Sunday, November 15, 2015

ATHARI ZA MACHO NA SAUTI PART 1

Asalaam Aleiykum

Nimepokea ombi watu wanataka wanione au kunisikia basi nawatoa wasiwasi huenda wakaniona au wasinione yote yanawezekana, nini haja ya kuniona sababu unataka kujiridhisha nikoje, kweli ndie mie ninoandika au kuna sehemu na (copy)na ku(Paste), wasiwasi umekushika unaona mafundisho ndiyo lakini huyu Mwenye kuandika anavaa vilemba, huyu kweli Sheikh? hali ya wasiwasi ndio inokufanya utake kunijua, basi kabla hujanijua wacha tuingie kwenye darsa hii ya (Athari za Macho na Sauti) ili uchume tunda la faida ambalo utakapo kula huwenda ukaonja ladha ya kufahamu kwa undani utendaji wa kazi wa viwili hivyo.
Utapata Muongozo wa kuepuka mambo ambayo ukiyashiriki huwenda yakakuangamiza, pata faida hii ili iwe silaha yako itakayokupa uwezo wa kujihifadhi Na pengine kuondoka hiyo hamu ya kunijua. 
Kuna msemo maarufu sana unaosema (Every Saint has past and every sinner have a future)Naam maneno sahihi hayo (Kila Walii ana Skeleton wake, Makovu na alama zipo hilo halina shaka, Na wewe Mtenda dhanmbi vile vile unayo nafasi yakua kama huyo Walii) Kwa hiyo usitie wasiwasi kwa lolote ulolifanya kama unataka kutubia basi midamu uhai unao jirekebishe hivi sasa kwa kuzingatia haya nitakayokujulisha,Na hiyo ndio maana ya ile aya isemayo (Msikate Tamaa na Rehma za Mwenye enzi Mungu).
Nini kinachotakiwa kifanyike?, Unatakiwa ufanye marekebisho ya Tabia yako ambayo ndimo vinavoishi viwili hivi Kusikia na Kuona. Leo tunakutana na viwili hivyo ambavyo ndio chanzo cha matatizo yote yanokufanya uangamie, viwili hivyo ni (Macho na Sauti au Kuzungumza) Nimeamua kuvizungumza hivi kwa kuwa kuna Baadhi ya Watu wanakejeli ile hekima ya kuambiwa usitizame mambo mabaya, au usisikize mazungumzo mabaya au kutizama Wanawake au kuzungumza na Wanaume, kuna baadhi ya watu hilo wanalitilia shaka na kuona kuna ukandamizwaji wa aina fulani kwenye (Dini)Basi ikiwa wewe unajiandaa na ushafanya uamuzi wa kuepuka au kujinusuru na (Uzinzi na Uasherati) Mada hii inakufaa.
Endelea part 2


No comments:

Post a Comment