Sunday, November 1, 2015

UFALME WA MUNGU PART 2

Asalaam Aleiykum

Nini Kinatokezea?
Yanatokezea Madhara makubwa iwe kwenye Nchi, Jamii, mpaka kwenye familia au Kikundi mpaka mtakapo kaa sawa na kukubali maamuzi ya Mollah wenu, Mpaka mrudi katika njia alopanga yeye Mollah Mwenye kumiliki, lakini iwapo mtaendelea na Ubishi basi maangamizi yake yanakua makubwa kwa wale wote wenye kushabikia uvunjifu huo wa amri ya Mwenye enzi Mungu, ndio utaona wenye kufaidika wachache sana, na wenye kuumia zaidi ni wale wenye kusimamia na kuutetea udhalimu huo hali zao zinakua ni duni kabisa, huwaburura na vizazi vyao katika hali hiyo ikawa Nchi au kijiji kimeathirika vibaya sana kutokana na hizo dhuluma zinazotendwa.
Aya inaendelea kusema "Humtukuza"amtakaye utaona wale walodhulumiwa au kukiri amri ya Mwenye enzi Mungu ndio wananyanyuliwa kimaisha japo wapo katika Mji huo huo, na ama wale wenye kushiriki kupinga amri ya Mwenye enzi Mungu, aya inasema" humdhalilisha amtakaye"hufanywa watu hao hali ya chini, hudhalilishwa wakapita kuomba huku na kule, huteremkiwa na umasikini mkubwa, Shida na Maradhi, mashaka ya maisha na kila aina ya dhiki, Na hupewa adui yao ndio kuwa Mfalme wa kuwamiliki na kuwatesa kwa njia ya dhahiri au kwa siri, na hautopatikana ufumbuzi mpaka mridhie Matakwa ya Mwenye Kuumiliki huo Ufalme.
Na Yeye ndie humtukuza kwa Ufalme wa Cheo katika hii dunia na huko akhera. Msije mkahadaika kuwaona wale wenye kupinga amri za Mwenye enzi Mungu wanafuraha, hao hawana furaha na wao wanajua kwenye nafsi zao moto unawaka lakini hawajui vipi watauzima, mtaona kwenu wanapendeza kumbe ndani wanateketea.
Basi ikiwa swali zima na makusudio yake ya Ufalme huo yamekuingia ndani ya fahamu yako, sasa wacha tutembelee maajabu mengine ya huo Ufalme upate maarifa ya kuufahamu.

تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيۡلِ‌ۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَىَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَىِّ‌ۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ۬
Huuingiza usiku katika mchana, na huingiza mchana katika usiku, Na hutoa aliye hai katika asiye uhai,Na hutoa Mfu katika aliye hai, Na humpa Riziki umtakaye bila hesabu.
Sasa Zama katika maajabu haya ili upate kujua nani Mwenye kumiliki hivyo vyote, Jambo la kwanza lazima kulifahamu hivi viwili vyote vipo, na vinaishi kama wewe unavoishi, kwani wewe si unajua tegemeo letu lilivo kuhusu Jua na huu Usiku, maajabu haya mawili kwa nje utaona kimoja kikija tunaamka na kufanya kazi na cha pili kikifatia tunakwenda kulala, lakini ushawahi kwenda (Deep)kwenye viwili hivyo?.
Endelea Part 3





No comments:

Post a Comment