Asalaam Aleiykum
Nimepokea ombi watu wanataka wanione au kunisikia basi nawatoa wasiwasi huenda wakaniona au wasinione yote yanawezekana, nini haja ya kuniona sababu unataka kujiridhisha nikoje, kweli ndie mie ninoandika au kuna sehemu na (copy)na ku(Paste), wasiwasi umekushika unaona mafundisho ndiyo lakini huyu Mwenye kuandika anavaa vilemba, huyu kweli Sheikh? hali ya wasiwasi ndio inokufanya utake kunijua, basi kabla hujanijua wacha tuingie kwenye darsa hii ya (Athari za Macho na Sauti) ili uchume tunda la faida ambalo utakapo kula huwenda ukaonja ladha ya kufahamu kwa undani utendaji wa kazi wa viwili hivyo.
Utapata Muongozo wa kuepuka mambo ambayo ukiyashiriki huwenda yakakuangamiza, pata faida hii ili iwe silaha yako itakayokupa uwezo wa kujihifadhi Na pengine kuondoka hiyo hamu ya kunijua.
Kuna msemo maarufu sana unaosema (Every Saint has past and every sinner have a future)Naam maneno sahihi hayo (Kila Walii ana Skeleton wake, Makovu na alama zipo hilo halina shaka, Na wewe Mtenda dhanmbi vile vile unayo nafasi yakua kama huyo Walii) Kwa hiyo usitie wasiwasi kwa lolote ulolifanya kama unataka kutubia basi midamu uhai unao jirekebishe hivi sasa kwa kuzingatia haya nitakayokujulisha,Na hiyo ndio maana ya ile aya isemayo (Msikate Tamaa na Rehma za Mwenye enzi Mungu).
Nini kinachotakiwa kifanyike?, Unatakiwa ufanye marekebisho ya Tabia yako ambayo ndimo vinavoishi viwili hivi Kusikia na Kuona. Leo tunakutana na viwili hivyo ambavyo ndio chanzo cha matatizo yote yanokufanya uangamie, viwili hivyo ni (Macho na Sauti au Kuzungumza) Nimeamua kuvizungumza hivi kwa kuwa kuna Baadhi ya Watu wanakejeli ile hekima ya kuambiwa usitizame mambo mabaya, au usisikize mazungumzo mabaya au kutizama Wanawake au kuzungumza na Wanaume, kuna baadhi ya watu hilo wanalitilia shaka na kuona kuna ukandamizwaji wa aina fulani kwenye (Dini)Basi ikiwa wewe unajiandaa na ushafanya uamuzi wa kuepuka au kujinusuru na (Uzinzi na Uasherati) Mada hii inakufaa.
Endelea part 2
Sunday, November 15, 2015
ATHARI ZA MACHO NA SAUTI PART 2
Asalaam Aleiykum
Sasa Kutana na aya inayofundisha athari za Macho na Sababu zake,
(An-Noor aya ya 30)
قُل لِّلۡمُؤۡمِنِينَ يَغُضُّواْ مِنۡ أَبۡصَـٰرِهِمۡ وَيَحۡفَظُواْ فُرُوجَهُمۡۚ ذَٲلِكَ أَزۡكَىٰ لَهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ
"Waambie Waislam Wanaume wainamishe macho yao,(Wasiangalie mambo mabaya), Na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, bila shaka Mwenye enzi Mungu anazo habari za wanayoyafanya".
Wameambiwa pia na Wanawake kwenye aya inayofatia ambayo nishawahi kuizungumzia huko nyuma aya ya (31) leo tunaogelea kwenye hiyo aya ya (30)wacha tupate faida zake ili tukazifanyie kazi.
Hapo katika maelezo hayo kuna mazingatio makubwa hususan ukiwa weye kijana, "Kwanini uangushe macho yako na wala hukuambiwa yafunge ila limetumika neno angusha", Umeambiwa uangushe kwa sababu binafsi yako ndani wewe unachemka, Na huna (Control)uwezo ulopewa ni huo wa kuangusha macho, kwa sababu ukiangusha macho (Connection)inakatika hupati tena mawasiliano, Na kama hupati mawasiliano Akili inatulia na Akili ikitulia ndio unawasili upande wa pili kwenye huo Utakaso(Ucha)Mungu ita upendavyo ukiingia ndio utajua umo kwenye hali gani wakati akili imetulia, kwa mara ya mwanzo utajua vipi utamu wa (Control)ya maisha yako, sasa kabla ya kwenda (deep) wacha tuyazungumze macho na shughuli zake.
Macho ni sawa sawa na kushika au nieseme yana mahusiano ya karibu sana na kushika, Sasa nini tafauti yake? Tafauti yake unaposhika kwa njia ya nje inayoongezeka ni hisia, na huku kushika kwa ndani ambako ndio (Powerful)penye kutumika macho, huku wengi mnajua inakuaje pale unapomtizama Mwanamke au Mwanamme, na vituko vikaanza kutokea ndani ya nafsi yako, Na yule Mwenye kushikwa kwa njia ya kutizamwa vile vile anajua kuwa sasa Nakamatwa bila ya (Idhini yangu) ndio maana kwa yule asoridhia utaona mara matusi au maneno yanamtoka, Nini kimetokezea?.
Kilichotokezea hapo ni mabishano ya Roho wewe unataka kumshika kwa nguvu na yeye hataki, ndio maana utaona tunapeana muda wa kutizamana wa sekunde nne tu, zikizidi hapo kuna jambo linafatia, na kama bado unafanya ukaidi (Jiulize)inakuaje Mtu kapita tu mimi huku ndani navurugika Akili.
Endelea part 3

ATHARI ZA MACHO NA SAUTI PART 3
Asalaam Aleiykum
Baada ya hizo sekunde nne ndio maridhiano au ugonvi vinaanza kutokea, Na kama umeridhia macho yanaanza mazungumzo (Bubu)ya ishara, unaweza kuandika (Love Story)nzima ya mapenzi, inaweza kutoka Amri ya mtu auliwe kwa ajili ya macho, Ikapelekwa posa pahala kwa ajili ya jicho, Akaumwa mtu maradhi ya kutoka na roho kwa ajili ya jicho, ikaingia pahala hasada kwa ajili ya jicho, Kwanini ikawa jicho?.
Kwa sababu jicho ni (Dirisha la Roho) Na Roho ni (Very Powerful Being)ndio maana ukimuona mwanamme au mwanamke ndani unachemka(Energy)inaanza kunyanyuka, na ikinyanyuka inachukua muda kutulia na Akili kuvurugika, Na kutokana na hilo jicho hapo tena (Mind) inakamata kazi yake, na (Body)inajiweka tayari kwa kutayarisha silaha za mapambano, Hapo tena Akili ya (Mja)ikichafuka Mtu anaweza kufukuzwa kazi au kupandishwa cheo, hiyo ndio Athari ya Jicho na madhara yake, ndio maana unaambiwa liangushe likustiri, kwani kwenye kuliangusha Jicho kuna siri kubwa ndio maana aya ikamalizia na (Wahifadhi Tupu zao) Kwanini Uhifadhi tupu?.
Kwa sababu kwa kufanya hivyo unahifadhi kitu adhimu kabisa ndani ya huo Mwili wako(Body), "Wewe una Mali ghafi" kama utaitunza ndio unaupata huo utakaso (Pureness)Na kama utatumia hiyo mali ghafi yako ovyo ovyo basi utaangamia kwa kuzorota kwa afya yako, utakua huwezi kazi, zitakuvaa tafran tupu kichwani, kwa hiyo unaambiwa hifadhi hicho ulichonacho usipite ukakitupa ovyo kwa furaha ya sekunde nne, uonee huruma mwili wako kwa kuupunguzia kazi za (Overtime)kutengeneza mali ghafi(Material)kila baada ya masaa 24, Halafu tena unaambiwa jiepushe na mazungumzo, kwa sababu mazungumzo au (Sauti) ndio daraja la majaribio, hapo ndipo vinapoanza vimbunga vyote, Fitna zote zinaanzia hapo, Ndio maana utaona wanaadamu tumepewa jambo hili muhimu sana la kuzungumza, Mazungumzo ni mawasiliano, hapo ndipo unapoonesha chuki na mapenzi, kwa kutumia mazungumzo ndio unaonesha hamaki na hasira, kwa hiyo ndio maana ukaambiwa jiepushe hata na mazungumzo sio macho pekee na huyo mwanamke au mwanamme, ila ukiwa ushafikia daraja la kuweza kujimiliki(Control), vipi kujimiliki huko ni pale ukiijua maana ya "(Maneno matamu humtoa nyoka pangoni)" sasa maana hiyo utaijua vipi, kwanza lazima ufahamu nyoka hasikii vipi utamtoa pangoni, basi kujimiliki nikule kumrejesha nyoka pangoni akatulie, ukifikia daraja hiyo wewe utakua katika wale walotajwa kwenye aya ya 31 ambayo hawana dhara ima wakitizama au wakizungumza, Wana uwezo wa kumuweka Nyoka pangoni hata asitamani kutoka. Ukifikia daraja hiyo hapo tena unaweza kuzungumza unaweza kuangalia hakuna chenye kukushughulisha na wala Akili yako haisumbuliwi tena na matukio ya Nje, hiyo ndio maana ya kuambiwa jiepushe na Athari za macho na sauti.

Sunday, November 1, 2015
UFALME WA MUNGU PART 1
Asalaam Aleiykum
قُلِ ٱللَّهُمَّ مَـٰلِكَ ٱلۡمُلۡكِ تُؤۡتِى ٱلۡمُلۡكَ مَن تَشَآءُ وَتَنزِعُ ٱلۡمُلۡكَ مِمَّن تَشَآءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَآءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَآءُۖ بِيَدِكَ ٱلۡخَيۡرُۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬
Hiyo ni aya ya (26)iliyomo kwenye sura ya (Al-Imran) inatafsirika hivi:"Sema Ewe Mollah wangu uliyemiliki Ufalme wote, Humpa Ufalme umtakaye,na humuondolea(Ufalme)umtakaye, Na humtukuza umtakaye, Na humdhalilisha umtakaye,Kheri imo mikononi mwako, bila shaka Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu".
Aya imeanza kwa kuambiwa "Sema",Kwanini ikawa sema ?Kwa sababu ukiambiwa sema ina maana unaujua ukweli, umeshaushuhudia ukweli, unaishi ndani ya ukweli, huna khofu tena kufa katika ukweli. kwa kuwa ushaujua ukweli siku zote upo na kwenye Ufalme wa Mwenye enzi Mungu hakuna lugha ila kuna shuhuda, Sasa kwa yule Mwenye kujua au kushuhudia ukweli anaambiwa wafikishie ujumbe huu wale wasojua au wasofahamu, ufanye nini?, Uwajulishe haya"Sema hivi" Ewe Mollah Wangu uliyemiliki Ufalme wote, ikitajwa kumiliki wenye Ufahamu mdogo wanadhani na yeye pia Mfalme kwa hiyo wanaanza kuuhusisha Ufalme huo Miliki na (Imagination)zao labda yuko hivi au vile, kumbuka hapo imetumika lugha ili kuwasiliana na wewe na hizo fahamu zako juu ya tendo hilo la Ufalme.
Ewe Mollah Mwenye kumiliki huo Ufalme wa kila kitu, Uwe Ufalme wenyewe wa Vinyama au Wanaadamu au kundi la majini, basi Wewe ni Mwenye kumpa huo "Uongozi"(Ufalme)umtakaye, Uwe Ufalme au Uongozi huo kwenye (Family)au kwenye Kabila, au Ufalme wa Nchi wa kuwaongoza watu, basi Wewe Unamchagua umtakaye awe Kiongozi kwa njia unazozijua wewe katika sehemu au pahala hapo, Na humuondoshea Ufalme huo Umtakaye na haya yote yamo kwenye uwezo wako.
Sasa nini Kitatokezea iwapo kuna baadhi ya Watu Wenyewe watapinga au kukataa au kumuondosha kwa nguvu yule ulomridhia wewe? Nini Dalili zake?, Tunafahamu Wewe ni Mwenye Uweza wa kila kitu, na si mwenye kushindwa katika jambo lolote, lakini pia tunatambua umetupa Wanaadamu Uhuru au uwezo wa kujiamulia tunavyotaka wenyewe(Hiyo ndio Democracy), ila umetuwekea Shuruti ikiwa uamuzi huo ni wa makosa utatuadhibu, na ukiwa katika Matakwa na maridhio kama ulivyopanga wewe basi umetwambia katika hiyo aya hapo juu(Kheri imo mikononi mwako).
Ilipotaja aya kuwa Kheri imo mikononi mwake ndipo ilipoachia huo Uhuru yakwamba kama kikundi au kundi au Mtu pekee kakubali kuridhia anavyopanga na kutaka yule ambaye kamiliki kila jambo, na kwa njia ya (Huria kabisa)ambayo ni ridhaa ya kila mmoja wenu kukubali, anakutieni mapenzi na nyinyi waja wake kulikubali lile ambalo kakuchagulieni ili akupeni hiyo kheri, mkitokezea kuupinga Ufalme wa Mwenye enzi Mungu nini kinatokezea?

UFALME WA MUNGU PART 2
Asalaam Aleiykum
Nini Kinatokezea?
Yanatokezea Madhara makubwa iwe kwenye Nchi, Jamii, mpaka kwenye familia au Kikundi mpaka mtakapo kaa sawa na kukubali maamuzi ya Mollah wenu, Mpaka mrudi katika njia alopanga yeye Mollah Mwenye kumiliki, lakini iwapo mtaendelea na Ubishi basi maangamizi yake yanakua makubwa kwa wale wote wenye kushabikia uvunjifu huo wa amri ya Mwenye enzi Mungu, ndio utaona wenye kufaidika wachache sana, na wenye kuumia zaidi ni wale wenye kusimamia na kuutetea udhalimu huo hali zao zinakua ni duni kabisa, huwaburura na vizazi vyao katika hali hiyo ikawa Nchi au kijiji kimeathirika vibaya sana kutokana na hizo dhuluma zinazotendwa.
Aya inaendelea kusema "Humtukuza"amtakaye utaona wale walodhulumiwa au kukiri amri ya Mwenye enzi Mungu ndio wananyanyuliwa kimaisha japo wapo katika Mji huo huo, na ama wale wenye kushiriki kupinga amri ya Mwenye enzi Mungu, aya inasema" humdhalilisha amtakaye"hufanywa watu hao hali ya chini, hudhalilishwa wakapita kuomba huku na kule, huteremkiwa na umasikini mkubwa, Shida na Maradhi, mashaka ya maisha na kila aina ya dhiki, Na hupewa adui yao ndio kuwa Mfalme wa kuwamiliki na kuwatesa kwa njia ya dhahiri au kwa siri, na hautopatikana ufumbuzi mpaka mridhie Matakwa ya Mwenye Kuumiliki huo Ufalme.
Na Yeye ndie humtukuza kwa Ufalme wa Cheo katika hii dunia na huko akhera. Msije mkahadaika kuwaona wale wenye kupinga amri za Mwenye enzi Mungu wanafuraha, hao hawana furaha na wao wanajua kwenye nafsi zao moto unawaka lakini hawajui vipi watauzima, mtaona kwenu wanapendeza kumbe ndani wanateketea.
Basi ikiwa swali zima na makusudio yake ya Ufalme huo yamekuingia ndani ya fahamu yako, sasa wacha tutembelee maajabu mengine ya huo Ufalme upate maarifa ya kuufahamu.
تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَىَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَىِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ۬
Huuingiza usiku katika mchana, na huingiza mchana katika usiku, Na hutoa aliye hai katika asiye uhai,Na hutoa Mfu katika aliye hai, Na humpa Riziki umtakaye bila hesabu.
Sasa Zama katika maajabu haya ili upate kujua nani Mwenye kumiliki hivyo vyote, Jambo la kwanza lazima kulifahamu hivi viwili vyote vipo, na vinaishi kama wewe unavoishi, kwani wewe si unajua tegemeo letu lilivo kuhusu Jua na huu Usiku, maajabu haya mawili kwa nje utaona kimoja kikija tunaamka na kufanya kazi na cha pili kikifatia tunakwenda kulala, lakini ushawahi kwenda (Deep)kwenye viwili hivyo?.
Endelea Part 3

UFALME WA MUNGU PART 3
Asalaam Aleiykum
Unapotaka kuviangalia viwili hivi vifanyavyo kazi zake inabidi kwanza tukujulishe vipi maneno hayo ya kuingizwa usiku ndani ya mchana na mchana ndani ya usiku, Na kwanini ikawa unaingizwa? (Ametukuka yule ambaye anakimiliki kila kitu kwenye Ulimwengu huu) kwanini ikatumika lugha hiyo ya kuingizwa, ili usije kufanya tena mzaha na Uwezo wa Mwenye enzi Mungu na kupinga amri zake, nakuchukua na kukufahamisha mfano ambao utaanzisha muamko kwenye akili yako, kama vipi? Chumba kikiwa kiza ukiingiza Taa, kiza kinafanya nini? kinatoweka, lakini swali la kujiuliza kinakwenda wapi? ndio maana nikakwambia viwili hivyo vyote vipo na vinaishi kama unavyoishi wewe, unachotakiwa ni kufanya utafiti wa Kidini ukutane na viwili hivi kimoja baada ya chengine, kwanini nikasema hivyo kwa sababu viwili hivi havikutani vinapishana, lakini havikutani. (Na Mfano huo huo kwa wale wenye ubishi kuwa labda Moto wa Jahannam hakuna nawaambia watizame Moto wa kibiriti mwanzo unakua haupo ukiwasha tu mara huo, unatokezea wapi?lazima ujiulize huu moto kuna sehemu unajificha? hayo ni maswali ya changa moto nakupa uyafanyie kazi usisubiri kila kitu nikuletee mezani ukisome).
Naam kuyataka kuyajua mawili hayo itakubidi ukashuhudie mwenyewe vipi vinaingizwa viwili hivyo katika nyakati mbili yaani kwenye Sala ya Magharibi kuna tukio linatokea ambalo huwa mchana(Light) ushaondoka na Usiku haujaingia(Dark) ukiweza kushuhudia tukio hilo kwa muono wa ndani kabisa utajua vipi Ufalme wa Mwenye enzi Mungu unavofanya kazi yake.
Na Jengine ni hili la kutolewa Roho ukawa unaishi kwenye Umauti au Kupewa Roho ukawa unaishi kwenye Uhai ni la kukujulisha kuwa wewe unapita katika sehemu hizi mbili ambazo hazikutani na kama ukiweza kulifanyia kazi hilo ukajua siri iliyopo hapo basi utakuwa mwenye kufaulu(Katika hili sitaki kueleza kwa kirefu kutokana na hatari zake) ila nasema baina ya Uhai na Umauti ni mpito, katikati kuna kitu hapa ambacho siri yake utakutana nayo Mwenyewe siku Mauti yatakapowasili kwako, kwa hiyo jua kufa utakufa lakini haitakua mwisho wako, kwa hiyo usiogope sana ukaanza kuomba dua za Mungu ninusuru na kifo wakati yeye ndiye aliyeumba viwili hivyo na wakati wetu ukifika sote lazima tuondoke, lazima ulivue hilo guo la (Body) yako na urejee Nyumbani.
Namalizia kwa kusema huyo Mwenye kumiliki hayo yote ndiye pia Mwenye kumiliki hiyo Riziki na humpa amtakaye pasi na hesabu kwa kadir na kima anachotaka yeye,(Usije ukaona hee mbona mafuta arabuni hayakauki) hivyo ndivyo Uwezo wa Mwenye enzi Mungu ufanyavyo kazi zake,Na kwa Mwenye enzi Mungu akitaka kumpa mtu hakuna hesabu, hakai akasema labda hichi, au hivi humiminia amtakaye pasina na hesabu,ila hesabu tunazo sisi ndio maana hatupewi kutokana na khofu zetu, Lakini tukiondoa khofu ya ufukara, khofu ya kifo tutapewa bila ya hesabu.

Subscribe to:
Posts (Atom)