweze kujua vipi utaishi bila ya Dhanmbi.
Endelea Part 2

MAISHA BILA YA DHANMBI PART 2

Asalaam Aleiykum

Najua unataka niseme kwa ufupi useme nishafahamu, vipi utafahamu hatujayapita hayo mafungu matatu ya (Awareness)Fahamu tukajua inakuaje, lazima tujiulize jee tuna uwezo wa kupita kwenye hizo daraja tatu?, Jawabu ndio uwezo upo tena kwa uchaguzi wako mwenyewe, hapa itabidi uwe makini katika kusoma kwako usije ukakosa kugundua siri iliyomo kwenye darsa hii, usije ukakikosa hicho chenye kukufanya uishi (Maisha bila ya Dhanmbi)iwapo utanifahamu.
Naam naanza kukileta kitu hicho kidogo kidogo kwa kukuuliza kwani wewe hujawahi "Kuamka usingizini ghafla kwa sekunde chache ukawa hujijui wewe nani na uko wapi"ikawa unaanza kuogopa, halafu fahamu zinakujia unafurahi, basi hapo kuna kitu unatakiwa ukigundue, unatakiwa ujiulize huyo anayejua na kuona"sijui niko wapi"na"Mbona sifikiri chochote"huyo ni nani?.
Ukigundua huyo ni nani basi hizo ndio (Level)za (Awareness)nilizozitaja hapo mwanzoni hiyo inojua na kuona na kujiuliza mwanzo, hiyo ndio wewe(Pure Being)na hiyo ndio aloitaja Mollah wako  kwenye sura ya (Qiyama aya ya 14 na 15)
"بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ۬ "
"Bali Mwanaadamu ni shahidi juu ya nafsi yake".
Huo ushahidi ndio msingi wa darsa yetu na huo ndio hiyo (Awareness)Fahamu ambayo kwa ujanja wako unailetea aya inofata.
"وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُ ۥ "
"Ingawa unatoa dharura"
Ikiwa umenifatilia kwa makini utaziona hapo zimetajwa hizo awamu za fahamu nilizozitaja mwanzoni, ya kwanza ni ile ya (Pure Being) na ya Pili ni ile ya (Awareness) na ya tatu ni hiyo ya dharura ya (Machenical Awareness)au ya kuleta nyudhuru katika kuitumia hiyo Fahamu yako.
Sasa tuendelee na uchambuzi wetu tujue vipi tutaishi bila ya Dhanmbi, kuna watu wana wasiwasi kuhusu kutizamwa na Malaika wawili katika shughuli za maisha yao, wengine wanalipinga hilo la Malaika wawili kuandika matendo yako, Mimi leo nawaambia wewe mwenyewe unaweza kujiangalia kila kitu na kuishi bila ya dhanmbi, sasa tatizo liko wapi?, tatizo limetokea tokea wakati ule tulipooneshwa sehemu zetu za (Siri)na hapo imetumika (Symbol)sura ya (Aaraf aya ya 27)
يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّڪُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡہُمَا لِبَاسَہُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٲتِہِمَآ‌ۗ 
"Enyi wanaadamu Shetani asikutieni katika matata(Fitina), kama alivowatoa wazee wenu katika pepo, akawavua nguo zao ili kuwaonyesha tupu zao,(Mpaka mwisho wa aya)"
Kuna mambo ya kuzingatiwa hapo usije ukadhani hee kuvua nguo tu ndio kumenifanya nifukuzwe peponi? Sasa nguo zipi hizo walizovuliwa?, wacha tutembee kwenye bustani tuchume faida mbili tatu ili ukiondoka hapa upate kujua mambo mapya ya kuyafanyia kazi.
Mwenye enzi Mungu kataja kwenye aya ya nyuma yake aya ya (26)kwa kusema "Enyi wanaadamu hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu, na nguo za pambo, na nguo za Ucha (Mungu)Utawa ndio bora, hayo ni katika ishara za Mwenye enzi Mungu ili wapate kukumbuka".
Hapo ndio makusudio ya hilo guo la Ucha Mungu(Innocence)ukivuliwa guo hilo ndio unapoanza kutenda makosa yote, kwa sababu ukiangalia mambo yote yanatokana na huko kuonekana kwa (tupu) au tuite (sex) kila kitu kina mahusiano na hilo, magonvi yote, utafutaji wa Mali mbio zote zinaongozwa na jambo hilo, ndio maana ukaambiwa kitu cha mwanzo kikatajwa hicho, na ukenda (Deep) utagundua ni hiyo fahamu ambayo (Ukibaleghe)au ukifikia(Puberty) tu fahamu zako zinakua nyengine kabisa, na hilo ndilo linotupelekea kuonyeshwa (Tupu)zao, na kumbuka ukioneshwa (Tupu yako)kwa kujua (Raha za Ufanyaji kazi yake)Maono hayo yanakua ni ya nje kwa hiyo kuanzia hapo ulipo(Baleghe) hukutizama tena ndani, kila mmoja wetu anatizama 
nje, na hatizami Mtu mwenyewe ila anatumia Kioo, na hicho Kioo ni hao Watu(Mfano)Imam anauliza watu nimesalisha vizuri, Sheikh anauliza wasikilizaji mawaidha yangu mazuri, watu wananipenda, Jitizame wewe Mwenyewe unavotegemea watu wakusifu, shuruti wakwambie fulani mtu mzuri, lakini ukisikia wamesema Mtu mbaya hapo hapo unaingiwa na maradhi, kwanini wamesema hivyo, Kioo Kiminicheza?, tuyatizame maisha yetu yote ili tupate kujijua sisi ni nani, lakini Mwanaadamu anaogopa kuifata aya akajitizama nafsi yake kwa sababu anajua akianza kujiangalia atakosa uhondo, bora alale aendelee kuishi na Dhanmbi, wakati njia ya kuishi bila ya dhanmbi ipo? sasa ufanye nini?
Endelea Part 3

MAISHA BILA YA DHANMBI PART 3

Asalaam Aleiykum

Sasa litizame Neno kuoneshwa (Tupu zao)hiyo ni (Symbol), Tulikua hatujui tukapewa (Fahamu)au(Knowledge)lakini cha muhimu kwa mara ya mwanzo tuliweza kujitizama (Nafsi)zetu, na tokea hapo sio Watu wengi walo rudi nyuma kujitizama tena nafsi yake, Imeingia tafaruku ya kuzitafuta Raha za Dunia Mtu yuko tayari kuchupa Motoni lakini asikose Raha za muda mfupi.
Kitu cha kukiangalia hapa ni lile tukio, lakini naomba tulitizame (Kisomi)sio(Kivitendo)kutokana na kuoneshwa huko inatulazimu tuelewe kwamba(Fahamu)zetu zina uwezo wa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, Tuna uwezo wa kuona nje na kuona ndani kwa wakati mmoja, Unaweza kukitizama kitu nje na ukajiona wewe Mwenye kutizama, hiyo naita mimi (Double take)zinoangalia nje ni Fahamu na zinoangalia ndani ni Fahamu.
Sasa ukiweza kuangalia vyote viwili kwa wakati mmoja hiyo ndio (Awareness)na hiyo ndio itakufanya (Uishi bila ya Dhanmbi), Sasa ufanye vipi kuipata hali hiyo?, kwa sababu mpaka umri ulofikia mafundisho mengi yameshaingia katika kichwa chako huna haja tena yakuleta nyudhuru tena, kila kitu kimo ndani ya (Mind)yako, kwa hiyo Sasa inabidi uanze kufuta yale yote yaloandikwa kichwani mwako, vipi utafuta?, kwanza lazima uelewe (Mind) yako ina mtindo wa kurejea mambo, sababu ni kama (computer)haina jambo jipya, kwa hiyo ukijichunguza utajikuta hata hizo dhanmbi zako sio mpya ila za kurejea rejea.
Sasa kuanzia leo Dhanmbi zako wewe unazijua, kama atakujia Mwanamke au Mwanamme katika jambo la la Matamanio, basi usimtizame huyo alokujia pekee jitizame na wewe nini kinatokezea ndani yako, kumbuka kila kwenye (Action) lazima iwepo(Re-Action) Na vyote viwili wewe unavishuhudia, na hiyo ndio maana ya kila "Mwanaadamu anaiona Nafsi yake".
Basi ukishalijua hilo sasa ukitaka kupokea Rushwa mtizame mtoaji jitizame na wewe ni kimaanisha tizama (Mind)yako nini kinatokea?, Ukisema Uongo pia wakati unausema itizame nafsi yako inavodanganya, hata ukiwa unalewa umekamata chupa basi jiangalie mvinyo unavokwenda ndani, ukipata hamaki tizama nini kinatokea ndani yako, ikiwa unakwiba umebobea kwenye wizi basi wakati unakwiba tizama ndani huyu nani anofanya wizi huu, na pia ukiwa unazini au kufanya maasi yoyote yale usisahau kujikumbuka na wewe mfanyaji, kuna wakati ukijikumbuka kuwa wewe ndio mfanyaji ghafla utasita na hutotenda tena hilo tukio na hapo ndio Akili inapotea.
Najua nikisema (Akili) inapotea kuna watu watashtuka, Naam lazima ushituke, Akili kupotea ni mambo makubwa inabidi nikufahamishe vizuri usije kikakupata kisa kama kilichonipata mimi huko kwetu Tanzania.(Ngoja nikupe mkasa huo japo kidogo)nilikua mapumzikoni nyumbani nikawa nimekaa na vijana kwenye baraza"Akapita kijana nikaambiwa mzee unamuona huyu kijana kapoteza saa"mimi nikamuonea huruma nikasema twendeni tukamsaidie nikawa wa mwanzo kunyanyuka"wale vijana nilokaa nao wakaona maskini sasa tumepata wagonjwa wawili"hiyo ni kwa sababu mimi sikuelewa kupoteza saa kumbe ni maradhi ya Akili", basi wacha nifafanue vizuri tusije sote tukapoteza maana.
Huku kupotea kwa Akili kuko kwa aina mbili, Aina ya kwanza Akili inakwenda Ardhini na kukaa kwenye(Body), ndio utasikia kazama ama ana wazimu wa kutafuta mali, au ana wazimu wa wanawake au wa wanaume, au utasikia pombe imemuharibu Akili, na mwisho utasikia kapata maradhi ya wazimu au akili imeshindwa kuchukua amerukwa na Akili, na Akili ikiruka ndio Mja haponi tena, kwani inakua Akili ishapotea lakini sio kwa hiyari .
Aina ya pili nakuomba uifahamu kwa uangalifu Akili ipo lakini unaipotea, au unakwenda (Beyond)unakua tafauti na Akili yako, au unakua (Master) na hiyo ndio tafauti yake, na huyu Mwenye kui(Master)ina maana akili yake imekwenda(Mbinguni)juu, na huko ndio (Kumcha Mungu)Na huyo ndie Mwenye kuangalia Nafsi yake ambaye anaishi bila ya (Dhanmbi), kila kitu anakiona (clear)mnapata mifano midogo midogo, kwani wewe kuna mambo mangapi umeyawacha unajua kwanini?umekwenda (Beyond)lakini bila ya kujijua, unaacha ulevi, unaacha uzinifu (something happen)lakini hujijui, nifanyacho mimi sasa hivi ni kukumbusha tu, lakini isiwe umeacha mambo hayo kwa ajili ya maradhi au sababu zengine huwezi kufanya, kwani ukifanya hivyo bado utakuwepo Ardhini, bado huioni nafsi yako, bado unatufanyia ujanja ujanja,unaacha mbele za watu lakini  kwenye Akili yako kutwa unazini, unasema uongo,unalewa, unatakiwa uwache kwa kuipotea akili yako kwa kwenda (Mbinguni)(Beyond)Mcha Mungu ikimbie Akili hiyo mpaka watu wakikutizama wanajua siku hizi hachezi mchiriku, hatizami senema za mambo machafu, kaacha kusema uongo na mengi mengineyo. Vipi utafanya hilo ni kwa kuamua kwenda (Beyond). Ufanye vipi?
Kumbuka katika chochote chenye kutendeka kuna mambo matatu yanatokea, (Mfano)unataka kufanya Uzinifu, Mwanamke au Mwanamme kashakuja unataka kufanya kitendo, jambo la kwanza mtizame huyo "alokuja"(1)Halafu kuna Akili yako ilojaa Shauku(2), na Jambo la tatu(3) na hilo ndio muhimu ukiweza kulikumbuka hilo lenye kuona hayo mawili ya mwanzo hilo ndio wewe", Ukiweza kulikumbuka hilo bila ya kuleta dharura ya kulisahau au kulipuuza hapo ndio utafanikiwa kuigundua au kuifahamu maana ya kila "Mja ni Mwenye kuiona Nafsi yake", na hiyo ndio (Pure Being). Na hapo utaweza kuishi bila ya dhanmbi, na hicho ndicho chenye Mapenzi, Afya, Furaha na matumaini.
Hicho ndio kile kisichoguswa na Maradhi wala kero na hata dhiki, na hii ndio maana ya "Tafsiri ya hizo aya mbili""Bali Mwanaadamu ni Mwenye kuiona Nafsi yake""Japo analeta Nyudhuru".
Nakupa dawa uifanyie kazi, lakini kama utaendelea kununua (Kaseti)zikupe nyudhuru za mawaidha mazuri basi endelea, lakini hii ndio haki na huu ndio ukweli.