Asalaam Aleiykum
Unapotaka kuviangalia viwili hivi vifanyavyo kazi zake inabidi kwanza tukujulishe vipi maneno hayo ya kuingizwa usiku ndani ya mchana na mchana ndani ya usiku, Na kwanini ikawa unaingizwa? (Ametukuka yule ambaye anakimiliki kila kitu kwenye Ulimwengu huu) kwanini ikatumika lugha hiyo ya kuingizwa, ili usije kufanya tena mzaha na Uwezo wa Mwenye enzi Mungu na kupinga amri zake, nakuchukua na kukufahamisha mfano ambao utaanzisha muamko kwenye akili yako, kama vipi? Chumba kikiwa kiza ukiingiza Taa, kiza kinafanya nini? kinatoweka, lakini swali la kujiuliza kinakwenda wapi? ndio maana nikakwambia viwili hivyo vyote vipo na vinaishi kama unavyoishi wewe, unachotakiwa ni kufanya utafiti wa Kidini ukutane na viwili hivi kimoja baada ya chengine, kwanini nikasema hivyo kwa sababu viwili hivi havikutani vinapishana, lakini havikutani. (Na Mfano huo huo kwa wale wenye ubishi kuwa labda Moto wa Jahannam hakuna nawaambia watizame Moto wa kibiriti mwanzo unakua haupo ukiwasha tu mara huo, unatokezea wapi?lazima ujiulize huu moto kuna sehemu unajificha? hayo ni maswali ya changa moto nakupa uyafanyie kazi usisubiri kila kitu nikuletee mezani ukisome).
Naam kuyataka kuyajua mawili hayo itakubidi ukashuhudie mwenyewe vipi vinaingizwa viwili hivyo katika nyakati mbili yaani kwenye Sala ya Magharibi kuna tukio linatokea ambalo huwa mchana(Light) ushaondoka na Usiku haujaingia(Dark) ukiweza kushuhudia tukio hilo kwa muono wa ndani kabisa utajua vipi Ufalme wa Mwenye enzi Mungu unavofanya kazi yake.
Na Jengine ni hili la kutolewa Roho ukawa unaishi kwenye Umauti au Kupewa Roho ukawa unaishi kwenye Uhai ni la kukujulisha kuwa wewe unapita katika sehemu hizi mbili ambazo hazikutani na kama ukiweza kulifanyia kazi hilo ukajua siri iliyopo hapo basi utakuwa mwenye kufaulu(Katika hili sitaki kueleza kwa kirefu kutokana na hatari zake) ila nasema baina ya Uhai na Umauti ni mpito, katikati kuna kitu hapa ambacho siri yake utakutana nayo Mwenyewe siku Mauti yatakapowasili kwako, kwa hiyo jua kufa utakufa lakini haitakua mwisho wako, kwa hiyo usiogope sana ukaanza kuomba dua za Mungu ninusuru na kifo wakati yeye ndiye aliyeumba viwili hivyo na wakati wetu ukifika sote lazima tuondoke, lazima ulivue hilo guo la (Body) yako na urejee Nyumbani.
Namalizia kwa kusema huyo Mwenye kumiliki hayo yote ndiye pia Mwenye kumiliki hiyo Riziki na humpa amtakaye pasi na hesabu kwa kadir na kima anachotaka yeye,(Usije ukaona hee mbona mafuta arabuni hayakauki) hivyo ndivyo Uwezo wa Mwenye enzi Mungu ufanyavyo kazi zake,Na kwa Mwenye enzi Mungu akitaka kumpa mtu hakuna hesabu, hakai akasema labda hichi, au hivi humiminia amtakaye pasina na hesabu,ila hesabu tunazo sisi ndio maana hatupewi kutokana na khofu zetu, Lakini tukiondoa khofu ya ufukara, khofu ya kifo tutapewa bila ya hesabu.
No comments:
Post a Comment