Asalaam Aleiykum
Sasa Kutana na aya inayofundisha athari za Macho na Sababu zake,
(An-Noor aya ya 30)
قُل لِّلۡمُؤۡمِنِينَ يَغُضُّواْ مِنۡ أَبۡصَـٰرِهِمۡ وَيَحۡفَظُواْ فُرُوجَهُمۡۚ ذَٲلِكَ أَزۡكَىٰ لَهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ
"Waambie Waislam Wanaume wainamishe macho yao,(Wasiangalie mambo mabaya), Na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, bila shaka Mwenye enzi Mungu anazo habari za wanayoyafanya".
Wameambiwa pia na Wanawake kwenye aya inayofatia ambayo nishawahi kuizungumzia huko nyuma aya ya (31) leo tunaogelea kwenye hiyo aya ya (30)wacha tupate faida zake ili tukazifanyie kazi.
Hapo katika maelezo hayo kuna mazingatio makubwa hususan ukiwa weye kijana, "Kwanini uangushe macho yako na wala hukuambiwa yafunge ila limetumika neno angusha", Umeambiwa uangushe kwa sababu binafsi yako ndani wewe unachemka, Na huna (Control)uwezo ulopewa ni huo wa kuangusha macho, kwa sababu ukiangusha macho (Connection)inakatika hupati tena mawasiliano, Na kama hupati mawasiliano Akili inatulia na Akili ikitulia ndio unawasili upande wa pili kwenye huo Utakaso(Ucha)Mungu ita upendavyo ukiingia ndio utajua umo kwenye hali gani wakati akili imetulia, kwa mara ya mwanzo utajua vipi utamu wa (Control)ya maisha yako, sasa kabla ya kwenda (deep) wacha tuyazungumze macho na shughuli zake.
Macho ni sawa sawa na kushika au nieseme yana mahusiano ya karibu sana na kushika, Sasa nini tafauti yake? Tafauti yake unaposhika kwa njia ya nje inayoongezeka ni hisia, na huku kushika kwa ndani ambako ndio (Powerful)penye kutumika macho, huku wengi mnajua inakuaje pale unapomtizama Mwanamke au Mwanamme, na vituko vikaanza kutokea ndani ya nafsi yako, Na yule Mwenye kushikwa kwa njia ya kutizamwa vile vile anajua kuwa sasa Nakamatwa bila ya (Idhini yangu) ndio maana kwa yule asoridhia utaona mara matusi au maneno yanamtoka, Nini kimetokezea?.
Kilichotokezea hapo ni mabishano ya Roho wewe unataka kumshika kwa nguvu na yeye hataki, ndio maana utaona tunapeana muda wa kutizamana wa sekunde nne tu, zikizidi hapo kuna jambo linafatia, na kama bado unafanya ukaidi (Jiulize)inakuaje Mtu kapita tu mimi huku ndani navurugika Akili.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment